Huwenda Mwigulu yupo sahihi sana
Hawa ni watu wenye influence kwenye jamii
kuwatumia hawa inafanya elimu watakayotoa kufikia watu wengi zaidi
Na matokeo yanaweza kuwa mazuri
Mfano mimi ningekuwa ndiyo afisa mwenye taaluma yangu ya maswala ya kodi ningetumia chombo gani kutoa elimu ili iwafikie wengi zaidi ingebidi nitumie gharama kubwa na mda mwingi na huwenda nisingefikia watu wengi kama Hamisa atakavyopost kwenye mitandao yake
dunia imebadilika watanzania hatuhitaji kutumia Maguvu ni akili kidogo na mambo yanaenda
Haihitaji wawe na taaluma hiyo kinachohitajika kutoka kwao ni huo ushawishi walio nao tu watachopewa wao ni semina ya nini cha kusema kuhusu maswala hayo ya kodi mbele ya wananchi
Maswala mengine ya kitaalamu wataalam wapo tu kwaajili hiyo
Watu hupelekea matangazo yao redioni kwa kuwa redio zinasikilizwa na watu wengi ni kitu kimoja na hichi alichofanya Mwigulu big up kwake
Leo kuwa na ushawishi/followers Ni mali ndiyo maana watu wanatangaza biashara kupitia hii mitandao na wanafanya vizuri sana sasa kwanini jambo hilo tu ndiyo liwe baya
Sent from my TECNO KC8 using
JamiiForums mobile app