Habari wasomaji na wananchi wote.
Je, tumekuwa Taifa la ovyo hivi.
Je, hili ni suluhisho la mjadala katika mambo ya Kitaifa?
Akiuawa, tunatuna ujumbe gani.
Pia soma
---
Ndugu Watanzania!
Dkt. Rugemeleza Nshala ametujulisha kuwa maisha yake yako hatarini. Wakili Dkt. Nshala anasema kuwa ametaarifiwa juu ya mipango ya kutaka kumuua (assassination) inayopangwa dhidi yake! Vitisho dhidi ya maisha ya Wakili Dkt. Nshala vinakuja muda mfupi tu baada ya yeye kutoa maoni yake kwa hisia kali akipinga Mkataba wa Bandari kati Serikali ya Tanzania na Ufalme wa Dubai.
Dkt. Rugemeleza Nshala, ambaye alikuwa Rais wa Tanganyika Law Society (TLS) ni wakili na mwanasheria mbobevu anayejua vema mipaka yake kikatiba na kwa nafasi yake anao wajibu wa kutoa ushauri na maoni kwa Watanzania katika masuala ya sheria na katiba ya nchi.
Sisi Askofu tumepata muda wa kuomba na Dkt. Nshala na kumtia moyo kuwa asiogope kwani alitoa maoni yake kama raia anayeipenda nchi yake na hakuvunja sheria ye yote ya nchi. Kwa maoni yetu, watu wanaomtisha Dkt. Nshala au wanaotaka kuondoa uhai wake ni watu waoga ambao wanataka kumchafua Rais Dkt. Samia ili dunia ifikiri ameanza kuwaua wakosoaji wake.
Kwa hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa watu, kikundi, vikundi hata taasisi ambao wanapanga kutoa uhai wa Dkt. Nshala pamoja na wanaharakati wengine wanaotoa maoni yao au hata kuikosoa Serikali kuhusiana na suala la Mkataba wa Bandari waache mara moja. Kama wao wanafikiri kuwa Dkt. Nshala na wenzake wamefanya kosa lo lote kisheria, wawapeleke mahakamani badala ya kuanza kuwatisha.
Kutisha watu na kutaka kuwaondoa au kuwaua watu nje ya mfumo wa kisheria ni uhaini, uuaji, unyama na ujambazi bila kujali mtu anayefanya matendo hayo. Sisi Askofu tunatoa tahadhari hii kama kukinga mapema ili watu hao wajue kuwa wanachokipanga kufanya hakikubariki. Kama Dkt. Nshala na wenzake watadhulika kwa lolote, watu waliowahi kutoa kauli zao kwa lengo la kuwatisha, hao watawajibika. Kukinga ni bora kuliko kutibu! Tumetimiza wajibu wetu!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 6 Julai 2023; 09:39 am.
View attachment 2680028