Dkt. Nchimbi apinga kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM Kagera aliyeahidi "kuwapoteza" wakosoaji wa serikali

Dkt. Nchimbi apinga kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM Kagera aliyeahidi "kuwapoteza" wakosoaji wa serikali

wahaya Kwa sifa 😂😂, uyo kijana ukute hajui chochote kuhusu wanaopotea lakini tayari kaisha ingia kwenye kikaangio
Kwa asilimia kubwa hajui chchote. Ni ile ''ntoke vipi mama anione''. Huu ujinga umekuwa kama ndiyo utamaduni wa vijana wa CCM sasa hivi.
 
Nadhani Nchimbi amekomaa na kuiva kisiasa.
Ni mara ya kwanza kwa Kiongozi wa ngazi ya juu ya Chama kutoa kauli sahihi ya kukemea maovu yanayofanywa na vijana wao kutishia Amani ya nchi.

Tunampongeza mno Dkt Nchimbi. Inaonekana yeye kuishi nje ya nchi kama Balozi amepata exposure ya kutosha Na ameona nchin za wenzetu siasa enadeshwaji bila uadui.
 
Ndio hivyo, kiongozi anatakiwa kupinga mambo ya kijinga hadharani. Tunasubiri la kijana wa Arusha.
---

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amekemea kauli zinazoweza kutolewa na vijana wa chama hicho juu ya kuwapoteza watu wanaowapinga: “Huyu ni kijana wetu kasema jambo la kijinga na lazima tulipinge.”

PIA SOMA:
- Mwenyekiti UVCCM Kagera, Faris Buruhan: Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia mitandaoni, Polisi msiwatafute

- CCM ya sasa ingekuwa smart ingemkana Mwenyekiti UVCCM Kagera. Kwa kunyamaza ni kama wanathbitisha ni wauwaji
Respect kwa Dr. Nchimbi.
 
Siasa za kishamba za kuteka watu na kutishia kuwaua ziliasisiwa na yule mwendawazimu kutoka Chato.

Mpwa wake ambaye sasa ni DC alisema wapinzani atawapoteza kwa kuwachoma sindano za sumu.

Rekodi zipo zimehifadhiwa.
 
Dr. Nchimbi ni CCM asilia, kalelewa na kukulia humo. Ana siasa za kistaarabu kwa misingi asili ya CCM na kamwe si mropokaji. Naamini atakirejesha chama katika maadili asilia.
 
Inategemea na nchi, Brazil kuna demokrasia Imara sana. Nchi kama Cuba Polepole anaendelea kuiva kwenye siasa za mfumo wa chama kimoja.
Polepole hata angepelekwa US bado angerudi mtupu. Ni kati ya watu ambao wapo addicted na zile siasa chafu ya awamu ya 5.
 
Ndio hivyo, kiongozi anatakiwa kupinga mambo ya kijinga hadharani. Tunasubiri la kijana wa Arusha.
---

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amekemea kauli zinazoweza kutolewa na vijana wa chama hicho juu ya kuwapoteza watu wanaowapinga: “Huyu ni kijana wetu kasema jambo la kijinga na lazima tulipinge.”

PIA SOMA:
- Mwenyekiti UVCCM Kagera, Faris Buruhan: Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia mitandaoni, Polisi msiwatafute

- CCM ya sasa ingekuwa smart ingemkana Mwenyekiti UVCCM Kagera. Kwa kunyamaza ni kama wanathbitisha ni wauwaji
Kauli hiyo itawafanya vijana waanze kuusoma upepo. Majigambo yatapungua sasa kwa hao vijana maana walishaigeuza hii nchi kuwa mali yao.
 
Back
Top Bottom