Dkt. Mwigulu Nchemba: Nikimposti mwanangu mnasema "kameshiba dola zetu hako"; kanakutana nazo wapi?

Dkt. Mwigulu Nchemba: Nikimposti mwanangu mnasema "kameshiba dola zetu hako"; kanakutana nazo wapi?

Kwa kweli tunatakiwa kuwaonea huruma wazazi wa Lucas Muwasha Mbwa. Ukisikia mtoto huyu siyo riziki, ndiye huyu. Kila mzazi hutegemea mwanae atakuwa mwerevu, mwenye akili timamu, mchapakazi, mwenÿe busara na mwenye kujitambua, LAKINI ukweli haiwi hivyo. Ukiwa na bahati mbaya unaishia kupata mtoto wa namna ya Lucas Muwasha Mbwa, mtu ambaye hajui hata thamani ya utu na ubinadamu wake. Yupo tayari kusifia hata kinyesi cha mtawala, lakini hata siku moja hawezi kumheshimu hata mzazi wake kwa kufanya mambo yatakayomfanya mazazi wake ajivunie kwa kuwa na mtoto mwenye uelekeo badala ya kuwa chawa mnafiki asiyejitambua.

Hatari sana mkuu kule India watu kama hawa familia inawauwa inaitwa honor killing.
Ni mfumo mbovu wa teuzi za kisiasa ndio zimezalisha wajingawajinga kama hawa wanategemea wasifiesifie hata ujinga ili wateuliwe nafasi za uteuzi mara nyingi watu wa namna hii hawana sifa wala vigezo vya kuteuliwa kwa hiyo mbinu wanazotumia ni kusifia sifia bila hata kuona haya ikibidi hata bila kujali utu wake
 
Waziri kilaza yani tupende vinavyozalishwa kwetu wakati nyie kutwa mna maduka yanu ya spea manaagiza uchinani kila uchwao toka muingie 2015 ni viwanda vitatu vya kueleweka bagamoyo sugar na kile chakuunganisha magari tena kile sio kiwanda ni assembling point hakizalishi yeye kinaunganisha kwa sio kiwanda mnajitapa sana uchumi umekua may be umekua mfukoni mwenu ila huku down pagumu sana leo hui Tz hatuna hata kiwanda cha kutengeneza t-shirt za kueleweke yani mnakimbilia uchinani kwenye low grade mkija huku mje mtupige pesa ndefu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Waziri wetu wa Fedha, Mheshimiwa Daktari Mwigulu Lameck Nchemba,Mchumi Daraja la Kwanza kutoka UDSM na aliyewahi kufanya kazi BOT na ambaye wengi hupenda kumwita Mr Clean, kutokana na uadilifu wake pamoja na uzalendo wake kwa Taifa letu.

Ameonyesha kusikitika na kusikitishwa sana na malalamiko ya watanzania mitandaoni yasiyo na msingi wala ukweli. Ametolea mfano kuwa anasikitika sana pale anapoona hata anapoposti picha ya mwanae na kumtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa, wanatokea watu wanasema "Ameshiba" Dola Zao.

Akasema kuwa, sijui wapi ambako mwanae anakutana na hizo Dola. Amewataka watanzania kuwa wazalendo kwa Taifa letu nakupenda vitu vinavyozalishwa na viwanda vyetu vya ndani.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Pia, Soma: Matokeo ya uchaguzi CCM chipukizi: Mtoto wa msanii Shetta na Mwigulu Nchemba wang'ara
 
Attachments

  • IMG_5563.jpeg
    IMG_5563.jpeg
    128.8 KB · Views: 1

Lipeni pesa za wakandarasi.
 
Back
Top Bottom