Dkt. Mwigulu: Pato la kila mtu nchini lafikia milioni 2.8

Dkt. Mwigulu: Pato la kila mtu nchini lafikia milioni 2.8

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema mwaka 2022 Pato Ghafi la Taifa lilikuwa TZS trilioni 170.3 ikilinganishwa na TZS trilioni 156.4 mwaka 2021.

Hivyo, kutokana na idadi ya watu Tanzania Bara, Pato la Taifa kwa Mtu kwa mwaka 2022 ni TZS milioni 2.844 ikilinganishwa na TZS milioni 2.708 mwaka 2021.

Kiasi hicho ni sawa na dola za Marekani 1,229.1 mwaka 2022 kwa mtu kwa mwaka ikilinganishwa na dola za Marekani 1,173.3 mwaka 2021.

Hali hii inaendelea kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ngazi ya chini.
 
Langu ni 890000 sijajua hiyo 2.8 anaipataje
 
Huu upunguwani ndo sijawahi kuukubali. Unachukua hela za Mwigulu, za akina Bakhresa na Mo Dewji unajumlisha na za kwangu unatafuta wastani alafu ndo pato la kila mtanzania. This is a bourgeous perspective. 90% ya uchumi unashikiliwa na 10% ya watu. alafu mnakuja kutudanganya na maneno ya kwenye khanga
 
Kwa ripoti kama hizi ndo unakuja kuona bora kina Dr Msukuma na Kishimba. Kwenye makaratasi ni sawa ila kiuhalisia on the ground hiyo hela ni nyingi kwa walio wengi. Wastani wa Tsh 230k kwa mwezi wakati kuna viwanda vinalipa watu Tsh 4000 kwa siku.

Kule vijijini kuna jamaa wanafanya kazi kwa mama muuza pombe mshahara wao ni pombe. Mwigulu na wataalamu wenzake nawaheshimu sana ila wajitahidi kuja na mikakati itakayotupa ripoti zenye uhalisia. Wasiwe kama wale wanaharakati wa haki za wanyama wanaojali maisha ya wanyama kuliko binadamu.
 
Deni huko limegawanyika, mara la Taifa mara la serikali....mkishtuka, tumepigwa mnada!

79trln, 93trln? Ongezeko la 13% ni kutoka wapi kwenda wapi?

Kukopa zaidi ta 10trln kwa 6months, zimefanya nini?

Achana na pato la mtanganyika, 70% wanaishi chini sh 2000 kwa siku.
 
Ukichanganya na gap ya walionacho na wasionacho kuwa kubwa na middle income ku-shrink..., Kwa hii path tunayokwenda kila pato linavyopanda na maisha ndio yataendelea kuwa magumu kwa wengi...

99% ya wealthy inashikiliwa na chini ya 1%
 
Kama nchi asilimia 23 ni wanafunzi
Asilimia 25 ni watoto
Asilimia 5 ni wazee
Walipa kodi ni chini ya milioni 5 hapo wategemea nini?

Watanzania hawapendi kusoma, kufanya kazi
Ila kupiga Domo,kulalamika,kulaumu na umbea 😁😁

Ona hizi takwimu za ujuaji wa kisekta yaani biashara na Kilimo zimedumaa
20230615_135458.jpg
 
Ukichanganya na gap ya walionacho na wasionacho kuwa kubwa na middle income ku-shrink..., Kwa hii path tunayokwenda kila pato linavyopanda na maisha ndio yataendelea kuwa magumu kwa wengi...

99% ya wealthy inashikiliwa na chini ya 1%
Na maskini wengi wako Vijijini ambako Serikali haiwasaidii Kwa lolote licha ya kuwa kwenye shughuli ya Kilimo ila imepuuzwa..

Wale wa Mjini ni machinga nao wamepuuzwa
 
Back
Top Bottom