Dkt. Nchimbi apinga kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM Kagera aliyeahidi "kuwapoteza" wakosoaji wa serikali

Dkt. Nchimbi apinga kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM Kagera aliyeahidi "kuwapoteza" wakosoaji wa serikali

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Ndio hivyo, kiongozi anatakiwa kupinga mambo ya kijinga hadharani. Tunasubiri la kijana wa Arusha.

---
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amekemea kauli zinazoweza kutolewa na vijana wa chama hicho juu ya kuwapoteza watu wanaowapinga: “Huyu ni kijana wetu kasema jambo la kijinga na lazima tulipinge.”


SIASA: Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekemea kauli za vitisho zinazotolewa na baadhi ya Vijana wa chama hicho dhidi ya Wapinzani wao akieleza Chama kinapinga utaratibu huo

Akizungumza kutoka Jijini Mbeya katika Mkutano wa Hadhara, Dkt. Nchimbi amesema "Akiinuka Kijana wa CCM akasema Wapinzani wetu wakifanya hivi na hivi lazima tuwapoteze, huyu ni kijana wetu lakini kasema jambo la kijinga tutalipinga kwasababu nchi hii ni yetu sote."

Kauli ya Balozi Nchimbi inakuja muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera, Faris Buruhan, kusema Wakiwapoteza wanaowatusi Viongozi Mitandaoni, Jeshi la Polisi lisiwatafute.

===================
The Secretary-General of CCM, Ambassador Dr. Emmanuel Nchimbi, has condemned threatening statements made by some youth within the party against their opponents, emphasizing that the party opposes such behavior.

Speaking from Mbeya City at a public meeting, Dr. Nchimbi stated, "If a CCM youth rises and says we must eliminate our opponents for doing this or that, while he is our youth, if he says something foolish, we will oppose it because this country belongs to us all."

Ambassador Nchimbi's remarks come shortly after the UVCCM Chairman for Kagera Region, Faris Buruhan, stated that if they lose those who insult leaders online, the police should not search for them.

PIA SOMA:
- Mwenyekiti UVCCM Kagera, Faris Buruhan: Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia mitandaoni, Polisi msiwatafute

- CCM ya sasa ingekuwa smart ingemkana Mwenyekiti UVCCM Kagera. Kwa kunyamaza ni kama wanathbitisha ni wauwaji
 
Ndio hivyo, kiongozi anatakiwa kupinga mambo ya kijinga hadharani.
View attachment 2966677
Nilitarajia majibu mazuri ya namna hii.

Kama itafaa CCM iwaondoe wale wote wenye mambo ya kijinga ili kuondoa sintofahamu nyingi zinazokihusisha Chama na mambo ya kijinga.

Hoja ya wakubwa kutukanwa isiwe ya Kisiasa bali iwe ni hoja hasa kwa vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama kudeal na hao watu kimya kimya na ikiwezekana wafikishwe kwenye vyombo vya Dola.

Mh.Rais sio wa CCM pekee bali ni wa kila mtanzania,hivyo si jukumu la CCM pekee kumsemea bali la wote.

Kuendelea kutumia siasa katika masuala nyeti yanayogusa mhimili wa Urais kunaweza kuingilia mihimili mingine na vyombo vya Dola kushindwa kufanya maamuzi.
 
SAfi kabisa,isiishie kumpinga tu bali huyo kijana anapaswa kuwajibishwa kabisa,hafai kuwa kiongozi,maana haheshimu utawala wa sheria,anampango wa kuchafua taswira ya chama chetu.

Ccm iwe makini isijekuwa huyo jamaa ni pandikizi toka chadema,maana nijuavyo chama cha ccm hakina hulka ya kupingana na mawazo ya mtu kwa kumuua
 
Nilitarajia majibu mazuri ya namna hii.
Kama itafaa CCM iwaondoe wale wote wenye mambo ya kijinga ili kuondoa sintofahamu nyingi zinazokihusisha Chama na mambo ya kijinga...
CCM haiwezi kujitenga Kwa mambo kama haya maana wanafundushwa
 
Back
Top Bottom