Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MHE. DKT. RITTA KABATI KUTOA BIMA ZA AFYA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM MKOA WA IRINGA
Kabati ameyasema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi kadi za bima ya afya 172 zilizotolewa na taasisi ya Rounding Hands kwa kushirikiana na Online Tv ya Makutano ambapo hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya taasisi ya Nyumba Ali iliyopo Manispaa ya Iringa.
Aidha, Mhe. Kabati amesema bima za afya kwa watoto wenye mahitaji maalum zina umuhimu mkubwa kulingana na watoto wengi kuhitaji matibabu ya mara kwa mara hali inayopelekea changamoto kubwa kwa wazazi wasio na uwezo wa gharama za matibabu.
Mhe. Kabati amewataka wadau zaidi kujitolea kwa watoto wenye mahitaji maalum kwa kuwapa vitu wezeshi vitakavyosaidia kupunguza changamoto walizo nazo.
Katika hatua nyingine Mhe. Kabati, amelaani vikali tabia za watu katika jamii kuonesha vitendo vya unyanyapaa pamoja kuwafanyia vitendo vya ukatili watu wenye ulemavu wakiwemo watoto wenye mahitaji maalum.