Uchaguzi 2020 Dkt. Mwinyi: Wajumbe wa Zanzibar waliotupigia kura ni 68 hata kama ni kweli wenzangu walipata 35 basi na mimi nilipata 33

Tujiandae saa tatu kamili kutazama mahojiano mahsusi Kati Dr. Hussein Mwinyi(Rais mtarajiwa wa Zanzibar) na Tido Muhando UTv(Channel 108 azam tv)
 
Fuatilia mahojiano mahsusi Kati Dr. Hussein Mwinyi(Rais mtarajiwa wa Zanzibar) na muandishi mahiri sana Tido Muhando UTv(Channel 108 azam tv)

Twende pamoja majibu ya maswali yote tutayapata hapa.

Karibuni sana
 
Dr. Mwinyi anajua kujieleza sana kwa kifupi na kwa kueleweka kabisa.

Anaonekana mtu makini sana kwenye kuzungumza
 
Kwamba mwanaccm kutoka Bukoba anachagua mtu anaeenda kuongoza nchi ya Zanzibar!! shida ni kua unatetea ujinga lakini kibaya zaidi Mh Rais/m.kiti akasema itenguliwe ili wananchi wa Z bar ndo wafanye uchaguzi pekeyao napo utatetea na kusema sawa.
Kwani hawa wazanzibar wanatokea mbinguni? Si wapo kwenye chama na Serikali. Sifa na ubora wao si unajulikana, sasa wanachama wote wakichagua mgombea wao kwa kuzingatia sifa zao kuna shida gani?

Hiki chama kiliungana kikawa chama kimoja, lazima mambo yake yafanyike kwa pamoja. Otherwise labda Afro Shiraz irudi iwe inachagua wagombea wake. Lakini kwasasa utaratibu ndo huo.
 
Mwinyi amesema hata kama ni kweli wenzake hawakupigiwa kura na wajumbe wa bara kitu ambacho hakiamini, bado yeye naye atakuwa amepata kura 33 kutoka Zanzibar.
 
Mwinyi ni bonge la rais Zanzibar hawatajutia
 
Asianze tabia ya Trump ya kujisifia na kulalamika hata pasipokuwa na ulazima. Maneno hayo hayakutakiwa kutolewa na yeye.
 
Si vibaya majina ya wajumbe wa Zanzibar yakiwekwa hapa ili tujirodhishe na huo utetezi. Vinginevyo wanaosema ni wajumbe 35, au yeye anayesema 68, wote ni waongo.
Kweli kabisa.
Hoja yako ni ya msingi sana.
Thanks mkuu.
 
Tunayo list yote, ni wajumbe 35 tu waliotoka Zanzibar, kama alipata kura 33 kutoka zanzibar basi hizo vote zilienda zikiwa zipo kwenye ballot box, na akileta ubishi tutaweka list yote.
 
Wanzanzibar muungeni Maalim mchukue nchi yenu tumewachoka huku Bara
 
Nmesoma meseji karbia zote lkn bado sijapata jibu la kwel, wajumbe walikua 68 au 35?. Km walkua 35 kunaulakini mkubwa sn lakini km walkua 68 inaonekana wazanzibar wanamkubali mwinyi.
 
Vijana wa lumumba mmeanza propaganda tena? Wajumbe wa Zanzibar walikua 35 na Bara 129, yeye alijipatia kura zote 129 kutoka bara. Iko hivyo, hata mtoto wangu mdogo hapa amekucheka sana. Unakwama wapi kwenye mahesabu ya kujumlisha na kutoa tu?
 
Kayasemea wapi haya.. kishajichnaganya.
 
Uliyosema ni kweli kabisa nilimuona Nahodha tangu siku ya uchaguzi amenuna mpaka leo hajacheka kati ya wagombea wote huyu ameumia kweli. Lakini napenda kumfahamisha kwamba duniani hakuna haki akitaka haki basi ataikuta mbinguni akubali yaishe na maisha yaendelee.
 
Hata kujieleza alishindwa maskini!!
 
Wakati wa mahojiano ya jana au juzi anaonekana kutaka kuonesha kuwa yeye alisimama yeye mwenyewe na wala sio kwa kubebwa na baba yake lakini pia na suala la kura alizopata. Naona namna alivyojibu kwa kweli ni aibu tu kwani inaonesha uwezo wake wa kupambanua mambo ni mdogo nikilinganisha pengine na baba yake alivyokuwa.

WaTanzania wote tunajua kuwa Mzee Mwinyi alikuwa mtu wa watu na anapendeka mpaka sasa. WaTanzania pia wanatamani kuwa na kiongozi kama alivyokuwa Mwinyi kwa baadhi ya mambo aliyoyasimamia - mfano kuwapa nafasi na uhuru zaidi - yaani "ruhusa". Kuna tunaoamini Hussein Mwinyi paia anaweza akawa kama alivyokuwa Mzee Mwinyi na tungependa awe hivyo.

Kwa maana hiyo tunavyomwona yeye vile alivyo ni kama tunakumbushwa mema ya Mzee Mwinyi yamerithiwa na Hussein Mwinyi huyu. Sasa anavyokataa kujilinganisha naye hata kidogo tu sidhani kama anapatia sana. Kwani ni dhambi mtu kusema baba yake kwa namna moja au ingine - direct or indirectly - anaweza akawa amechangia yeye kupigiwa kura?. Kwani ni lazima Hussein Mwinyi ajue kuwa baba yake alimpigia debe? Sidhani kama Mzee Mwinyi ilitokea hakumwombea kura kwa mtu hata mmoja mwanae Hussein.

Kuna lile suala la kura 35 pia. Nafikiri Hussein alivyoanza kufafanua kwa kuweka assumptions ya kura zile zilivyopigwa alikuwa anakosea sana! Yeye alivyoulizwa na Tindo angesema tu kuwa sio kweli waliopiga kura zile ni WaZanzibari 35 tu. Alitakiwa tu ajibu kuwa waliopiga kura walikuwa 64 na sio 35 kama watu tunavyotaka kuaminishwa!

Hussein Mwinyi we ni Raisi Mtarajiwa jitahidi sasa kuwa Mwanasiasa makini sio kila swali kulijibu kivileeeeeeeee! Ukiendelea kufanya hivyo hakika kuna mambo utaibua na utasababisha upinzani ukugalagaze huko Visiwani!
 
Yaani unataka ajibu maswali kama wewe unavyotaka.
Nyie ndio kama wale walimu mnaotaka mwanafunzi ajibu kama ulivyomkremisha
Ndiyo anafaulu mtihani! Sasa ajibuje nje ya marking scheme yangu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…