Dkt. Rugemeleza Nshala: Nimetishiwa maisha baada ya kutoa maoni kuhusu mkataba wa Bandari na DP World

Dkt. Rugemeleza Nshala: Nimetishiwa maisha baada ya kutoa maoni kuhusu mkataba wa Bandari na DP World

If they kill you, your blood will speak more than your mouth spoke.

Tutachinjana hadharani. Waache ujinga. Tanganyika yetu haiuzwi.

Walimuua Dr. Mvungi kwa katiba. Huyu hatutakubali
Utafanya nini? msitafute kick mijini nani anashida na mtu hana impact yoyote. Eti vyanzo kuna watu watafuta kick tu ndio kwanza namjuwa leo.
 
إِنَّ ٱلْمُسْلِمِينَ وَٱلْمُسْلِمَٰتِ وَٱلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَٰتِ وَٱلْقَٰنِتِينَ وَٱلْقَٰنِتَٰتِ وَٱلصَّٰدِقِينَ وَٱلصَّٰدِقَٰتِ وَٱلصَّٰبِرِينَ وَٱلصَّٰبِرَٰتِ وَٱلْخَٰشِعِينَ وَٱلْخَٰشِعَٰتِ وَٱلْمُتَصَدِّقِينَ وَٱلْمُتَصَدِّقَٰتِ وَٱلصَّٰٓئِمِينَ وَٱلصَّٰٓئِمَٰتِ وَٱلْحَٰفِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَٱلْحَٰفِظَٰتِ وَٱلذَّٰكِرِينَ ٱللَّهَ كَثِيرًا وَٱلذَّٰكِرَٰتِ أَعَدَّ ٱللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا
“Indeed, the Muslim men and Muslim women, the believing men and believing women, the obedient men and obedient women, the truthful men and truthful women, the patient men and patient women, the humble men and humble women, the charitable men and charitable women, the fasting men and fast women, the men who guard their private parts and the women who do so, and the men who remember Allah often and the women who do so – for them Allah has prepared forgiveness and a great reward.” [al’Ahzaab 33:35]
 
Wewe ndie huna hoja, unaandika upuuzi mtupu. Wasiojulikana wapo na tulishaona walichomfanya Lissu, ana haki ya kutoa taarifa kuhusu uhai wake.

Asipuuzwe.
Taarifa kwa nani? angemwambia mkewe sisi anatuhusu nini.
 
huyo mjinga tu masifa ya kihaya yamemjaaa
Sana unaliona tu na sura lake jitu linatafuta sifa wewe mtaani tu watu hawakujui eti natishiwa. Kwanza kwa kauli zake hizi kutishia mamlaka wangempa anachostahili wamekuta Rais mpole tu.
 
It is by Allah’s mercy that you are gentle to them; and had you been harsh and hardhearted, surely they would have scattered from around you. So excuse them, and plead for forgiveness for them, and consult them in the affairs, and once you are resolved, put your trust in Allah. Indeed Allah loves those who trust in Him.” (Quran 3:159)
 
Undani gani ndugu yangu wakati mjadala uko wazi kwa kila mtu kutoa maoni? Labda kama ana mambo yake tinted huko. Uhuru wa maoni nchini ni mkubwa mno. 🙏🙏🙏
Huyu hakutowa maoni ametowa Suluhu na hicho ni kitu hatari sana kuelimisha wajinga na wakamwelewa amesoma Yale,Harvard na wakimgusa itakuwawkazi kwao kwani aliosoma nao ndio wengi wanatoa misaada Tanzania kwa hiyo wamtumie akili yake kama sio fisadi wa kununulika la sivyo watadumbuana nae sana ana akili na Dr wa veti fake na vyuo fake
 
"Kwa hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa watu, kikundi, vikundi hata taasisi ambao"

Why is he referring to himself as "SISI"...?
Makanisa mengi ta walokole unakuta uongozi ni wa mchungaji na mama mchungaji (mke wa mchungaji).

Labda anaposema sisi anamaanisha uaskofu wake ni wa yeye na mkewe!

Just thinking aloud.
 
Huyu Mwamakula ni askofu wa CHADEMA hivyo apuuzwe. Achague kuwa askofu au mwanasiasa. Anachofanya hakikubaliki kwa Mungu wala kwa shetani. NI MNAFIKI
Huwa anawauliza watu kuwa wapo mrengo gani kabla ya kuwapazia sauti ili haki itendeke!!??
Yeye ni mtetezi wa haki bila kujali chama,itikadi,dini wala dhehebu.
 
MAISHA YANGU YAPO HATARINI;WAKILI DKT NSHALA RUGEMELEZA AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.

"Damu yangu kama itamwagika basi ikapalilie mapambano ya kulinda rasilimali za nchi yetu Tanzania" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWa Habari

"Kuna maagizo kutoka ndani yanayosema,Mimi nikionekana niteketezwe,nimalizwe,niuawe,na jina langu liwe refu lianze na Marehemu Rugemeleza Albert Kamwagwa Nshala" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza

"Kama wenye dhamana watapenda Mimi niondoke,niitwe Marehemu basi yatawapata makubwa,vizazi vyao mia nne na arobaini vitakwenda kuteseka na kujibu juu ya jambo hili" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.

"Siko tayari kupigishwa magoti,kunyamazishwa au kukandamizwa na mtu yeyote ambaye kikatiba na Yeye ni Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Mimi" Wakili Dkt. Nshala Rugemeleza.

"Nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko,sitatishiwa na binadamu mwenzangu anayeumbwa kama Mimi,anayeenda chooni kama Mimi,anayeumwa kama Mimi,anayekufa kama Mimi"Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.

"Nimetumia lugha nyepesi sana,na laini kwa walichotufanyia viongozi wetu,kama ingekuwa ni huru na kawaida basi viongozi wetu wangekuwa mbele ya sheria muda huu tunavyozungumza" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza.

"Mfumo wetu ni ule ambao hata Rais akikukanyaga unasema ooh ahsante kwa kunikuna" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza

"Sitasalimu amri,nitaendelea kupinga ugawaji huu wa rasilimali za nchi yetu,nitasimama na maneno yangu" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza

"Mkataba huu mbaya kuwahi kutokea Rais anahusika Moja kwa Moja kwa sababu sahii yake ipo mwisho wa jedwali la mkataba,Marais uwa hawasaini lakini yeye kasaini"Wakili Dkt Nshala Rugemeleza#MkutanoWaWaandishiWaHabari

"Bunge la mwaka 2017 lilitunga sheria kuhusu mikataba ya rasilimali zote zipite bungeni,ila mkataba wa bandari unasema Dp World haiusiki na sheria hiyo" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza

"Mkataba huu unalimbikiza Mali zote za nchi hii kuhusiana na bandari kwa kampuni binafsi ya DP World,sheria inasema tulinde maliasili kwa ajili ya kizazi hiki na vizazi vijavyo,hiki ndicho kilichotufanya tunyanyuke tupinge" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza

"Kama nasema uwongo nashika biblia yangu Mimi ni mkristo,nianguke chini Mungu achukue uhai wangu" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.

"Nimesoma digrii yangu ya kwanza Udsm,digrii ya pili Havard,nikaenda kusoma digrii ya tatu Yale na PhD Havard baada ya kutoelewa lugha iliyozungumzwa kwenye mgogoro wa Bulyakhuru" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.

"Tuna haki ya kulinda maliasili za Taifa kama zipo hatarini,sio kama mkubwa hakosei,Bandari ni mali ya Watanzania wote, tuna haki kuhoji au hata ikiwezekana kwenda mahakamani kama Mali za nchi zinauzwa"Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.

"Naipenda nchi yangu Tanzania,nipo tayari kuifia nchi yangu,na kama huu ni mwisho wangu basi nasema kwa herini tutaonana Paradiso" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.
 
Daah, hatari, ila..

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

Tanganyika wazanzibar wanachukua Mali yetu kisa Cha muwekezaji jamani.
WHY WHY BANDARI ZA ZANZIBAR No. KUWA FAIDA WACHUKUE WAO TU YOTE HATA TANGANYIKA ISIPATE FAIDA YA 0TZS. HUKU MASIKINI WAKIUMIZWA NA KODI YA MIAMALA NA KILA SEHEMU IMEJAA KODI WHY HUYO ASEMEHEWE KODI HAMUONI KUWA HAO JAMAA WANAJILIPA KWENYE BANDARI KAMA WENGINE WALIVYOKWISHAJILIPA KWENYE UMEME, GESI NA MAFUTA WAO TU NDIO MADILA BASI PAMOJA NA SUKARI.

WATU MMELALA SIJUI MTAJUJA KUWAAMBIAJE WAJUKUU ZENU WATAKAPOKUWA HAWANA PA KWENDA NA KUTUMIKISHWA KAMA PUNDA NA HUKU WEWE UMESHIBA LEO PEKEE.

JAMANI ACHENI UOGA KIZAZI CHA AKINA NYERERE WALITESEKA SIE TUWE HURU WHY SIE TUNAKUWA WAOGA NA ASKARI ANAGANYA KAZI KAMA ROBOTI ANAUA MTU ANAYETETEA TAIFA KISA CHA AJIRA YAKE AMBAYO KWANZA INAMFANYA AWE MASIKINI.
ANGALIENI NCHI YETU IMESHAUZWA IMEISHA PORI TENGEFU, MADINI YAMEISHA YOTE WANAWAPA WATU KWA GAWIO LA SIRI KIVYAO NA SIO LA SERIKALI.

BAADAYE UNAKAMULIWA KODI MPAKA VIMA YAISHE.


YAANI HUJIULIZI UNALIPWA SALARY KODI, UKITOA HELA BANK KODI, UKIITUMA KODI, UKIITOA ULIYOTUMIWA KODI, UKINUNUA KITU KODI , YAANI KUNA KODI NYINGI MNO UNALIWA MPAKA UNAKUJA KUIPATA HELA YAKO.
HUKU WATU WAKIWAPA MA EX WAO GARI ZA 500M.
ASKARI usifanye kazi Kama roboti kuwa Ni amri unaumiza wananchi wanaotetea maisha mpaka ya mjukuu wako. Usiwaze tumbo lako Leo tu.
Unataka wazanzibar WACHUKUE bandari yetu mbona wao za kwao hazimo.

Yaani wasamehewe Kodi asilimia kweli afande wewe unayetumwa jamani na huku sie kila kona Kodi na maisha ya wananchi hawapati huduma za muhimu. Haya tuueni Mana nyie mtaishi milele.Ivi kweli kuwa jamaa wasemehewe Kodi ili iweje na kwa faida ya Nani na bandari inachukuliwa Kama shamba la mtu milele ,

Ila kweli kuwa mwanasiasa hata jambazi anao uafadhali
 
Habari wasomaji na wananchi wote.

Je, tumekuwa Taifa la ovyo hivi.

Je, hili ni suluhisho la mjadala katika mambo ya Kitaifa?

Akiuawa, tunatuna ujumbe gani.

Pia soma

-
Kwa mujibu wa ibara ya 14 ya katiba ya nchi yetu kila mtu ana haki ya kuishi na kwamba anapaswa kupata hifadhi ya maisha yake kutoka kwenye jamii hiyo.

Maneno yaliyosemwa dhidi yake na watu wengine waliojiita masheikh yalikuwa yanasikitisha kwa mtu ambaye anamfahamu Profesa Issa Shivji kwa uzalendo wake na utumishi wake uliotukuka na kujitoa kwake kwa nchi yetu, wale watu walikuwa wanaongea kana kwamba ni maneno yao bali kulikuwa na watu ambao walikuwa nyuma yao.

Damu yangu kama itamwagika basi ikapalilie mapambano ya kulinda rasilimali za nchi yangu Tanzania.

Mtu hawezi kuishi katika nchi ambayo ni Jamhuri na watu wengine wakawa na leseni ya kuondoa uhai wao. Mwenye leseni, ruhusa na mamlaka pekee ya kuondoa uhai wa mtu hapa duniani ni Mwenyezi Mungu pekee.

Kiukweli kuua watu kupo na watu wamefariki, watu wamejeruhiwa na kupata matatizo makubwa. Kufuatia hilo nimeamua kuja mbele ya umma wa Watanzania kuwaambia kwamba mimi Rugemeleza Nshala maisha yangu yako hatarini. Kuna maagizo kutoka ndani kwamba nitakapopatikana niteketezwe, niangamizwe na kuitwa marehemu.

Mkataba huu wa bandari umesainiwa au umepewa kibali kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kibali hiko kinaonekana katika kiambatanisho kimojawapo katika mkataba huo ambacho kina saini ya Rais Dkt. Samia

=============

Wakili wa kujitegemea Dkt.Rugemeleza Nshala amesema amepokea taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya mifumo kuwa anatakiwa kuuwawa kwa kile alichokieleza kuwa ni kutokana na msimamo wake dhidi ya watu waliojitokeza kumshambulia kwa maneno ya kejeli na kuudhi Prof.Issa Shivji baada ya msomi huyo wa sheria kutoa maoni yake dhidi ya sakata la uwekezaji wa Bandari linaloendelea sasa hapa nchini

Akizungumza na Wanahabari kwenye ukumbi wa Mesuma Hotel, Makumbusho Jijini Dar es Salaam, Dkt.Nshala ambaye pia amewahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ameeleza kuwa hivi karibuni kupitia jukwaa la 'club house' alitoa maneno makali ambayo kiuhalisia amedai kuwa ndio msimamo wake dhidi ya watu hao ambao anaamini kuwa walichokizungumza si maneno yao bali wanatumiwa na watu wenye mamlaka nchini kutoa lugha za kashfa na kuudhi dhidi ya mtu mwenye umri mkubwa na anayestahiki heshma kubwa dhidi yao kwenye jamii

Dkt.Nshala aliyefika kwenye Kikao hicho akiwa amebeba Vitabu viwili alivyoeleza kuwa anavyoviamini zaidi (Biblia na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) amesema anawaeleza wenye mamlaka walio nyuma ya mpango huo kuwa yuko tayari kufa kwaajili ya nchi yake

Ikumbukwe kuwa kupitia jukwaa hilo ambalo lilijadili mjadala wa kina kuhusiana na uwekezaji wa Kampuni ya DP World ya Dubai kwenye Bandari, Dkt.Nshala alitoa kauli zolizoonekana kuwashambulia zaidi viongozi waandamizi serikalini akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa nk


---
Ndugu Watanzania!
Dkt. Rugemeleza Nshala ametujulisha kuwa maisha yake yako hatarini. Wakili Dkt. Nshala anasema kuwa ametaarifiwa juu ya mipango ya kutaka kumuua (assassination) inayopangwa dhidi yake! Vitisho dhidi ya maisha ya Wakili Dkt. Nshala vinakuja muda mfupi tu baada ya yeye kutoa maoni yake kwa hisia kali akipinga Mkataba wa Bandari kati Serikali ya Tanzania na Ufalme wa Dubai.

Dkt. Rugemeleza Nshala, ambaye alikuwa Rais wa Tanganyika Law Society (TLS) ni wakili na mwanasheria mbobevu anayejua vema mipaka yake kikatiba na kwa nafasi yake anao wajibu wa kutoa ushauri na maoni kwa Watanzania katika masuala ya sheria na katiba ya nchi.

Sisi Askofu tumepata muda wa kuomba na Dkt. Nshala na kumtia moyo kuwa asiogope kwani alitoa maoni yake kama raia anayeipenda nchi yake na hakuvunja sheria ye yote ya nchi. Kwa maoni yetu, watu wanaomtisha Dkt. Nshala au wanaotaka kuondoa uhai wake ni watu waoga ambao wanataka kumchafua Rais Dkt. Samia ili dunia ifikiri ameanza kuwaua wakosoaji wake.

Kwa hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa watu, kikundi, vikundi hata taasisi ambao wanapanga kutoa uhai wa Dkt. Nshala pamoja na wanaharakati wengine wanaotoa maoni yao au hata kuikosoa Serikali kuhusiana na suala la Mkataba wa Bandari waache mara moja. Kama wao wanafikiri kuwa Dkt. Nshala na wenzake wamefanya kosa lo lote kisheria, wawapeleke mahakamani badala ya kuanza kuwatisha.

Kutisha watu na kutaka kuwaondoa au kuwaua watu nje ya mfumo wa kisheria ni uhaini, uuaji, unyama na ujambazi bila kujali mtu anayefanya matendo hayo. Sisi Askofu tunatoa tahadhari hii kama kukinga mapema ili watu hao wajue kuwa wanachokipanga kufanya hakikubariki. Kama Dkt. Nshala na wenzake watadhulika kwa lolote, watu waliowahi kutoa kauli zao kwa lengo la kuwatisha, hao watawajibika. Kukinga ni bora kuliko kutibu! Tumetimiza wajibu wetu!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 6 Julai 2023; 09:39 am.






View attachment 2680028
Umesikika mtumishi wa aliye juu,

Wanarudisha mapanga Yao alani, ingawa macho Yao mekunduuu!!!!
 
Jadili hoja
Hoja SI wote tunajua hatuitaki DP World. Na wanaopinga sana kama wakili msomi hapo wanawekwa kwenye target.
Tunaendelea kukataa aina hii ya ukoloni mamboleo na ujinga wa Serikali kutaka kukandamiza na kuumiza raia wake wanapoexercise their rights kupinga kuuzwa kwa nchi Yao.

Just wanted to know though, kwanini Askofu Mwamakula anajirefer yeye kama "sisi"
 
Nimemsikia sana huyu Wakili Msomi. Naamini kama Rais Samia atasikiliza hii link ya youtube atabadili mawazo yake kuhusu mkataba wa DP WORLD!! Itakuwa ni ni NUKSI kubwa kwake kama raia wa Tanzania atapoteza maisha sababu ya kutetea raslimali za nchi.

Labda kuwe na nguvu nyingine nyuma yake ambayo ni sadist. Naamini hata hao wanaowatisha hawa mawakili wasomi kuwatoa uhai hawajatumwa na Rais Samia bali na makundi masilahi yanayomzunguka Samia.

Samia amka jitoe kwenye hayo makundi ya akina Rostam na JK, wanakutumia tu ili kufanikisha masilahi yako. Usikubali kumwaga damu ya Mtanzania yeyote kama alivyofanya Magufuli!! Ukikaidi na wewe pia hutadumu kwenye kiti hicho kama mtangulizi wako alivyofanya
 
Back
Top Bottom