Dkt. Nchimbi apinga kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM Kagera aliyeahidi "kuwapoteza" wakosoaji wa serikali

wahaya Kwa sifa 😂😂, uyo kijana ukute hajui chochote kuhusu wanaopotea lakini tayari kaisha ingia kwenye kikaangio
Kwa asilimia kubwa hajui chchote. Ni ile ''ntoke vipi mama anione''. Huu ujinga umekuwa kama ndiyo utamaduni wa vijana wa CCM sasa hivi.
 
Nadhani Nchimbi amekomaa na kuiva kisiasa.
Ni mara ya kwanza kwa Kiongozi wa ngazi ya juu ya Chama kutoa kauli sahihi ya kukemea maovu yanayofanywa na vijana wao kutishia Amani ya nchi.

Tunampongeza mno Dkt Nchimbi. Inaonekana yeye kuishi nje ya nchi kama Balozi amepata exposure ya kutosha Na ameona nchin za wenzetu siasa enadeshwaji bila uadui.
 
Respect kwa Dr. Nchimbi.
 
Siasa za kishamba za kuteka watu na kutishia kuwaua ziliasisiwa na yule mwendawazimu kutoka Chato.

Mpwa wake ambaye sasa ni DC alisema wapinzani atawapoteza kwa kuwachoma sindano za sumu.

Rekodi zipo zimehifadhiwa.
 
Dr. Nchimbi ni CCM asilia, kalelewa na kukulia humo. Ana siasa za kistaarabu kwa misingi asili ya CCM na kamwe si mropokaji. Naamini atakirejesha chama katika maadili asilia.
 
Inategemea na nchi, Brazil kuna demokrasia Imara sana. Nchi kama Cuba Polepole anaendelea kuiva kwenye siasa za mfumo wa chama kimoja.
Polepole hata angepelekwa US bado angerudi mtupu. Ni kati ya watu ambao wapo addicted na zile siasa chafu ya awamu ya 5.
 
Kauli hiyo itawafanya vijana waanze kuusoma upepo. Majigambo yatapungua sasa kwa hao vijana maana walishaigeuza hii nchi kuwa mali yao.
 
A
Kupinga haitoshi,

Anatakiwa afukuzwe CCM
Aende jela na tushuhudie akienda jela na kuadhibiwa vilivyo pia yafukuliwe makaburi atuambie uhusika na waliotoweka kusikojulikana🤪
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…