The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha amesema kupitishwa kwa Sheria ya TBC kunatokana na mapenzi makubwa aliyonayo Rais Samia Suluhu Hassan kwa shirika hilo.
Akizungumza mkoani Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa TBC, Dkt. Rioba amesema utashi wa Rais Samia wa kutaka maendeleo ya TBC ndio umesukuma sheria hiyo kupelekwa bungeni na hatimaye kupitishwa.
Amesema Serikali pia imekuwa ikilisaidia shirika hilo katika kutekelezea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuongeza usikivu wa redio ya Taifa kutoka asilimia 54 mpaka asilimi 92 kwa sasa.
Dkt. Rioba ameongeza kuwa maboresho ya studio za redio ni sehemu ya maendeleo yaliopigwa na TBC, na miradi yote hiyo inatumia pesa za ndani.
Baraza la wafanyakazi wa TBC linafanyika mkoani Dar es Salaam ambapo mambo mbalimbali yanajadiliwa ikiwa ni pamoja na maendeleo ya shirika hilo kwa ujumla.