Dkt. Rugemeleza Nshala: Nimetishiwa maisha baada ya kutoa maoni kuhusu mkataba wa Bandari na DP World

Yaaani uhuru wote huu wa kutoa maoni bado kuna watu wanatengeneza hadithi? Katoa maoni Jaji Warioba, Profesa Shivji, Profesa Lipumba, BAKWATA, TEC na Mbowe ambaye alitumia maneno baadhi ya kuudhi hakuna alietishwa iweje kwa wakili flan mmoja tu? TLS imezungumza hawakutishwa. Hebu tuache kutaka kuichafua nchi. Uhuru wa maoni ni mkubwa mno. Muhimu tuutumie kwa maendeleo na nidhamu.🙏🙏🙏
 
Awe makini
 
Nafikiri hujui undani wa masuala haya.
 
Anatafuta umarufu kupitia bandari , mbona watu wengi wakiwemo na maprofesor wamesema mengi kuhusi hiyo bandari ila hamna anaetishiwa, wewe ni mzalendo muoga kwanini hutaki kusimamia ulicho sema kama kufa ufe nakuja kulalamika ili iweje
Hata kwa Tundu Lissu wakati ule mlisema hivi hivi. Kumbuka, mwezi uliopita yaani Mwezi Juni, 2023 walijipitishia Sheria yao ya Kutoshitakiwa Mahakamani pale wanapotaka kumuua mtu yoyote yule katika nchi hii, Sheria hiyo ipo na inafanya kazi sasa hivi.
 
Tanzania ni nchi ya waungwana na waoga pia, japo pia upande mwingine wapo mashetani, wabinafsi, wauaji, waporaji na viongozi madikteta na walaghai.

Lakini kwaajili ya hao waungwana, waoga na wenye haki wachache, Mungu huwapigania. Kwaajili yao, hakuna atakayeua au kutaka kuua atakayeishi.

Rais Samia akiwategemea wauaji, naye atakuwa ameisha. Atakayeua kwaajili ya mtawala atakuwa anaharakisha kifo chake na cha mtawala.
 
Karibia tawala zote za Afrika uwepo wake madarakani wanategemea Wauaji.
 
Anatafuta umarufu kupitia bandari , mbona watu wengi wakiwemo na maprofesor wamesema mengi kuhusi hiyo bandari ila hamna anaetishiwa, wewe ni mzalendo muoga kwanini hutaki kusimamia ulicho sema kama kufa ufe nakuja kulalamika ili iweje
stupid!
 
huyo tapeli tu anatafuta umaarufu, auawe mtu km kwa lipi hasa? Acheni utapeli
 
"Kwa hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa watu, kikundi, vikundi hata taasisi ambao"

Why is he referring to himself as "SISI"...?
 
Kwanza kabisa hakuna watanganyika. Wewe ni mtabiri kwamba kuna siku hali yangu itakuwa mbaya na huyo Askofu wa CHADEMA awe mtetezi wangu? Acha utabiri wa kishenzi.
 
Serikali chini ya Mh Samia sidhani Kama ni serikali ya visasi na kuuwa watu..Kwa wingi wa utu,ubinadamu na unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu alionao Kiongozi Mkuu wa nchi naamini hawezi ruhusu Damu Za watu zichafue taswira nzuri ya mema mengi na mazuri aliotenda..

Wanaoongoza Serikali ni watu (Wana dini na maadili ya ubinadamu)..Kukosolewa,Kushauriwa na kusahihishwa si jambo la vita..Kikubwa wakosoaji yapasa kuwa na staha na heshima..Matusi,kejeli,dharau havipaswi kuwa msingi wa hoja..Tutoe maoni,Ushauri na mapendekezo Kwa lugha ya kiungwana..

Mwisho,Uongozi ni jalala..Viongozi msiache kusamehe wananchi wanapokosea..Msamaha ni kitendo kinachompendeza mwenyezi Mungu wakati wote ili mzidi kupata Neema,rehema na fadhili..

Kuna maisha baada ya Uongozi,vyeo,Mamlaka na Tunu mbalimbali..Tuwe wanyenyekevu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…