nduza
JF-Expert Member
- Feb 7, 2019
- 1,595
- 2,503
Sijapinga wataalamu wasiajiriwe na kuwepo kwa hawa watu watatu hakujazuia wataalam kuajiriwaMkuu Watu wanalipa Kodi Kwa Kuwa Influenced? How Comes? Hili la Mobeto, Kumwembe, Samata Ni Aibu Sana Kwa Vijana wanaosota Vyuoni Wakisomea Kodi. Tungekua Na Viongozi ambao Wako Serious na Majukumu yao, Hizi Nafasi zingeshindaniwa na wanafunzi IFM, TIA, CBE, nk
Mtaalamu aliyetoka chuo atakaa wapi ili atoe elimu kwa maelfu ya watu kwa wakati mmoja au atembelee ofisi kwa ofisi mpaka lini?
Hamisa akipost siku moja watu laki mbili wameona
kazi ni lazima ihusishe watu wa aina mbalimbali hawa pia wana nafasi yao
Kazi zinategemeana huwezi kuhitaji wataalam tu ushawishi pia unatakiwa
Radio station nyingi siku hizi haziangalii sana taaluma bali ushawishi lengo lao ni biashara zaidi watu wasio na taaluma za utangazaji huajiriwa kwa kuwa tu wanavutia wasikilizaji wengi lakini nyuma yao kuna watu wenye taaluma
Makampuni huandaa matamasha na kualika wasanii kufanya show na kuwalipa hela nyingi kwa sababu gani ushawishi walio nao kuwavutia watu kutumia bidhaa zao
Mambo siyo magumu kiasi hicho dunia imekuwa rahisi sana msishupaze shingo
Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app