Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 7,207
- 17,674
Waziri wa fedha aliyeweka rekodi ya kukaa kwenye uwaziri kwa kipindi chote cha miaka mitano ya rais Magufuli, wakati akihitimisha kusoma bajeti kuu ya serikali ametangaza kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuwataka wana Buhigwe wampe kura za ndiyo.
Mbunge wa Jimbo hilo kwa sasa ni Albert Ntabaliba Obama (55yrs) wa CCM.
Dkt Mpango anaenda kugombea ubunge akiwa kifua mbele baada ya kusimamia ufufuaji uchumi wa Tanzania na kuwa moja ya chumi zinazokua kwa kasi Afrika na duniani kwa ujumla, Dkt Mpango ndiyo amekuwa mtafutaji na mlipaji wa pesa zote kwenye miradi mikubwa ya nchi yetu kama vile SGR na bwawa la kufua umeme la Nyerere, hivyo wana Buhigwe na wana Kigoma kwa ujumla tembeeni kifua mbele kuwa mmepata mkombozi wa kweli hasa wakiungana na Prof Ndalichako.
Ni wakati sasa umefika kwa wana Kigoma kuachana na makanjanja na matapeli wa kisiasa kama akina Zito Kabwe ambao kazi yao ni kushinda Twita wakijikomba kwa mabeberu na kuichafua nchi kimataifa.