Dkt. Mwigulu Nchemba ateua wadau watakaotoa elimu ya mlipa kodi; wamo Hamisa Mobetto, Edo Kumwembe na Mbwana Samatta

Dkt. Mwigulu Nchemba ateua wadau watakaotoa elimu ya mlipa kodi; wamo Hamisa Mobetto, Edo Kumwembe na Mbwana Samatta

Hakuna mfanyabiashara asiyejua umuhimu wa "kodi" lakini kodi ni kitu ambacho kinachukiwa na kila mtu duniani, awe ni msomi au kanjanja.

Kodi haijawahi kupendwa na yeyote yule na ndiyo maana inapojitokeza mianya ya kukwepa kodi basi watu huikwepa kodi.

Mwigulu ulitakiwa kuweka nguvu kubwa kwenye kuziba na kupambana na mianya ya ukwepaji kodi.

Swala la kodi siyo la kubembelezana hata kidogo. Wekeni utaratibu ambapo kila mfanyabiashara atakatwa kodi automatically bila ya kufuatana fuatana.
 
Mkuu ebu Toa Elimu Kwenye Hyo last paragraph ya Andiko Lako [emoji120][emoji120]
 
Nina uhakika maneno pekee wanayoyaelewa hao kwenye uwanda wa kodi ni "Lipa kodi kwa maendeleo ya nchi". Kwingine hawafahamu kitu. Hebu waTz tubadilike tuheshimu taaluma za watu.

Kuna mambo yanahitaji hamasa kama Utalii, hamisa na Eddo wapewe ubalozi wa kuhamasisha waTz wakiopo Tz kutembelea vivutio vya kitalii vya TZ, na Samatha apewe ubalozi wa kuhamasisha watu wa nje kuja kutalii Tz. Kwenye kodi Mwigulu atuache kidogo. Tunahitaji sheria na mikakati katika hili.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hao ndo wanaotoa elimu ya walipa kodi?

Mi ndio maana sionagi sababu ya kusoma mpaka nipate PhD maana hata wenye nazo naonaga hawaeleweki nahisi kuna uchawi huko kwenye elimu za juu
Hizo ni Ph.D zinazotokana na njaa ya waalimu wa vyuo vikuu. Nakuhakikishia Mwigulu ana Ph.D ya kulipia. Aliyehangaikia Ph.d. hapa Bongo, akaimaliza hawezi kuwa na udhifu wa kufikiri kiasi hiki. Jamaa hawa wamegundua urafi wa maprofesa. Anajisajili na kutoa pesa za kutosha. Tangu adniko la kwanza hadi la mwisho yeye ni kuandikiwa na kuitwa kuweka sahihi.
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amewateua Mbwana Samatta, Hamisa Mobeto na Edo Kumwembe kuwa mabalozi wa kuhamasisha ulipaji kodi. Mbali na hao amewateua wanasiasa wengine kuwa mabalozi wa elimu ya kodi, ili kuhakikisha wananchi wanalipa kodi bila kushurutishwa.

=========

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya uteuzi wa watu mbalimbali watakaotoa elimu ya mlipa kodi kwa Watanzania wakiwemo

Mbwana Samata, Edo Kumwembe na Hamisa Mobeto.

View attachment 1826377
Katika kutafuta ulipaji wa kodi kwa njia hiari, Mh. Nchemba angejitahidi wizara yake itengeneze mfumo rafiki wa ukusanyaji wa kodi mbalimbali ambao uknaweza kusimamiwa vyema na TRA. Kwanza, wizara yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kodi wangeweza kuisaidia TRA katika kufanya "research & development" ili kupanua wigo wa kodi hapa nchini katika sekta rasmi na ile isiyo rasmi.

Katika suala la "voluntary tax compliance" inabidi uzidi kusisitizwa ili walipa Kodi waone fahari juu ya tozo zao kwa uthibitisho wa uwepo "public services" zinazotolewa na serikali. Ila katika suala la "involuntary tax compliance" hapo panahitajika ubunifu mzuri zaidi ya kutumia njia za kibalozi katika kuhamasisha walipa kodi.

Pakikosekana uhiari wa kulipa kodi maana yake misuli inahitajika ili kumwezesha mlipa kodi mwenye kuweza kuthibitika ana "taxable income" ili apate kulipa stahiki yake ya kodi. Hapo mimi ningemshauri waziri afikirie njia mbadala ya kukusanya kodi kwa njia ya uwakala, yaani "collecting tax via recognizable tax agencies" ambao watapewa nguvu za kisheria kufanya hivyo.

Wakala hao wa kikodi wanaweza kupewa jukumu la kukusanya stahiki ya kodi kwa nyongeza tuseme ya 5% kwa rasilimali zao wenyewe. Ni lazima mstari uchorwe katikati ya uhiari na kukosa uhiari wa kulipa kodi, ili endapo yule mwenye kipato na kustahili kulipa kodi akishindwa kuwajibika ipasavyo wakala hao wakodi wapewe nguvu ya kisheria ya kufilisi mali zake ili kodi ipate kukusanywa.
 
Aisee dah.. inasikitisha sana kwakweli, tuna safari ndefu sana sana, nikiwafikiria kitaa raia wamemaliza chuo wanasota tu, hela zinapelekwa kwa wapaka poda wakatoe elimu ya kodi, kodi kabisa unamteua Hamissa Mobetto akafundishe kodi? Aisee
 
Unamchukua Mohammed Ally unamweka kwa Michael Jackson and vice versa....Catastrophe
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amewateua Mbwana Samatta, Hamisa Mobeto na Edo Kumwembe kuwa mabalozi wa kuhamasisha ulipaji kodi. Mbali na hao amewateua wanasiasa wengine kuwa mabalozi wa elimu ya kodi, ili kuhakikisha wananchi wanalipa kodi bila kushurutishwa.

=========

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya uteuzi wa watu mbalimbali watakaotoa elimu ya mlipa kodi kwa Watanzania wakiwemo

Mbwana Samata, Edo Kumwembe na Hamisa Mobeto.

View attachment 1826377
Sasa Mabwana yuko likizo kwa mwe moja tu unamteua. Sasa hiyo kazi atazifanya lini su ndiyo mwenye nacho huongezewa.
 
Back
Top Bottom