Dkt. Rugemeleza: Kwa DP World, Samia na serikali yake wameisaliti nchi

Ww tu
 
Sagia kunguni kutoka angle zote hadi waone aibu.
 
Ni kweli kabisa, ameisaliti nchi, amewasaliti wananchi wenzake pamoja na maslahi yao yote kabisa. Kwa mtu mwenye akili zako timamu kabisa, ambaye ni mzalendo wa kweli kwa nchi yako huwezi kukubali kuingia au kukubali kusaini mkataba wa namna ile. Nafsi lazima itakusuta tu, huwezi kukubali mkataba kama ule. Alichifanya ni usaliti mkubwa sana, Mimi binafsi sikutegemea kitu kama hicho kinaweza kufanywa na mtu wa kaliba kama yake. Kutokana na Mkataba huu namna ulivyo, Mimi roho inaniuma sana kuona nchi yangu niliyozaliwa inahujumiwa makusudi namna hii. Roho inaniuma sana. Kitendo hiki kibaya walichofanya ni sawa na Nahondha ameamua kutoboa meli anayoiongoza ili kusudi maji yaingie ndani ya Meli na kisha meli yote izame kwenye maji ikiwa na abiria wake pamoja na mizigo yao yote. Mbaya sana hiyo!!
 
Sisi layman wanatuchanganya kwakweli, majaliwa alisema mkataba uko poa, na wengine wamepeleka kesi mahakamani kupinga mkataba, Rugemeleza anasema raisi ame*ea katiba kupitia huo mkataba!
 
Sisi layman wanatuchanganya kwakweli, majaliwa alisema mkataba uko poa, na wengine wamepeleka kesi mahakamani kupinga mkataba, Rugemeleza anasema raisi ame*ea katiba kupitia huo mkataba!
Kwa hiyo ushauri wako ni kwa nani kuwanusuru ma laymen wasichanganywe?
 
Mjumbe hauwawi!
 
Mwanafunzi wako tulia amesapoti hii agreement.
Unahisi kwa nini amesapoti?
1. Yawezekana kweli mkataba ni mzuri
2.Yawezekana ameusapaoti bila kuulewa (kwa kutojua) - kama wengi tulivyo
3. Yawezekana ameusapoti kwa kuujua ukweli wake lakini akafumba au akafumbwa macho (kama inavyohisiwa kwa wabunge walioenda Dubai)
4. Yawezekana ameusapoti kwa kuogopa yalimkuta Ndugai - ukumbuke mkataba uliletwa bungeni baada ya kuwa umesainiwa tayari
Tena niliona mle bungeni spika alionekana kuufahamu vizuri mkataba kuliko wengine wote; ni kama alishausoma muda mrefu kabla. Ndiyo maana aliweza kuwavuruga akina Halima kila alipoona wanakwenda kugusa penye tatizo, anawatoa kwenye reli. Hivyo basi nyinyi wanasheria mkutane naye awaeleze, nayi mumueleze kile ambacho kimekaa vibaya. Mnajua bado mwenye uwezo wa kubadilisha hili jambo ni yeye, Nimeona kuna mahali mmeshauri Bunge likae upya na kufuta azimio/ridhaa yake kama njia pekee iliyobaki, Mwenye kuamua Bunge likae upya ni yeye.
 
Umeandika ujinga alafu upo busy kushare link
 
Namba 3 na 4 ndio ukweli wenyewe
 
Mwezi huu hutopata hedhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…