Pre GE2025 Dkt. Ndugulile: Uchaguzi wa 2020 ulikuwa na dosari ambayo hatuwezi kuificha, siungi Mkono kupita bila kupingwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mtu yule ameacha Machukizo ndani na nje ya ccm
 
Kuongea ukweli pia ni jambo jema.

Ukweli ni ukweli tu na utabaki kuwa Ukweli.

Haiwezekani Wapinzani peke yao tu ndiyo hawawezi kujaza form wakati wote wamesoma shule hizo hizo za kata kama maCCM.
 
Katiba yetu ina mapungufu na watu wa CCM wamekaza shingo, yaani kumkosoa mwenyekiti wa chama, amiri jeshi mkuu, mkuu wa serikali na mihimili mingine ambayo inasubiri maelekezo yake ni mpaka afe.

Yaani hata Kikwete hawana uwezo wa kumkosoa waziwazi mpaka wamzike ndio waanze unafiki wa kumsema maana katiba imempa raia namba moja kinga na jeuri ya kufanya chochote bila kuwajibishwa.
 
Inaelekea Dr. Ndugulile ni msomi aliyesoma akaelimika!
 
Kupita bila kupingwa kwa wakati ule na sasa ni vitu viwili tofauti! Amir Jamal wa a well read person na alii-manage vizuri sana Wizara ya Fedha, tofauti sana na hawa akina chemba wadesaji!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…