Dkt. Mwigulu, inakuwaje mnatuambia Miradi ya Hayati Dkt. Magufuli inaendeshwa kwa mikopo mikubwa na migumu kuhimilika?

Nchi inajengwa na mwananchi mwenyewe, nashauri waziri kila Mtanzania ana wajibu wa kulipa kodi ili kujenga nchi yake,uangaliwe utaratibu wa day worker au vibarua wa viwandani,migodini.

Kwenye miradi mbalimbali ya serikali na binafsi nao wanawajibu wa kulipa kodi kama analipwa 5000 kwa siku akikatwa hata 200 inatosha ajira zisizo rasmi zina watu wengi kushinda hata watumishi walio kwenye ajira rasmi, utekelezaji wake ni simple tu kila kiwanda.

Mgodi, au kwenye mradi wowote mkubwa lazima wawe na rekodi ya vibarua wao walio fanya kazi kwa kila siku na kiasi wanachowalipa na wakati wa kuwalipa wanakata kodi kabisa TRA wapo makini sana hii kazi haiwezi kuwa ngumu kwao, nchi za ulaya viwandani hii imeshazoeleka.
Tatizo sio kulipa kodi mkuu tatizo hizo hela badala zikafanye vitu vya maana zinaishia mifukoni mwa watu wachache wenye tamaa imagine watu wanalipana mil 400 kwa siku na kigwangala kachota za kutosha kama uzalendo ni kulipa basi zitumike kwa matumizi sahihi sio janja janja
 
Wanapeana zawadi za benzi kwenye birthday hawana habari na wananchi.Hii nchi hiiiiiiii.
 
Hahaha...

Nacheka jinsi ambavyo walioiweka CCM madarakani, sasa wanagundua kuwa walipigwa changa la macho...

CCM piga matukio mazezeta wote ambao huwa wanashtuka baadaye kuwa wamakosea na bado wanaendelea kukosea...
 
Mwenda zake aliacha akikusanya kodi ya shillingi trillioni 1.9,toka ameondoka machi, april makusanyo yamefikia trillioni 1.3,na kwa sa hv hizi mbio za covid zinazoanzishwa tutafikia bilioni mia 800 hadi 900 mwisho wa mwaka.

Wakati katika kila mwezi tunatakiwa tulipie bilioni 700 kwa ajili ya madeni tu.

Mwendazake aliacha trilioni 9 hazina sasa zipo 6.

Kazi iendelee
Nisaidie sehemu naweza pata hizi data zako kama hutojali
 
Madikteta wote hua wanafanana! Kwa waliokuwa makini wote tulijua muelekeo wake na anapotupeleka
 
“Hatujaweka kodi kwenye laini za simu kama ambavyo baadhi ya wananchi wamekuwa wakichanganya, hata kule Bungeni wanachanganya wanasema sasa kila siku itakuwa inakatwa shilingi 10 mpaka 200 kwa hiyo kama ni 200 kwa siku 30 ni shilingi 6000, halafu hata kama hukuweka fedha, siku ukiweka inakatwa kama nipige tafu, hatukuweka hivyo”, alieleza Dkt. Nchemba.

Alibainisha kuwa haimaanishi kwamba shilingi 10 sio mzigo lakini Serikali iliangalia matatizo yaliyopo na kugundua kuwa yanagharimu zaidi, kuliko thamani ya shilingi 10 itakayotozwa kama kodi.

Alifafanua kuwa miradi mikubwa inayotekelezwa nchi ukiwemo wa mradi wa Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere ambao unahitaji zaidi ya shilingi trililioni nne na ujenzi wa Reli ya Kisasa unaohitaji zaidi ya shilingi trilioni 20 ili kukamilika, iwapo fedha zote zitategemea mikopo nchi itapitiliza uwezo wa kukopa na kutokukopesheka hivyo ushiriki wa wananchi ni muhimu.

My Take:
Leo mmeamua kutuvisha zigo la kujenga Reli na Bwawa la Stiegglers kupitia simu zetu wakati mlituambia fedha ipo na mipango ilikuwa tayari mezani. What went wrong?? (In Dk Mpamire`s voice).
Mbona unabebweshwa vigo la kununua chanjo ya Covid? Tulia sindano ikuingie
 
Serikali ya ccm inaongoza nchi kwa kywaomgopea watanzania. Tuliambiwa miradi yote inajengwa kwa pesa za kodi zetu yaani pesa za ndani. Lakini leo anasimama waziri anatuambia ni mikopo inatumika kuijenga miradi. Marehemu na hawa wa sasa nani anawadanganya watanzania?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Aliyedanganya kwa kusema fedha zipo au tunatumia fedha zetu za ndani hayupo tena...
 
Ninaupeo kidog wa elimu ya uchumi na wazo la Mhe. Nchemba ni la kitoto kibixa kwasababu mtu ukiweka vocha palepale unakatwa indirect tax na Leo hii unakuja na wazo la kunitoza Tsh 10 maana ake hapo ninalipa tax twice na kitu kingine watanzania wengi ni wapo maisha ya chini xana yaan mtu anahagaika kuitafuta 1000 aweke vocha siku nzima alf wonderful enough unamkata 10 maana ake anabaki na Tsh. 990 xaxa Apo anaweka kifurushi kipi tuelezane tu ukweli .
Yaan unaisaka bikira kweny odi ya wazazi huzi ni akili uchwala .
Yaleyale ya head tax ya mkapa yanarundi teni in modified form .
"HII NCHI NGUMU HII"
Kubaliane tutakuwa tunaweka vocha za 1500 ili wakikata inabaki ya kujiuga kifurushi Alf ile Mia 490 potelea mbali na je serikali haiona xaxa ni loss kubwa unaenda kujitokesa kwa watanzania amby ni kupoteza 490 hii itaasiri xana kwa watumiaji wa voda make voda ukiunga kifurushi centi zinazobakia Kama sehemu ya vocha wanazitumia kwanza ndo wanaenda kweny kifurushi this is a big loss .
Hawa watu wawili waliplay a big role in building a nation ,
1. Mkapa alitoa head tax ambayo ndo
imerundi in form of cm.
2. JPM Alifanikiwa kuweka infrastructure nzuri
Kwa kukusanya tax zinazoeleweka na kwa
Kuzingatia uchumi wa watu wake .
Mkapa, JPM pumzike salama kwa kweli mwanga wa bwana uwamulikie siku zote Amina .
Tanzania kila mtu ni mpiga .
 
Mwenda zake aliacha akikusanya kodi ya shillingi trillioni 1.9,toka ameondoka machi, april makusanyo yamefikia trillioni 1.3,na kwa sa hv hizi mbio za covid zinazoanzishwa tutafikia bilioni mia 800 hadi 900 mwisho wa mwaka.

Wakati katika kila mwezi tunatakiwa tulipie bilioni 700 kwa ajili ya madeni tu.

Mwendazake aliacha trilioni 9 hazina sasa zipo 6.

Kazi iendelee
Tutajua hatujui, muda si mrefu...Utakuta hawa hawa leo wanaomtukana watakuwa wakwanza kutukumbusha jinsi alivyoweza kupeleka miradi usiku na mchana na kufungua kwa mbwembwe iliyokamilika within time frame!
 
Yaa kwa vipande vyote,Magu ni kimeo sana bora hizi pesa ambazo tayari zimewekwa kwenye sgr ambayo inaweza kukamilika 2030 zingewekwa kwenye barabara tungeshafika mbali sana
Acha mawazo mgando wewe, kwa hiyo unaona 2030 ni mbali sana? SGR na Bwawa la umeme Rufiji ni miradi muhimu sana itakayoboost uchumi wa nchi.
 
“Hatujaweka kodi kwenye laini za simu kama ambavyo baadhi ya wananchi wamekuwa wakichanganya, hata kule Bungeni wanachanganya wanasema sasa kila siku itakuwa inakatwa shilingi 10 mpaka 200 kwa hiyo kama ni 200 kwa siku 30 ni shilingi 6000, halafu hata kama hukuweka fedha, siku ukiweka inakatwa kama nipige tafu, hatukuweka hivyo”, alieleza Dkt. Nchemba.

Alibainisha kuwa haimaanishi kwamba shilingi 10 sio mzigo lakini Serikali iliangalia matatizo yaliyopo na kugundua kuwa yanagharimu zaidi, kuliko thamani ya shilingi 10 itakayotozwa kama kodi.

Alifafanua kuwa miradi mikubwa inayotekelezwa nchi ukiwemo wa mradi wa Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere ambao unahitaji zaidi ya shilingi trililioni nne na ujenzi wa Reli ya Kisasa unaohitaji zaidi ya shilingi trilioni 20 ili kukamilika, iwapo fedha zote zitategemea mikopo nchi itapitiliza uwezo wa kukopa na kutokukopesheka hivyo ushiriki wa wananchi ni muhimu.

My Take:
Leo mmeamua kutuvisha zigo la kujenga Reli na Bwawa la Stiegglers kupitia simu zetu wakati mlituambia fedha ipo na mipango ilikuwa tayari mezani. What went wrong?? (In Dk Mpamire`s voice).
Mkuu sisi wengine tulijua tu kwamba huko mbeleni Mkuu bubu atasema, kiziwi atasikia, mwenye macho ataona na wenye pua atanusa, it was just a matter of time.
 
Tatizo Magufuli alikua mlaghai. Huu utaratibu ulitakiwa uwepo tangu mwanzo. Wananchi washiriki kujenga inchi yao. Kwa uongo wa magufuli kwamba miradi inajengwa na fedha za ndani ilibidi waumie wachache kwa kuporwa fedha zao na kunambikia watu kesi za uhujumu uchumi, kudhurumu haki za wafanyakazi , uporaji kwwnye beural de change nk
 
Ipigwe Harambee ya wazi itakayowashirikisha wenzetu waliounga mkono juhudi, wabunge, wazalendo wa Twitter na makundi kama hayo. Watakapoishia waliobaki watazajazia
 
Back
Top Bottom