Nchi inajengwa na mwananchi mwenyewe, nashauri waziri kila Mtanzania ana wajibu wa kulipa kodi ili kujenga nchi yake,uangaliwe utaratibu wa day worker au vibarua wa viwandani,migodini,kwenye miradi mbalimbali ya serikali na binafsi nao wanawajibu wa kulipa kodi kama analipwa 5000 kwa siku akikatwa hata 200 inatosha ajira zisizo rasmi zina watu wengi kushinda hata watumishi walio kwenye ajira rasmi, utekelezaji wake ni simple tu kila kiwanda, mgodi, au kwenye mradi wowote mkubwa lazima wawe na rekodi ya vibarua wao walio fanya kazi kwa kila siku na kiasi wanachowalipa na wakati wa kuwalipa wanakata kodi kabisa TRA wapo makini sana hii kazi haiwezi kuwa ngumu kwao, nchi za ulaya viwandani hii imeshazoeleka.
Umeongea vizuri sana na bila shaka wewe ni Mbunge au Mh fulani.
Na umemtaja hapo anayelipwa sh 5000 kwa siku, hii ina maana huyo unayemuongela hapo anapata wastani wa sh 150,000/= kwa mwezi(kama atapata hicho kibarua kwa siku zote za mwezi), akikatwa kinachotakiwa kukatwa labda atabakiwa na sh 140,000 hivi.
Sasa je, kile mnachopata nyie hata baada ya makato bado mnabaki na 140,000?
Hata hivyo hii kwangu sio tatizo kabisa, tatizo kwangu ni namna nyie mnavyomlazimisha kila Mtu aone/afikirie mambo vile mnavyoona nyie kana kwamba wote tupo kwenye Boti moja.
Hivi leo hii ukinipa hicho unacholipwa wewe kwa mwezi nawe upokee 5000 kwa siku unafikiri nitashindwa kuja na mchanganuo kama huo uliotoa hapo?.
Sipingi kabisa Watu kuchangia ujenzi wa Nchi yao, la hasha.....bali naumia sana kumsikiliza Mnafiki anaye assume kana kwamba wote tunapata maumivu sawasawa.
Ningetamani kuona nanyi pamoja na kutuhimiza Wananchi tujitoe basi nanyi pia mtoe vivyohivyo, yaani ikiwezekana nanyi mbakiwe na bajeti kama zetu.....yaani namaanisha mbaki na hiyo 140,000 kwa mwezi.
Sisi huku hata tusipokatwa senti tano bado tunaishia kusomesha Mtoto ST Kayumba ili hali huko hata mkatwe vipi bado Watoto wenu wote Watano wanasoma Feza Boys.
Mnapotutaka tufunge mikanda hebu mmaanishe usoni mpaka mioyoni.