Dkt. Nchimbi apinga kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM Kagera aliyeahidi "kuwapoteza" wakosoaji wa serikali

Tatizo ni kuwa ccm wamezoea kufuga wahalifu. Yule mwenyekiti wa uvccm aliyetamka hadharani hiyo mipango ya mauaji a.k.a "kupoteza" watu ilifaa awe yupo jela by now.

Kuna uwezekano huyo mtu alihusika kupoteza wale waliotoweka awamu ile
 
Yeye kama mtendaji mkuu wa Chama kwanini asimchukulie hatua kuonesha yuko serious kimatendo na alichokisema? Asipochukuliwa hatua meaning hii kauli ya Karibu mkuu tutaichukulia kama porojo tu mbele ya halaiki
 
Hawa vijana wenye siasa za kishamba hawasomi majira na nyakati. Bado wanadhani nafasi za uteuzi bado zinatokana na kauli zao za Kipumbavu kwa wapinzani. Wanashidwa kujenga hoja na kuongea mipango ya maendeleo kwa chama chao kete yao ni kutisha watu. Hii statement aliyowambia polisi kutowatafuta waliopotezwa kweli inaweza kutoka kwa mtu mwenye akili? Nchimbi kaongea vizuri kuwa huo ni ujinga.
 
Yeye kama mtendaji mkuu wa Chama kwanini asimchukulie hatua kuonesha yuko serious kimatendo na alichokisema? Asipochukuliwa hatua meaning hii kauli ya Karibu mkuu tutaichukulia kama porojo tu mbele ya halaiki
Kwa mwenye akili, kitendo cha kukemewa hadharani kitamfanya ajitafakari kama nafasi aliyonayo inamtosha. Hiyo ni adhabu kali zaidi ya unavyofikiria.
 
Ccm iwe makini isijekuwa huyo jamaa ni pandikizi toka chadema,maana nijuavyo chama cha ccm hakina hulka ya kupingana na mawazo ya mtu kwa kumuua
Duuh
Ccm na uongo ni kama mwanamke na pesa..

Kwani ni chama gani huwekea sumu, pamoja na kuteka na kuua wakosoaji?

Tofauti ya huyu mhalifu na wanaccm wengine ni kwamba wenzie hufanya siri
 
Kwa mwenye akili, kitendo cha kukemewa hadharani kitamfanya ajitafakari kama nafasi aliyonayo inamtosha. Hiyo ni adhabu kali zaidi ya unavyofikiria.
Kwa hawa viongozi wa CCM sijui, nimekaa pale nasubiria mkuu
 
Nchimbi kaja vizuri. Huyu ndiye kiongozi sasa. Siyo kama yule chizi wa Arusha
Kama hatachukua hatua kwa huyu mjinga na ikawa wazi basi na yeye atakuwa kama wa huyo wa Arusha.
 
Vijana wa ccm wengi wao ni wapuuzi, anaekupinga sio adui mnatofautiana tu mitazamo
 
Ni muhimu chama kurudi kwenye mstari na utaratibu wa asili wa maadili, uungwana utu na heshima kwa wote. Tabia za unyama na kujitoa ufahamu ili kupata teuzi ni upumbavu usiokubalika na sio sawa kwa mustakabali mwema wa jamii, chamachama, serikali na taifa.
CCM lazima iwe mfano wa kuigwa kwa vyama vingine ndani na nje ya nchi.
Itachukua muda kurekebisha utamaduni wa kujitoa ufahamu na unyama kwenye siasa kwa sababu umejengeka kwa muda na wanufaika wamekuwa mfano kwa wanaotafuta.
Hata hivyo, kufanya kosa kuna athari ndogo kuliko kurudia kosa.
 
Kila sehemu ina vichaa, kama tunavyowasihi wale wa vidole juu wamkemee Mdude Nyagali na genge lake
Vichaa hawapewi nafasi kwenye jamii ya watu wenye akili, hudhibitiwa.
Wakipewa rungu inakuwaje?
Wazee wa zamani walituasa.
 
Khe eti leo ninyi digba na mwashamba mnasupport wapinzani wasishughulikiwe! Kweli! Mwashamba huyuhuyu! Halafu awaita watu nyumbu leo.

Leo vijana wa vyama wajifunze maana ya utaifa na siyo uchama.
 
Alichokicanya huyo kijana wa UVCCM ni kuropoka,,
Lakini hayo aliyoropoka ndy hali halisi ilivyo kwa sasa.

Ni sawa na kumlaumu mtoto mdogo anayelalq chumba kimoja na wazazi wake,,.
kuropoka matendo wafanyayo wazazi wake usiku wa manane..

Katibu wa chama ni kama mzazi lazima akemee yale mtoto aliyoropoka..hata kama ni kwl.
 


Wangemtoa katika nafasi yake, kumkemea tu haitoshi, maana katoa kauli mbaya sana, maana ya kumpoteza mtu ni kumuua, hivyo huyo kijana wa Kagera angefaa atolewe katika uongozi wa CCM haraka sana sbb anaichafua CCM yetu, Mh. Katibu Mkuu najua atampa adhabu ya kumtoa katika uongozi..

Huyo kijana wana CCM kumpinga naomba iwe pamoja na kumtoa katika uongozi haraka kabisa, asante sana Mh. Katibu Mkuu Dr. Nchimbi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…