Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Katibu Mkuu wa Chama cha mapinduzi Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi akizungumza na Wananchi wa Tinde Shinyanga amemuagiza Waziri wa Tamisemi kuhakikisha kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025 ahakikishe Moja ya maeneo yenye uhitaji wa Kituo cha Afya kiwe kimejengwa ili kurahisisha huduma kwa jamii.
"Kuna maeneo matatu yanatajwa hayana vituo vya Afya ila eneo moja tayari limepata fedha Milioni Mia sita na Sitini na Sita (666) bado maeneo mawili, nataka nitumie nafasi hii unajua vitu hivi vinaenda kidogo kidogo, Mimi nimuambie Waziri Tamisemi ambae ndio anahusika na kutoa Vituo vya Afya kwamba kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao wa 2025 Kituo cha Pili kiwe pia kimepatikana".