Dkt. Rugemeleza Nshala: Nimetishiwa maisha baada ya kutoa maoni kuhusu mkataba wa Bandari na DP World

Kwa jinsi ninavyoifahamu nchi hii ya Tz, uwezekano wa jambo hili kuwa kweli ni zaidi ya takribani asilimia 99.9999
 
Rais Mstaafu wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Dkt.Rugemeleza Nshala amesema amepokea taarifa za vitisho ikiwemo kuuawa.

Akizungumza leo Julia 6, 2023 mbele ya waandishi wa habari amesema kuwa amepata taarifa hizo kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika ambavyo akuwa tayari kuviweka adharani.

Amedai kuwa vitisho hivyo vimekuja kufuatia maoni yake aliyoyatoa kuhusu sakata la Bandari ambalo limekuwa gumzo kubwa.

"Nimekuja hapa kama mtanzania na nashikilia Imani yangu, nasema nilichokisema kama Mungu anaona ni uongo kwa kushika biblia hii nianguke chini niondoke duniani. Sisemi Mungu nisaidie Bali nasema kama niliyosema ya uongo naomba uhai wangu Mungu auchukue. Mimi mkristo mkatokiki kwa miaka yangu 57 nineyaona mengi"amesema Dkt. Rugemeleza

Akiwa ameshikiria Biblia pamoja na Katiba mkononi amesema atasimamia anachokiamini kwa imani yake na mapenzi yake kwa Nchi, huku akiwataka wanahusika kutoa vitisho kutubu.

"Naipenda Tanzania, nitaifia nchi yangu damu yangu ikimwagika iendelee kumwagilia rasilimali za nchi yetu na hao watakaofikiria hayo yatawakuta mabaya sana kwao. Nawasihi watuvu wafahanu kwamba siku ya mwisho watajibu sio kwao Bali kwa familia zao na vizazi vyao 440 vya familia zao. Kuanzia Sasa zitateswa na zitateseka kwa dhambi hiyo wanayoifanya. Nayasema haya nikiwa na moyo mweuoe lakini ndugu zangu kama ndio mwisho wangu nasema kwaherini tutaonana paradise" amesema Dkt. Rugemeleza

Ikumbukwe kwenye kauli zake alizozitoa hivi karibuni kuhusu sakata hilo ni pamoja na kukosoa vikali mkataba huo na wahusika waliosaini sambamba na Bunge lililojadili na kupitisha.
 
KATISHIWA KUWAWA KWELI HUYU
 
Aache upumbavu kutafutia kiki za sifa za kihaya wangapi wametoa maoni Yao kuhusu bandari na hawajatishiwa yeye ni nani nchi hii ana nguvu gani ya kuzuia jambo wenye maslai nalo wakitaka kulipitisha
 
Kwa hisia kali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…