Dkt. Nyambura Moremi ateuliwa tena kuwa Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa. Aliondolewa baada ya sampuli za mimea kukutwa na UVIKO-19

Dkt. Nyambura Moremi ateuliwa tena kuwa Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa. Aliondolewa baada ya sampuli za mimea kukutwa na UVIKO-19

Katiba mpya ni muhimu sana... Haiwezekana CEO wa shirika fulani anateuliwa tu. Tunatakiwa tubadilike. Ina maana kwa katiba hii naweza kwenda kijijini kwetu nikachukua classmate wangu akawa mkurugenzi hata bila ya vigezo
bila vigezo vip sasa šŸ’
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemrejesha kwenye nafasi yake aliyekuwa Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii (NPHL), Dk Nyambura Moremi aliyesimamishwa kazi Mei 4, 2020 kupisha uchunguzi.

Dk Moremi amerejeshwa ikiwa ni miaka minne, baada ya kuondolewa katika nafasi hiyo na Waziri wa Afya, baada ya Rais wa wakati huo, hayati John Magufuli kutia shaka usahihi wa vipimo vya Maabara ya Taifa vilivyothibitisha kuwapo Uviko-19 katika sampuli za wanyama na mimea.

images (32).jpeg

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Afya, Englibert Kayombo, Dk Moremi ameteuliwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa maabara hiyo, Medard Beyanga.

ā€œKwa kipindi chote Dk Moremi alikuwa Mkuu wa Idara ya Tafiti katika Maabara Kuu ya Taifa,ā€ amesema Kayombo.

Dk Moremi ni miongoni mwa wabobezi katika fani ya maabara na ni mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza.

Mwananchi
 
Huyu Moremi alipewa sampuli za oil na mapapai azipime kwenye mashine inayopima sampuli za vimelea za binadamu. Akatoa majibu.

Baada ya yale majibu Magufuli akamfuta kazi kuwa mashine zinatoa majibu ya uwongo.
Sasa si angezifuta kazi hizo mashine zilizotoa majibu ya uongo? Moremi alikosea nini?
 
JPM alikua Genius!! Hili halitokaa kufutwa.


Mlivyo wapumbavu, ... Walewale mnaompinga JPM kuhusu COVID-19 nahuyu mwanamke ,, ndo hao hao ambao Mara baada ya Samia kutangazia Dunia kua Kuna COVID bado mpaka Leo HAMJACHANJWA.

mnatembelea Nyota ya JPM.

*****.
 
Isije dr afunguke ilikuwa kweli hivyohivyo au alimnyima mtu uchi
Aseme ,mana hayupo
 
JPM alikua Genius!! Hili halitokaa kufutwa.


Mlivyo wapumbavu, ... Walewale mnaompinga JPM kuhusu COVID-19 nahuyu mwanamke ,, ndo hao hao ambao Mara baada ya Samia kutangazia Dunia kua Kuna COVID bado mpaka Leo HAMJACHANJWA.

mnatembelea Nyota ya JPM.

*****.
Wewe ndiyo hujachanja
 
Back
Top Bottom