Dkt. Mwigulu, inakuwaje mnatuambia Miradi ya Hayati Dkt. Magufuli inaendeshwa kwa mikopo mikubwa na migumu kuhimilika?

Dkt. Mwigulu, inakuwaje mnatuambia Miradi ya Hayati Dkt. Magufuli inaendeshwa kwa mikopo mikubwa na migumu kuhimilika?

Nchi inajengwa na mwananchi mwenyewe, nashauri waziri kila Mtanzania ana wajibu wa kulipa kodi ili kujenga nchi yake,uangaliwe utaratibu wa day worker au vibarua wa viwandani,migodini.

Kwenye miradi mbalimbali ya serikali na binafsi nao wanawajibu wa kulipa kodi kama analipwa 5000 kwa siku akikatwa hata 200 inatosha ajira zisizo rasmi zina watu wengi kushinda hata watumishi walio kwenye ajira rasmi, utekelezaji wake ni simple tu kila kiwanda.

Mgodi, au kwenye mradi wowote mkubwa lazima wawe na rekodi ya vibarua wao walio fanya kazi kwa kila siku na kiasi wanachowalipa na wakati wa kuwalipa wanakata kodi kabisa TRA wapo makini sana hii kazi haiwezi kuwa ngumu kwao, nchi za ulaya viwandani hii imeshazoeleka.
Sisi sio kwamba hatutaki kuchangia,tatizo ni viongozi kutudanganya utazani hayo madeni watalipa wao.
 
Sio kwamba hatutaki kuchangia,tatizo ni viongozi kutudanganya utazani hayo madeni watalipa wao. Wenye nchi ni sisi lazima tuambiwe ukweli.
 
Kat
Mwendazake alikua mtu wa fix sana
Katuachia deni kubwa sana la Trillion 31 katika kipindi cha miaka 5 tu,inakaribia jumla ya madeni yalioachwa tokea Raisi Nyerere, Mwinyi,Mkapa,Kikwete .
Wengi wetu tuliamini tunajega mega projects kutumia mapato ya kodi zetu ,kumbe ni vice versa.
Lakini kuna wakati Zitto akiwa mbunge alionya kuhusu kupanda ghafla kwa deni la taifa.
Na wabunge walio wengi wa CCM wakapuuzia,Magufuli alijua kucheza na akili za Watanganyika,tuandike katiba mpya,tuachane na one man show.
 
sisi tunajenga miradhi yetu kwa fedha za ndani, hatukopi sehemu... ni mwendo wa CASH!
 
Brain wash,ni siraha hatari, kila siku unaambiwa kitu kile kile TUNAJENGA SGR KWA PESA ZETU ZA KODI,TUNAJENGA BWAWA LA NYERERE KWA PESA ZETU ZA NDANI,WAKANDARASI WAKO SITE, TUNAFANYA HAYA NDUGU ZANGU KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU.TUMECHEZEWA MNO,TUMECHELEWA MNO.
Na hayo maneno yanapambwa na takwimu za gharama zake,ukubwa wake,muda wa kumaliza mradi,tena anayesema ni Raisi wa Jamhuri. Katupata wengi na tulimwamini.R.I.P mjomba Magu.
Na pia kiwango cha ujinga walicho kiingiza vichwani mwa watu ni sawa na maradhi ya yasiyo na Tiba Tungejitambua japo robo haya yasingetokea
 
Mwenda zake aliacha akikusanya kodi ya shillingi trillioni 1.9,toka ameondoka machi, april makusanyo yamefikia trillioni 1.3,na kwa sa hv hizi mbio za covid zinazoanzishwa tutafikia bilioni mia 800 hadi 900 mwisho wa mwaka.

Wakati katika kila mwezi tunatakiwa tulipie bilioni 700 kwa ajili ya madeni tu.

Mwendazake aliacha trilioni 9 hazina sasa zipo 6.

Kazi iendelee
Alikuwa anakusanya kodi,au alikuwa anaingia kwenye account za watu anapora fedha?
 
“Hatujaweka kodi kwenye laini za simu kama ambavyo baadhi ya wananchi wamekuwa wakichanganya, hata kule Bungeni wanachanganya wanasema sasa kila siku itakuwa inakatwa shilingi 10 mpaka 200 kwa hiyo kama ni 200 kwa siku 30 ni shilingi 6000, halafu hata kama hukuweka fedha, siku ukiweka inakatwa kama nipige tafu, hatukuweka hivyo”, alieleza Dkt. Nchemba.

Alibainisha kuwa haimaanishi kwamba shilingi 10 sio mzigo lakini Serikali iliangalia matatizo yaliyopo na kugundua kuwa yanagharimu zaidi, kuliko thamani ya shilingi 10 itakayotozwa kama kodi.

Alifafanua kuwa miradi mikubwa inayotekelezwa nchi ukiwemo wa mradi wa Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere ambao unahitaji zaidi ya shilingi trililioni nne na ujenzi wa Reli ya Kisasa unaohitaji zaidi ya shilingi trilioni 20 ili kukamilika, iwapo fedha zote zitategemea mikopo nchi itapitiliza uwezo wa kukopa na kutokukopesheka hivyo ushiriki wa wananchi ni muhimu.

My Take:
Leo mmeamua kutuvisha zigo la kujenga Reli na Bwawa la Stiegglers kupitia simu zetu wakati mlituambia fedha ipo na mipango ilikuwa tayari mezani. What went wrong?? (In Dk Mpamire`s voice).
Wasimamishe ujenzi.
"Rome was not built in a day"

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Kodi ya Railway Levy haitoshi au kazi yake nini??
Railway Levy inahusisha maingizo ya Magari, je hayo magari yanayoingizwa yanaweza gharamia?
Hujui kwa mwaka magari yanayonunuliwa Tz hayafiki 100000?
 
Huku walisema wanatekeleza kwa cash, leo imekuwaje tena? wapuuzi sn hawa.
Ndicho wanacho maanisha,kwani serikali ina biashara gani kwamba itafanya kwa fedha zake,unapoambiwa hawahitaji kukopa zaidi maana yake pesa hiyo itapatikana kwa njia ya kodi na hiyo ndio maana yapesa zetu wenyewe. Kwa maana nyingine pesa za serikali ni fedha inayotokana na kodi,gawio na tozo hiyo ndio biashara ya serikali.
 
Nchi inajengwa na mwananchi mwenyewe, nashauri waziri kila Mtanzania ana wajibu wa kulipa kodi ili kujenga nchi yake,uangaliwe utaratibu wa day worker au vibarua wa viwandani,migodini.

Kwenye miradi mbalimbali ya serikali na binafsi nao wanawajibu wa kulipa kodi kama analipwa 5000 kwa siku akikatwa hata 200 inatosha ajira zisizo rasmi zina watu wengi kushinda hata watumishi walio kwenye ajira rasmi, utekelezaji wake ni simple tu kila kiwanda.

Mgodi, au kwenye mradi wowote mkubwa lazima wawe na rekodi ya vibarua wao walio fanya kazi kwa kila siku na kiasi wanachowalipa na wakati wa kuwalipa wanakata kodi kabisa TRA wapo makini sana hii kazi haiwezi kuwa ngumu kwao, nchi za ulaya viwandani hii imeshazoeleka.
Haswaaa umepiga nakos ya utosi watanzania tulizoeshwa kutembeza bakuri matonya staili,hatupendi kuwajibika kwa maendeleo yetu wenyewe. LAZIMA TULIPIE MAENDELEO YETU HAKUNA NAMNA.
 
Hivi Ni lazima mjenge hio reli yote saivi

Hilo kipande Cha moro dar Hadi leo hakijakamilika bado mnaenda mwaga hela kwengine .

Mtaifanya hii nchi ifilisike
 
Back
Top Bottom