Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: Maendeleo aliyoleta Rais Samia kwa miaka 3 Madarakani ni kama miujiza

Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: Maendeleo aliyoleta Rais Samia kwa miaka 3 Madarakani ni kama miujiza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

INAPENDEZA KUONA NISHATI INASOGEZWA KWA WENGI AWAMU HII YA SITA

Tushukuru,

Kaka Biteko,

Kaka Mramba,

Pandeni basi mbegu ya shauri ili matumizi ya Umeme yajekuwa kama nishati ya msingi ya kupikia kwa utaratibu maalum...

Kaka Mramba, Katibu-Nishati, unaweza kutengeneza mazingira ya kuitafuta suluhu ya wabunifu wa ndani ama nje ambao wanaweza kubuni mifumo inayoweza kujumuishwa na uundwaji wa majiko ya Umeme ambavyo Umeme unaotumika kwenye jiko unatengeneza/kujinereti 'kode' maalum inayorudishia 'Units' za credits za LUKU.

Majiko mengi ya kawaida ni vifaa vinavyotumia umeme mwingi na hivyo kula 'units' nyingi; japo matumizi yake ni afueni kubwa kimazingira, jamii na uchumi.

Japo kiuchumi na taratibu za kiutendaji Serikalini, mambo ya ruzuku kwa ajili ya 'matumizi maalum kama kupikia majumbani' ama pia 'kushusha bei ya umeme' kwa ujumla 'yana figusi' za maslahi ya 'Wadau wa Huduma/Biashara ya NIshati'; khasa inapokuja kwenye uandaaji wa sera na sheria za kusimamia 'Utoaji Huduma' wa Serikali/Sekta binafsi; basi hebu tutumie suluhu za tekinolojia kuruka vihunzi, kupunguza mikingamo, ya wadau wenye maslahi na 'biashara za nishati'; kwa maslahi mapana ya taifa.

Mambo ya kutengeneza/jinereti 'kode' na ujumuishaji wake wa mifumo ya kitekinolojia ni masuala ya kiufundi tu; ikiwa LUKU inaweza 'kuusoma' umeme unatumika nyumba nzima kama klaenti mmoja; jambo hili hili linawezekana kwa kufunga kifaa kama hicho kuusoma umeme unaingia moja kwa moja, ili kutumika, kwenye kifaa chochote cha kiumeme--hapa lakini tukazie suluhu za kupikia majumbani: JIKO...

Ikiwa kila nyumba inakuwa na mita moja ya LUKU; pia inakuwa na kifaa pacha, kinachokaa 'mahala muafaka katika mfumo wa Jiko la umeme', basi uwezekano upo wa kubuni mfumo wa mawasiliano wa kidigitali ambavyo kiasi cha umeme unatumika unasomwa na unageuzwa kuwa data ya 'kusawazishia' reti ya matumizi ya umeme kwa kaya...

Kiufundi, Data hiyo inaweza kujineretiwa na kurajisiwa kwenye 'LUKU ndogo ya Kujitegemea ya Jiko' ambavyo:-

(1) Kama inatengeneza/jinereti 'Kode' basi mtu anaweza kutumia hiyo kode kurudishia 'Units' za umeme kwenye LUKU kuu
(2) Kama ina mawasiliano ya kujitegemea na LUKU kuu basi iwe inapeleka 'signali' -- mrejesho wa kusawazisha 'reti' za matumizi ya umeme katika Klaenti huyo huyo mmoja wa Tanesco
(3) Kama mfumo mzima wa taarifa za usomaji na uthibiti wa matumizi ya umeme unajumuishwa kwenye 'LUKU ZA KISASA/ZILIZOBORESHWA/SASISHWA' basi taarifa zote za matumizi ya kawaida ya nyumbani na ya 'umeme wa kupikia' yanakuwa ni sehemu 'hesabu na ankara' ya rajisi ya 'nishati na gharama zake' kwa klaenti -- mteja wa TANESCO.

HILI LINAWEZEKANA...

Asitokee 'mhuni' yeyote akaleta biashara za 'kufunika funika' ukweli wa mawezekano haya; Kama anataka 'Biashara' basi aharakishe 'Ubunifu wa Kitekinolojia' na aweke 'dau nafuu' la kuipatia huduma bora TANESCO kibiashara; ili shirikia hili nalo litimize matakwa na matarajio yake kwa umma; na kama umma wenyewe unavyohitaji...
cc: Logikos
 
Back
Top Bottom