Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: Maendeleo aliyoleta Rais Samia kwa miaka 3 Madarakani ni kama miujiza

Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: Maendeleo aliyoleta Rais Samia kwa miaka 3 Madarakani ni kama miujiza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hiyo growth rate imeonyesha Tz ndio pekee inayokuwa au the whole of EA inakuwa kiuchumi?
Nchi zote zinakua ila Tanzania ndio tumekuwa na consistency nzuri miaka yote tofauti na hao wengine ambao economic shocks zikitokea Huwa wanayumba sana then wanaanza recovery
 
Mjomba wangu ni meneja pale TRA. Uwepo wake pale unaninufaisha mimi na familia yetu kwa kiasi kikubwa. Tutafanya kila tuwezalo aendelee kubaki pale. Uwepo wake pale ni assurance kwangu na familia yetu kwamba tutaendelea kuneemeka. Ahsante sana mjomba.​
 
Pita mitaa ya masaki, mikocheni, mbezi beach uone namna biashara mpya zinavyozidi kuanzishwa. Huhitaji takwimu tumia macho yako utaona kitu fulani kinaendelea katika suala zima la biashara binafsi za watu.

Pale TPA kutakuwa na waendeshaji wengine wawili mpaka itakapofika mwezi wa nane mwaka huu.
Sio huko tuu ni Tanzania nzima

View: https://twitter.com/InvestTanzania/status/1777797813037895986?t=DtjuBrz1UNXVZRBeoP-2TA&s=19

View: https://twitter.com/InvestTanzania/status/1774033331211948075?t=zvDPjZAs-vqzj2PKcNMBOQ&s=19
 
Then how comes wana growth rate kubwa kuliko tz?
Unaelewa maana ya consistency? Pili hiyo ni projections lakini mwaka 1 na mingine nyuma hakuna Nchi hata Moja kwenye hiyo list ukitoa Rwanda imewahi izidi Tanzania.

Mara wawe -ve ,mara 3,mara 4 ila ni mwaka wa uviko tuu ndio Tanzania tulishuka chini ya 5 tukawa 4 wakati hao wengine walikuwa kwenye -ve huko.
 
Unaelewa maana ya consistency? Pili hiyo ni projections lakini mwaka 1 na mingine nyuma hakuna Nchi hata Moja kwenye hiyo list ukitoa Rwanda imewahi izidi Tanzania.

Mara wawe -ve ,mara 3,mara 4 ila ni mwaka wa uviko tuu ndio Tanzania tulishuka chini ya 5 tukawa 4 wakati hao wengine walikuwa kwenye -ve huko.
Naelewa consistency but future haiko guaranteed tuki judge from past records. Kila nchi ina pambana. And how come nchi kama rwanda inatuzidi? Those guys hawana resources tulizonazo yet wako juu? Why?
 
Hayo yameelezwa na KM wa CCM Dkt.John Nchimbi wakati wa ziara yake ya Mikoa 6 akiwa Njombe.

DK Nchimbi ameonekana kushangazwa na kufurahishwa na Wingi wa miradi na maendeleo yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika akisema ni kama miujiza maana kilichotakiwa kufanyika Kwa muda mrefu kimewezekana ndani ya mda mchache kabisa.

Kwa wasio fahamu,haters na wabishi hii hapa ni summary tuu ya kilichofanywa na Samia.
-Mapato ya TRA kuongezeka kutoka wastani wa 1.5T Hadi 2.2T(ongezeko bil.700 )
-Makusanyo ya Halmashauri kuongeza kutoka Bil.800 Hadi Trilioni 1.2(Ongezeko Bil.400)
-Ongezeko la Mapato ya Utalii Hadi 3.5T(Watalii 1.9m) kutoka 3T(Watalii 1.5mln).
-Ujenzi wa Bandari Ziwa Nyasa(MbambaBay),Ziwa Tanganyika(Kigoma),Ziwa Victoria (Mwanza,Bukoba,Chato) na Bhari ya Hindi(Dar,Tanga,Kilwa na Mtwara).
-Ujenzi wa viwanja wa ndege 15 Unaendelea Tanzania nzima
-Ujenzi wa Hospital za Wilaya mpya 129 ,Mikoa 7 na Rufaa za Kanda 3(Mtwara,Kigoma na Ukerewe).
-Ujenzi wa Vituo vya Afya vipya 402 kwenye kata za kimkakati hapo tozo za miamala (234).
-Ununuzi wa vifaa tiba ambavyo havikuwahi kuwepo Kwenye hospital za Tanzania mfano Ultra Sound 192 ,Digital X-rays 147,CT Scan 32,MRI machines 7.
-Ujenzi wa majengo ya Wagonjwa Mahututi(ICU) 28 na Dharula 127,
-Upanuzi na Ujenzi wa Vyuo Vikuu vipya na kampasi za Vyuo kwenye Mikoa 14 ambayo swali haikuwa na Vyuo Vikuu au kampasi eg Kigoma,Simiyu,Njombe,Ruvuma, Rukwa,Katavi,Shinyanga,Lindi,Mtwara nk.
-Kaongeza Bajeti Kila Wizara ila Kwa upekee ni Wizara ya Kilimo(Umwagiliaji )kutoka Bil.270 Hadi Bilioni 950.Skimu Mpya za uwamwagiliaji hectare 95,000 zimejengwa na kufufuliwa,kafungua ofisi za Kilimo Kila Wilaya na kaajiri Wataalamu na kawapa vitendea kazi.
-Kaondoa shida ya vitambulisho NIDA,zaidi ya vitambulisho 12,000,000 vimegawiwa.
-Ujenzi wa minara mipya 1,200 ambapo Kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali minara 728 inaendelea na Ujenzi Kwa Bilioni 126.(Kijijini kama mjini)
-Amefikisha maji ya Bomba Kwa zaidi ya Vijiji 11,000
-Amefikisha umeme Kila Kijiji
-Amewasha Umeme gridi ya Taifa Mikoa Kigoma,Katavi
-Amejenga zaidi ya Shule Mpya za Sekondari 3,200 ,shule za msingi zaidi ya 300 na madarasa 24,000 ,mabweni 137 nk
-Kupitia TanRoads amekamilisha zaidi ya km 1,000 za lami na zingine zaidi ya 3,700 zinaendelea na Ujenzi.
-Kupitia Tarura amejenga zaidi ya km 800 za lami na zingine zaidi ya 500 zinaendelea na Ujenzi (Hapa amefungua maelfu ya Vijijini Kwa Barabara Mpya za changarawe na madaraja). Bajeti ya Tarura aliongeza kutoka bil.270 Hadi Bil.800.
-Sekta ya mifugo amegawa Boti za Kisiasa zaidi ya 200 na viximba zaidi ya 1300 Kwa Vijana.
-Sekta ya Elimu kaongeza mikopo Kwa wanafunzi ambapo Sasa Diploma Hadi Chuo Kikuu wanapata,chekechea Hadi form six Elimu Bure(kafuta ada ya form Six),Kafuta Mapenato na mambo ya hivyo ya Bodi ya Mikopo.
-Katoa Ajira zaidi ya 55,000 kada zote huku Elimu na Afya wakipewa kipaombele.
-Anajenga na kukamilisha zaidi ya miradi ya maji 3,700 mikubwa Kwa midogo mfano mradi wa Miji 28,bwawa la kidunda na kukwamua miradi iliyokwamba kama same-mwanga,Tarime-Kiabakari nk.
-Kwenge sekta ya biashara baada ya maboresho maelfu ya miradi imemenika Kila sekta baada ya Wafanyabiashara kurejesha Imani Kwa Serikali Kupitia sera ya Diplomasia ya Uchumi na kuifungua Nchi.Hakuna ziara ambayo mama alifanya Nje ya Nchi hajakutana na Wafanyabiashara wa Kimataifa.
-Sekta ya michezo na Burudani.Huko Kila mtu anajua kwamba Mama alikatabati viwanja,akaleta ufunguzi wa AFL na sasa ameileta Afcon 27 na uwanja Mpya inajengwa Arusha.Likewise kuwapa mikopo Wasanii.
Kiufupi ni vigumu kuelezea vyote,pamoja na Changamoto ila Mama kaupiga mwingi ,Anatosha na Chenji inabakia.

View: https://www.instagram.com/p/C59CY7uMJC5/?igsh=MTNiYnozM2hubjMwZQ==
My Take
Yote hayo kafanya na anaendelea kufanya lakini hajawahi acha mradi hata 1 aliourithi kutoka Kwa Mwendazake kama Bwawa la JNHPP,Daraja la JPM,EACOP,SGR,Ndege Mpya,Ujenzi wa Mji wa Serikali na hajatoa visingizio.

View: https://twitter.com/MfanyakaziNews/status/1781317600514809949?t=yhy9JBufLMEhmo34FTghDg&s=19

Ndio vizuri!
 
Kwahio kwa mujibu wa CCM hiki kilichofanyika ni over-performance ? Kwamba walichopanga kifanyike kilikuwa ni kidogo kuliko kilichofanyika ?

Either CCM ni mediocre au ni mwendo wa kuendeleza Propaganda...

 
Naelewa consistency but future haiko guaranteed tuki judge from past records. Kila nchi ina pambana. And how come nchi kama rwanda inatuzidi? Those guys hawana resources tulizonazo yet wako juu? Why?
Rwanda ni Moja ya Nchi open zaidi kwenye biashara,Tzn hapa mentality za ujama zinasumbua vitu vingi vinahitaji reforms ila Kuna kusita sita na kujikongoja eg sakata la DP World, Ngorongo,DART nk.

Hat hivyo Rwanda ni LDC,Tanzania ni Middle Income Country
 
Kwahio kwa mujibu wa CCM hiki kilichofanyika ni over-performance ? Kwamba walichopanga kifanyike kilikuwa ni kidogo kuliko kilichofanyika ?

Either CCM ni mediocre au ni mwendo wa kuendeleza Propaganda...

Huwezi kusema kilichopangwa kilikuwa kidogo bali hata wao wanaona Kwa kulinganisha huko nyuma hakuna Rais ametekeleza Ilani Yao Kwa Ukubwa kumzidi Samia na sio sifa ila ndio uhalisia wenyewe.
 
Hizo pesa zote za kufanya hayo katoa wapi?.
 
Rwanda ni Moja ya Nchi open zaidi kwenye biashara,Tzn hapa mentality za ujama zinasumbua vitu vingi vinahitaji reforms ila Kuna kusita sita na kujikongoja eg sakata la DP World, Ngorongo,DART nk.

Hat hivyo Rwanda ni LDC,Tanzania ni Middle Income Country
Rwanda imebarikiwa 🐼
 
Back
Top Bottom