Dkt. Philip Mpango maneno uliyotamka siku unaapishwa yalitoka ndani ya moyo wako? Ulikuwa unawakebehi Watanzania?

Nasema hivi, pole. Huyo ni mtumwa wa ajira.
Sawa,lakini sio sababu ya kusema hawezi kujiajiri. Yeye kama mchumi mzuri aisaidie nchi yake,full stop.
 
Ahaaa ahaaa. Au ndio hao wachumi wenye PhD lakini ni motivational speakers?
Mkuu hao wanakubishia bure tu watu tunashuhudia huku mtaani wastaafu wanavoanzisha vibiashara vinakufa. Ukweli ni kwamba Waziri Mpango hana akili yoyote ya ku survive nje ya kuajiriwa maana angekua na uwezo huo angeshafanya hivyo.
 
Mkuu hao wanakubishia bure tu watu tunashuhudia huku mtaani wastaafu wanavoanzisha vibiashara vinakufa. Ukweli ni kwamba Waziri Mpango hana akili yoyote ya ku survive nje ya kuajiriwa maana angekua na uwezo huo angeshafanya hivyo.

Ndio namwambia huyo anayemsaifia eti ni mchumi mbobezi. Akope hata 1b kisha awekeze aone kama hajaishia kufa kwa BP.
 
Kuisaidia nchi ni lazima aajiriwe? Angekopa bank afungue viwanda vitoe ajira tuone nguvu ya PhD yake ya uchumi.
Hapo ndio unapokosea kwani kila mtu lazima awe mjasiriamali? Kisa tu ni mchumi. Nguvu ya Phd yake inaweza kutumika kama mtu anayeshauri taifa kwa masuala ya msingi ya kiuchumi.
 
Atafanya nini huyo mchumi fake zaidi ya kumsifia jiwe na kujifanya mtu wa dini saana kwa tuvifungu alitokariri?
Huyo ni aina ya wasomi waliokulia Dar na hawajui shida na kwao walikuwa hawaendi,yeye ndio tunapaswa kumshangaa kwa kushangaa Hali za wananchi
Kingine huyu ndio kawa mchumi toka enzi za Jk Hadi leo hii lakini hajui anachosimamia ,watu wa hivi ni wasomi maamuma wa kupuuzwa,seems anasimamia sera za uchumi za kwenye madafutari/nadharia.
Nilitegemea mchumi kama yeye aje na sera za kuinua kipato cha watu na kuwawekea mazingira rafiki kwenye urafutaji wa kipato lakini ndio Kila siku kuna utitiri wa kodi za kijinga,tra iko kukomoa watu badala ya kuwawezesha,wao mipango yao ni kununua ndege na kujenga airports kwa ajili ya watu wasio na uwezo wa kupanda yaani Hawa wasomi ni shida tupu
 
We jamaa una matatizo? Mtu mwenye PHD ya uchumi hawezi kujiaajiri?
Kwani cha ajabu nini? Kuna uhusiano upi Kati ya phd ya uchumi na kujiajiri? Hukumsikia malaika wenu anasema kuna mtu alikuwa na phd lakini walikuwa nae lumumba anazhngukazunguka huku wanamlipa laki 6 ndio wakamteua ukuu wa wilaya?
 
Sio Tanroads huyo alitolewa kufundisha uchumi mlimani/ udsm akapewa kuwa mtendaji mkuu wa tume ya uchumi enzi za BRN kipindi cha Jk ndio kawa na muendelezo wa kaxi za kuajiriwa Hadi leo,kifupi hawezi kazi yoyote nje ya kuajiriwa ndio maana malaika wao alijigamba kumtukana lakini jamaa hakuwa na cha kufanya kutunza utu wake
 
Sawa,lakini sio sababu ya kusema hawezi kujiajiri. Yeye kama mchumi mzuri aisaidie nchi yake,full stop.
Wewe kwa akili yako hiyo kaz ya uchumi ndo kaanza leo? Nini amesaidia miaka yote ambacho anaweza fanya leo? Hana kipya huyo
Binafsi ningekuwa Rais kwenye nafsi kama hizi ningeweka watu wenye exposure na biashara tena za kimataifa sio kuchukua ma academician na kuwapa nafasi nyeti hakuna watafanya nje ya makaratasi waliyokariri si ajabu msukuma huwa anawaponda
 
Hapo ndio unapokosea kwani kila mtu lazima awe mjasiriamali? Kisa tu ni mchumi. Nguvu ya Phd yake inaweza kutumika kama mtu anayeshauri taifa kwa masuala ya msingi ya kiuchumi.
Miaka yote kashauri nini au ushauri wao ndio huo wa tiaraei?
 
Umewaona hao wa bureau tu, vipi wale Wajasiriamali waliokuwa na pesa zao benki zilizosimamishwa na wakaambulia 1.5m kati ya 50m au 70m Mtu alizokuwa nazo kweye akaunti?.

Kwa ufupi tupo wengi tunaoamini Wanasiasa wana namna yao ya kutafsiri mambo tofauti kabisa na hali halisi. Nimetumia Wanasiasa kwa sababu hata uwe na phd kumi ukishaingia siasa phd zote zinafunikwa....kumbuka kuna tofauti ya kutamani kufanya jambo na kujua namna ya kulifanya hilo jambo litokee.

Mwanasiasa akikuita Masikini au Mnyonge actually zaidi anamaanisha "Mpiga kura".
 
Mpango ana ukakasi,hajui basic ya uchumi wa mtu mmoja ndio uchumi halisia.Wezesha wananchi uone tafsri halisi ya kukuwa kwa uchumi.
Hajui ateme au amungunye amegeuka popo.
Magufuli hana rafiki wa kudumu nafasi itaenda kwa Hussein Bashe ndio mwenye bongo ya kiti hiki.
 
Makusanyo kutoka bil 8 mpaka tril 1.7 hulioni hilo?
 
Hana jipya ameshawaagiza TRA wahakikishe wakusanya trilioni 2 kila mwezi ,
Wanaendelea kutukamua tu , wakati malisho yenyewe hakuna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…