Uchaguzi 2020 Dkt. Mwinyi: Wajumbe wa Zanzibar waliotupigia kura ni 68 hata kama ni kweli wenzangu walipata 35 basi na mimi nilipata 33

Unaweza kuweka takwimu ni kwa vipi wa zanzibar hawamtaki Mwinyi?

Mlishazusha eti hajapigiwa kura na wajumbe wa zanzibar?

Kura 68, yeye kapata 33 wenzie wamegawana 35.
Ina maana hata wangepiga wanzanzibar pekee angeshinda tofauti na mnavyizusha!

Mwambieni Seif kipigo kipo pale pale na hivi ni mzee.
 
Kua mbunge miaka zaidi ya 10 , sijui waziri sijui nn.. hakumfanyi mtu awe na uwezo wa kupambanua mambo.

Kuna watu ukiwasikiliza tu unajua hamna kitu unazima na TV

Kuna mtu ukimsikikiza tu unajikuta umekesha kwa kumsikiliza.
Hapana ila tatizo linalo kusumbua ni hizo chuki binafsi zako.
 
Hujui madhara ya majibu yake! Kwani unafikiri waliozua kuwa wapiga kura wa Zanzibari walikuwa 35 unafikiri walikuwa hawajui?
Madhara yake ni yapi? Si kajibu kuondoa sintofahamu wanayozusha wazushi? Sasa shida iko wapi?

Yeye kasema wagimbea walikuwa 3, wapiga kura walikuwa 68 wenzie wamepata kura 35 yeye 33. Sasa hatari yake iko wapi hapo? Au mnajaribu kutengeneza picha kwamba kuna hatari?

Au ulitaka angepata kura zote wakati ule ulikuwa ni uchaguzi wenye washindani 3?
 
Kizazi hiki kinataka ushahidi!!!!!....Uchaguzi ukiwa huru na haki mwinyi hawezi kua rais wa zanzibar, hizo za mwinyi zimeibiwa tu ndio maana wazanzibari wote walitoka kwenye kikao wanalia.....
Zamani ccm ilikua na wenyewe lkn siku hizi ccm ina mwenyewe anayeamua kila kitu. Haya mambo ya ndani huwezi kuyajua ww endelea kulamba makalio tu utapata cheo
 
Nyie wengine labda wakati wa Mwinyi hamkuwepo au mlikuwa watoto, Mzee mwinyi pia alikuwa anaongea na kufanya matakataka mengi sana!

Misingi ya nchi hii alianza kuibomoa Mwinyi, ndio maana Mwl akawa anasimama mara kwa mara kumweka sawa.

Hivyo msitegemee akili za kurithi toka kwa mwanae!
 
Jamani mwachieni Rais kijana.
Wembe ameutaka mwenyewe, msichagulie namna ya kunyoa!
 
Wazanzibari wanasema haya, Zanzibar kwanza mengine yatafata baadae, hata utoe ahadi mia 100 kama hakuna Zanzibar kwanza wananchi watakwambia no.

Mifano ipo halisi bila ya kuwa na Zanzibar yenye mamlaka kamili.

Kwanza Zanzibar haiwezi kunufaika na rasilimali zake za ndani kama utalii, visa za wageni wote , fedha zinaenda Tanganyika

Pili mikopo, Zanzibar haiwezi kukopa nje wala haiwezi kupata misaada moja kwa moja ya kifedha bila ya kupitia serikali kuu Tanganyika kwa kupata kibali au kusainiwa na vile vile fedha za kigeni lazima zipite BOT

Tatu mapato ya muungano ikiwemo misaada, Zanzibar haifadiki hata kidogo kupitia hilo, ndio maana wazanzibari wanataka mamlaka kamili ya Zanzibar.

Michezo, michezo sio jambo la muungano Lkn time ijiitayo ya taifa imeundwa kinyume na katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, ikachukua mamlaka na kuingia katika socca la kimataifa FIFA , imeikosesha Zanzibar fursa nayo kimichezo, hili kero kubwa la muungano.


Kama huna strategy ya Zanzibar kwanza, kushinda uchaguzi labda kwa bunduki, kwa kura huwezi kushinda , wazanzibari wanajielewa sana na tunajua mahitaji yetu
 
Mpumbavu kweli wewe! Kila kitu kinaenda kwa takwimu siyo kwa hisia za kichadema,!

Kikao kilikuwa live kwa uwazi na kura zilipigwa live alafu unataka kuaminisha watu kwa mind set zako za kuibiwa kwamba hata zile kura za kumchagua mgombea wa zanzibar ziliibiwa?

Hao wazanzibar ndio katika ile kamati nusi yao walimpigia kura Mwinyi katika wagombea wote 3!

Narudia, mwambieni mzee Seif ajiandae kisaikolojia.
 
Patachimbika Zanzibari mwaka huu!
 
Mzee Mwinyi ni mtupu mpaka kesho.

Na alidhihirisha hilo alipoanza kusema Magufuli aongezewe miaka mitano baada ya 2025, katiba ibadilishwe mara moja kwa ajili ya Magufuli, halafu akipita urudishwe ukomo wa urais wa miaka 10.

Hiyu ndiye mtu aliyepigiwa kelele sana na Nyerere kuhusu umuhimu wa kuheshimu katiba.

Sasa sijui hakuelewa somo au amedharau tu.
 
Kamkoa cha Zenji kama mtosha, kataendeshwa kwa rimoti kutokea Chamwino
 
wengine sio lazima wajielezee ndio uelewe wana uelewa mkubwa.kujieleza ni karama kama ikrama nyingine huenda ukawa una utendaj kazi mkubwa na wa ajabu ila kujieleza kidogo inakua sio sana.nabii musa alikua na kigugumizi ila aliwakoa wana wa israel
 
Hakika inatia hamasa maelfu ya wananchi wajitokeza kumlaki Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dr Hussein Mwinyi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…