Dkt. Rugemeleza Nshala: Nimetishiwa maisha baada ya kutoa maoni kuhusu mkataba wa Bandari na DP World

Habari wasomaji na wananchi wote.

Je, tumekuwa Taifa la ovyo hivi.

Je, hili ni suluhisho la mjadala katika mambo ya Kitaifa?

Akiuawa, tunatuna ujumbe gani.

Pia soma

---
Ndugu Watanzania!
Dkt. Rugemeleza Nshala ametujulisha kuwa maisha yake yako hatarini. Wakili Dkt. Nshala anasema kuwa ametaarifiwa juu ya mipango ya kutaka kumuua (assassination) inayopangwa dhidi yake! Vitisho dhidi ya maisha ya Wakili Dkt. Nshala vinakuja muda mfupi tu baada ya yeye kutoa maoni yake kwa hisia kali akipinga Mkataba wa Bandari kati Serikali ya Tanzania na Ufalme wa Dubai.

Dkt. Rugemeleza Nshala, ambaye alikuwa Rais wa Tanganyika Law Society (TLS) ni wakili na mwanasheria mbobevu anayejua vema mipaka yake kikatiba na kwa nafasi yake anao wajibu wa kutoa ushauri na maoni kwa Watanzania katika masuala ya sheria na katiba ya nchi.

Sisi Askofu tumepata muda wa kuomba na Dkt. Nshala na kumtia moyo kuwa asiogope kwani alitoa maoni yake kama raia anayeipenda nchi yake na hakuvunja sheria ye yote ya nchi. Kwa maoni yetu, watu wanaomtisha Dkt. Nshala au wanaotaka kuondoa uhai wake ni watu waoga ambao wanataka kumchafua Rais Dkt. Samia ili dunia ifikiri ameanza kuwaua wakosoaji wake.

Kwa hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa watu, kikundi, vikundi hata taasisi ambao wanapanga kutoa uhai wa Dkt. Nshala pamoja na wanaharakati wengine wanaotoa maoni yao au hata kuikosoa Serikali kuhusiana na suala la Mkataba wa Bandari waache mara moja. Kama wao wanafikiri kuwa Dkt. Nshala na wenzake wamefanya kosa lo lote kisheria, wawapeleke mahakamani badala ya kuanza kuwatisha.

Kutisha watu na kutaka kuwaondoa au kuwaua watu nje ya mfumo wa kisheria ni uhaini, uuaji, unyama na ujambazi bila kujali mtu anayefanya matendo hayo. Sisi Askofu tunatoa tahadhari hii kama kukinga mapema ili watu hao wajue kuwa wanachokipanga kufanya hakikubariki. Kama Dkt. Nshala na wenzake watadhulika kwa lolote, watu waliowahi kutoa kauli zao kwa lengo la kuwatisha, hao watawajibika. Kukinga ni bora kuliko kutibu! Tumetimiza wajibu wetu!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 6 Julai 2023; 09:39 am.

View attachment 2680028
Yaaani uhuru wote huu wa kutoa maoni bado kuna watu wanatengeneza hadithi? Katoa maoni Jaji Warioba, Profesa Shivji, Profesa Lipumba, BAKWATA, TEC na Mbowe ambaye alitumia maneno baadhi ya kuudhi hakuna alietishwa iweje kwa wakili flan mmoja tu? TLS imezungumza hawakutishwa. Hebu tuache kutaka kuichafua nchi. Uhuru wa maoni ni mkubwa mno. Muhimu tuutumie kwa maendeleo na nidhamu.🙏🙏🙏
 
Awe makini
 
Nafikiri hujui undani wa masuala haya.
 
Anatafuta umarufu kupitia bandari , mbona watu wengi wakiwemo na maprofesor wamesema mengi kuhusi hiyo bandari ila hamna anaetishiwa, wewe ni mzalendo muoga kwanini hutaki kusimamia ulicho sema kama kufa ufe nakuja kulalamika ili iweje
Hata kwa Tundu Lissu wakati ule mlisema hivi hivi. Kumbuka, mwezi uliopita yaani Mwezi Juni, 2023 walijipitishia Sheria yao ya Kutoshitakiwa Mahakamani pale wanapotaka kumuua mtu yoyote yule katika nchi hii, Sheria hiyo ipo na inafanya kazi sasa hivi.
 
Wasiojulikana bado wapo, kama walifanya kazi huyu msaliti akiwa msaidizi na hakuwahi kuwakemea, sitashangaa msaliti nae akiamua kuwaacha wasiojulikana wamsaidie kuwafunga watanganyika midomo wanaolilia ardhi yao iliyopewa mwarabu.

Anawaacha wasiojulikana wamsaidie kwasababu ameshaona maji yamezidi unga, watanganyika wanachachamaa, japo alijidai kuziba masikio lakini sasa anaona kelele zinazidi, huku majibu ya maswali ya watanganyika akiwa hana, Samia anaelekea kuchanganyikiwa.

Huyu mtu anayeelekea kuchanganyikiwa anaweza kuja kuwa dikteta mbaya zaidi ya wote, kwasababu anajua anaongoza watu wasiomuamini, hivyo hata akijitahidi vipi itakuwa ngumu kwake kurudisha imani kwao, lakini pia, mamlaka makubwa aliyopewa kikatiba, anaweza kuyatumia kuwaumiza anaowaongoza, hasa kwa tabia zake za kukomoana kama alivyomfanya Job.
Tanzania ni nchi ya waungwana na waoga pia, japo pia upande mwingine wapo mashetani, wabinafsi, wauaji, waporaji na viongozi madikteta na walaghai.

Lakini kwaajili ya hao waungwana, waoga na wenye haki wachache, Mungu huwapigania. Kwaajili yao, hakuna atakayeua au kutaka kuua atakayeishi.

Rais Samia akiwategemea wauaji, naye atakuwa ameisha. Atakayeua kwaajili ya mtawala atakuwa anaharakisha kifo chake na cha mtawala.
 
Tanzania ni nchi ya waungwana na waoga pia, japo pia upande mwingine wapo mashetani, wabinafsi, wauaji, waporaji na viongozi madikteta na walaghai.

Lakini kwaajili ya hao waungwana, waoga na wenye haki wachache, Mungu huwapigania. Kwaajili yao, hakuna atakayeua au kutaka kuua atakayeishi.

Rais Samia akiwategemea wauaji, naye atakuwa ameisha.
Karibia tawala zote za Afrika uwepo wake madarakani wanategemea Wauaji.
 
Anatafuta umarufu kupitia bandari , mbona watu wengi wakiwemo na maprofesor wamesema mengi kuhusi hiyo bandari ila hamna anaetishiwa, wewe ni mzalendo muoga kwanini hutaki kusimamia ulicho sema kama kufa ufe nakuja kulalamika ili iweje
stupid!
 
Habari wasomaji na wananchi wote.

Je, tumekuwa Taifa la ovyo hivi.

Je, hili ni suluhisho la mjadala katika mambo ya Kitaifa?

Akiuawa, tunatuna ujumbe gani.

Pia soma

-
Kwa mujibu wa ibara ya 14 ya katiba ya nchi yetu kila mtu ana haki ya kuishi na kwamba anapaswa kupata hifadhi ya maisha yake kutoka kwenye jamii hiyo.

Maneno yaliyosemwa dhidi yake na watu wengine waliojiita masheikh yalikuwa yanasikitisha kwa mtu ambaye anamfahamu Profesa Issa Shivji kwa uzalendo wake na utumishi wake uliotukuka na kujitoa kwake kwa nchi yetu, wale watu walikuwa wanaongea kana kwamba ni maneno yao bali kulikuwa na watu ambao walikuwa nyuma yao.

Damu yangu kama itamwagika basi ikapalilie mapambano ya kulinda rasilimali za nchi yangu Tanzania.

Mtu hawezi kuishi katika nchi ambayo ni Jamhuri na watu wengine wakawa na leseni ya kuondoa uhai wao. Mwenye leseni, ruhusa na mamlaka pekee ya kuondoa uhai wa mtu hapa duniani ni Mwenyezi Mungu pekee.

Kiukweli kuua watu kupo na watu wamefariki, watu wamejeruhiwa na kupata matatizo makubwa. Kufuatia hilo nimeamua kuja mbele ya umma wa Watanzania kuwaambia kwamba mimi Rugemeleza Nshala maisha yangu yako hatarini. Kuna maagizo kutoka ndani kwamba nitakapopatikana niteketezwe, niangamizwe na kuitwa marehemu.

Mkataba huu wa bandari umesainiwa au umepewa kibali kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kibali hiko kinaonekana katika kiambatanisho kimojawapo katika mkataba huo ambacho kina saini ya Rais Dkt. Samia

=============

Wakili wa kujitegemea Dkt.Rugemeleza Nshala amesema amepokea taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya mifumo kuwa anatakiwa kuuwawa kwa kile alichokieleza kuwa ni kutokana na msimamo wake dhidi ya watu waliojitokeza kumshambulia kwa maneno ya kejeli na kuudhi Prof.Issa Shivji baada ya msomi huyo wa sheria kutoa maoni yake dhidi ya sakata la uwekezaji wa Bandari linaloendelea sasa hapa nchini

Akizungumza na Wanahabari kwenye ukumbi wa Mesuma Hotel, Makumbusho Jijini Dar es Salaam, Dkt.Nshala ambaye pia amewahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ameeleza kuwa hivi karibuni kupitia jukwaa la 'club house' alitoa maneno makali ambayo kiuhalisia amedai kuwa ndio msimamo wake dhidi ya watu hao ambao anaamini kuwa walichokizungumza si maneno yao bali wanatumiwa na watu wenye mamlaka nchini kutoa lugha za kashfa na kuudhi dhidi ya mtu mwenye umri mkubwa na anayestahiki heshma kubwa dhidi yao kwenye jamii

Dkt.Nshala aliyefika kwenye Kikao hicho akiwa amebeba Vitabu viwili alivyoeleza kuwa anavyoviamini zaidi (Biblia na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) amesema anawaeleza wenye mamlaka walio nyuma ya mpango huo kuwa yuko tayari kufa kwaajili ya nchi yake

Ikumbukwe kuwa kupitia jukwaa hilo ambalo lilijadili mjadala wa kina kuhusiana na uwekezaji wa Kampuni ya DP World ya Dubai kwenye Bandari, Dkt.Nshala alitoa kauli zolizoonekana kuwashambulia zaidi viongozi waandamizi serikalini akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa nk

---
Ndugu Watanzania!
Dkt. Rugemeleza Nshala ametujulisha kuwa maisha yake yako hatarini. Wakili Dkt. Nshala anasema kuwa ametaarifiwa juu ya mipango ya kutaka kumuua (assassination) inayopangwa dhidi yake! Vitisho dhidi ya maisha ya Wakili Dkt. Nshala vinakuja muda mfupi tu baada ya yeye kutoa maoni yake kwa hisia kali akipinga Mkataba wa Bandari kati Serikali ya Tanzania na Ufalme wa Dubai.

Dkt. Rugemeleza Nshala, ambaye alikuwa Rais wa Tanganyika Law Society (TLS) ni wakili na mwanasheria mbobevu anayejua vema mipaka yake kikatiba na kwa nafasi yake anao wajibu wa kutoa ushauri na maoni kwa Watanzania katika masuala ya sheria na katiba ya nchi.

Sisi Askofu tumepata muda wa kuomba na Dkt. Nshala na kumtia moyo kuwa asiogope kwani alitoa maoni yake kama raia anayeipenda nchi yake na hakuvunja sheria ye yote ya nchi. Kwa maoni yetu, watu wanaomtisha Dkt. Nshala au wanaotaka kuondoa uhai wake ni watu waoga ambao wanataka kumchafua Rais Dkt. Samia ili dunia ifikiri ameanza kuwaua wakosoaji wake.

Kwa hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa watu, kikundi, vikundi hata taasisi ambao wanapanga kutoa uhai wa Dkt. Nshala pamoja na wanaharakati wengine wanaotoa maoni yao au hata kuikosoa Serikali kuhusiana na suala la Mkataba wa Bandari waache mara moja. Kama wao wanafikiri kuwa Dkt. Nshala na wenzake wamefanya kosa lo lote kisheria, wawapeleke mahakamani badala ya kuanza kuwatisha.

Kutisha watu na kutaka kuwaondoa au kuwaua watu nje ya mfumo wa kisheria ni uhaini, uuaji, unyama na ujambazi bila kujali mtu anayefanya matendo hayo. Sisi Askofu tunatoa tahadhari hii kama kukinga mapema ili watu hao wajue kuwa wanachokipanga kufanya hakikubariki. Kama Dkt. Nshala na wenzake watadhulika kwa lolote, watu waliowahi kutoa kauli zao kwa lengo la kuwatisha, hao watawajibika. Kukinga ni bora kuliko kutibu! Tumetimiza wajibu wetu!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 6 Julai 2023; 09:39 am.

View attachment 2680028
huyo tapeli tu anatafuta umaarufu, auawe mtu km kwa lipi hasa? Acheni utapeli
 
"Kwa hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa watu, kikundi, vikundi hata taasisi ambao"

Why is he referring to himself as "SISI"...?
 
Watanganyika wanalalamika uhuru wao ndani ya mipaka ya nchi yao uko hatarini. Hiyo kadi ya Chadema ulimpa wewe? Kwa akili zako fupi hujui iko siku hata wewe hali yako inaweza kuwa mbaya, Askofu Mwamakula atageuka mtetezi wako
Tambua tu, aliyezoea kula nyama za watu huwa haachi, akiwamaliza wa mbali, atawageukia ndugu zake.
Kwanza kabisa hakuna watanganyika. Wewe ni mtabiri kwamba kuna siku hali yangu itakuwa mbaya na huyo Askofu wa CHADEMA awe mtetezi wangu? Acha utabiri wa kishenzi.
 
Serikali chini ya Mh Samia sidhani Kama ni serikali ya visasi na kuuwa watu..Kwa wingi wa utu,ubinadamu na unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu alionao Kiongozi Mkuu wa nchi naamini hawezi ruhusu Damu Za watu zichafue taswira nzuri ya mema mengi na mazuri aliotenda..

Wanaoongoza Serikali ni watu (Wana dini na maadili ya ubinadamu)..Kukosolewa,Kushauriwa na kusahihishwa si jambo la vita..Kikubwa wakosoaji yapasa kuwa na staha na heshima..Matusi,kejeli,dharau havipaswi kuwa msingi wa hoja..Tutoe maoni,Ushauri na mapendekezo Kwa lugha ya kiungwana..

Mwisho,Uongozi ni jalala..Viongozi msiache kusamehe wananchi wanapokosea..Msamaha ni kitendo kinachompendeza mwenyezi Mungu wakati wote ili mzidi kupata Neema,rehema na fadhili..

Kuna maisha baada ya Uongozi,vyeo,Mamlaka na Tunu mbalimbali..Tuwe wanyenyekevu
 
Back
Top Bottom