Dkt. Ndungulile, hutaki kujiuzulu au unasubiri usaidiwe kazi?

Inabidi vifurushi vitozwe kodi ya kawaida na sio kukomoana ili watu washindwe kufanya mawasiliano kimtandao!! Najua ulikuwa mpango mkakati ila sasa Mama aseme hapana!
 
Jimbo lake watu wake maskini kama nini, nahisi aliongeza cha juu kwa kila bando.
 
Hali bado ni maumivu,menu zinasoma vifurushi vipya vya Ndungulile ndivyo vilivyopo. Huyu huyu Waziri alisisitiza kuwa wamiliki wa mitandao hawawezi kubadilisha vifurushi hadi baada ya miezi mitatu, ndicho kinachoendelea?Hili tangazo la kurejesha vifurushi vya zamani lilitolewa lini na kuanza lini?

Hii siyo ile style ya kuanzisha tatizo ili upate umaarufu kwa kuleta utatuzi/suluhisho?
 
Hiyo afya yenyewe sijui Kama ipo tena kichwani maana hata akiulizwa panadol ina mg ngapi huenda asiweze kujibu.
 
huyu alikuwa anafanyia kazi maelekezo ya JPM.
kama unakumbuka vizur huu mchakato ulianza chini yake.
na hayati angekuwepo lingeshapita.

huyu waziri anatakiwa aamke . ajue yuko zama zipi.
 
Katika mawaziri ambaye angetolewa mara moja ni huyo Ndungulile, waziri muongo kuliko shetani, hafai kabisa huyo. Mimi naamini mama Samia atamtimua kazi haraka huyo kipara kama layoni wa kimasai
 
Wadau mwenye ile clip ya Ndungulile akielezea namna bei ya mawasiliano itakavyokuwa bei nafuu kuanzia tarehe 2/4/2021 naomba atupie.... humu. Tujikumbushe😀😀
 
Eti huo mpango wake mpya ni kuruhusi kushare bundle kupitia mitandao yote. Hivi hapo unategemea nini. Hata boya kama mimi naona ni matope matupu.

Kwa mfano halotel 1 GB ni 1000 halafu voda 1 GB ni 2000 Eti unaweza kununua bundle halotel halafu unashare na vodacome. Hivi hapo unategemea nini.

Serikali saa nyingine iwe inatumia akili!!
 
Itakuwa anasubiri Kwanza Kampuni zote za Simu zimalize Kurejesha Vifurushi vile nafuu vya Awali ( kama ilivypamriwa Jana jioni na TCRA ) ndipo nae afungashe Virago vyake.
Akijisahau akumbushwe kuandika barua kabla ya Pasaka.
 
Huyu jamaa nilikuwa namkubali sana ila ameniangusha
Alipokuwa Naibu Waziri wa Afya, alipambana vilivyo kwenye kupinga kujifukiza na barakoa za vitambaa nikaona kwa vile ni taaluma yake kasomea.

Lakini lilipokuja suala hili ameshindwa kabisa kupiga biti makampuni ya simu, nimemdharau sana na sina imani naye tena, akwende mbele huko
 
Huyu jamaa huwa ana kiburi sjawahi ona, roho mbaya sana, sijajua huwa ana tatizo gani kichwani!

Yaani bora abaki na ubunge tu!
 
Ahahahaaaa inawezekana akili yenyewe ndio haipo mkuu. Hapo lazima matokeo yawe kama hivi.
 
Tcra hii ya kilaba? Huwa anashauri waziri au anatangaza tu?

Kwani ewura wanapotangaza bei za mafuta guess waziri anapitisha?
 
Ahadi ni deni, rudi nyuma miezi michache kwenye ahadi ya Waziri utamuelewa tu mdau hapo juu.
Tuliahidiwa na nyerere, mwinyi, mkapa, jakaya na magu virus vingi Sana

VipiVipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…