Pre GE2025 Dkt. Ndugulile: Uchaguzi wa 2020 ulikuwa na dosari ambayo hatuwezi kuificha, siungi Mkono kupita bila kupingwa

Pre GE2025 Dkt. Ndugulile: Uchaguzi wa 2020 ulikuwa na dosari ambayo hatuwezi kuificha, siungi Mkono kupita bila kupingwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
"Uchaguzi wa 2020 ulikuwa na dosari ambayo hatuwezi kuificha, haiwezekani wagombea wa upinzani tu ndio hawakujua kujaza fomu ipasavyo halafu wagombea wa CCM wakaweza kujaza fomu ipasavyo kila mahali” Dkt. Faustine Ndugulile.

Ndugulile amesema haungi mkono suala la wagombea kupita bila kupingwa “Mtu kama unajiamini kwa nini upite pasipo ushindani..?”

Hata hivyo Ndugulile amesema alikuwa na uhakika wa kuwashinda wapinzani wake kwenye uchaguzi wa ndani ya CCM akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Paul Makonda, ambaye kwa sasa ni katibu muenezi wa CCM Taifa.

“Mimi sijawai kuwa na uchaguzi rahisi kigamboni na uwa sipendi uchaguzi mwepesi, hata 2015 niligombea na vigogo wengi akiwemo mtoto wa Rais Mkapa lakini nilishinda” Ndugulile.

Mtu yule ameacha Machukizo ndani na nje ya ccm
 
Katiba yetu ina mapungufu na watu wa CCM wamekaza shingo, yaani kumkosoa mwenyekiti wa chama, amiri jeshi mkuu, mkuu wa serikali na mihimili mingine ambayo inasubiri maelekezo yake ni mpaka afe.

Yaani hata Kikwete hawana uwezo wa kumkosoa waziwazi mpaka wamzike ndio waanze unafiki wa kumsema maana katiba imempa raia namba moja kinga na jeuri ya kufanya chochote bila kuwajibishwa.
 
"Uchaguzi wa 2020 ulikuwa na dosari ambayo hatuwezi kuificha, haiwezekani wagombea wa upinzani tu ndio hawakujua kujaza fomu ipasavyo halafu wagombea wa CCM wakaweza kujaza fomu ipasavyo kila mahali” Dkt. Faustine Ndugulile.

Ndugulile amesema haungi mkono suala la wagombea kupita bila kupingwa “Mtu kama unajiamini kwa nini upite pasipo ushindani..?”

Hata hivyo Ndugulile amesema alikuwa na uhakika wa kuwashinda wapinzani wake kwenye uchaguzi wa ndani ya CCM akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Paul Makonda, ambaye kwa sasa ni katibu muenezi wa CCM Taifa.

“Mimi sijawai kuwa na uchaguzi rahisi kigamboni na uwa sipendi uchaguzi mwepesi, hata 2015 niligombea na vigogo wengi akiwemo mtoto wa Rais Mkapa lakini nilishinda” Ndugulile.

Inaelekea Dr. Ndugulile ni msomi aliyesoma akaelimika!
 
Huyu naye ni mtafuta kick tu ya kukubaliwa na waliochukua CCM sasa. Mbona hakupinga wakati huo.

Swala la wagombea kupita bila kupingwa limekuwapo tangu tupate uhuru, halikuanza majuzi tu. Amil Jamal alikuwa Mbunge wa Morogoro kwa muda mrefu sana akiwa anapita bila kupingwa. Baada ya vyama vingi na kuhitaji kila mgombea awe amesimamishwa na chama cya siasa, kuna majimbo mengi sana mwaka 1995 yalichukuliwa na CCM bila kupingwa kwa sababu vyama vya upinzani havikusimamisha wagombea.

Kilichotokea mwaka 2020 ni kwamba kuna majimbo ambayo ama vyama vya upinzani vilikuwa na wagombea walioenguliwa kwa sababu yeyote ile au havikutoa mgombea kabisa. Nape na Majaliwa ni kai ya waCCM waliopita bila kupingwa kwa sabababu majimbo yao hayakuwa na wagombea wa vyama vya upinzani. Angepinga jinsi wagombea wa upinzani walivyoenguliwa siyo kupinga kitendo cha mgombea wa CCM kupita bila kupingwa wakati ndio utaratibu uliokuwapo miaka yote hiyo.

Sheria ya Uchaguzi inatakiwa marekebisho sana lakini huyu naye asitake kutafuta kukubaliwa na kundi lilipo sasa hivi kwa kukandia uchaguzi ambao yeye mwenye alishiriki na kukubali matokeo yake.
Kupita bila kupingwa kwa wakati ule na sasa ni vitu viwili tofauti! Amir Jamal wa a well read person na alii-manage vizuri sana Wizara ya Fedha, tofauti sana na hawa akina chemba wadesaji!
 
Back
Top Bottom