Dkt. Ntuli Kaporogwe Kuwania Uongozi wa Jumuiya ya Afya ya Afrika Mashariki, Kati, na Kusini

Dkt. Ntuli Kaporogwe Kuwania Uongozi wa Jumuiya ya Afya ya Afrika Mashariki, Kati, na Kusini

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Tanzania Dkt. Ntuli Kaporogwe anatarajiwa kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye uchaguzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati, na Kusini (ECSA – HC).

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika leo Februari 11, 2025 kwenye Mkutano Mkuu wa 74 wa Mawaziri wa Afya wa Jumuiya hiyo unaoendelea kufanyika Jijini Lilongwe, Malawi.

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama wakati akimnadi Dkt. Ntuli amesema kuwa, ana uzoefu mkubwa katika utawala wa afya, maendeleo ya sera pamoja na uhamasishaji wa rasilimali na uimarishaji wa mifumo hasa ndani ya Wizara ya Afya ya Tanzania, uzoefu huu unamwezesha kuendeleza malengo ya ECSA-HC, ikiwa ni pamoja na huduma ya Afya kwa wote (Universal Health Coverage).

Snapinst.app_472606162_513249888031761_5030964249016473343_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom