Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.
Ametoa kauli nzito na yenye kuleta furaha na tabasamu kwa watanzania wazalendo na wapenda Amani ,utulivu na usalama wa Taifa letu. Kwa kuwatoa hofu watanzania juu ya usalama wao siku ya kupiga kura wiki chache zijazo.
Ambapo Rais wetu Mpendwa amesema ya kuwa Watanzania wajitokeze kwa wingi sana kupiga kura na wala wasiwe na hofu wala wasiwasi na wala wasitishe na yeyote yule . Kwa kuwa Vyombo vya ulinzi na usalama vipo imara na vimejiandaa na kujipanga vyema kabisa kuwalinda watanzania.
Kauli hiyo ya Amiri Jeshi Mkuu imewapa furaha na kulipua na kuibua shangwe , nderemo na vifijo mitaani kote kwa wote waliokuwa wakifuatilia matangazo ya moja kwa moja. Watanzania wanasema ya kuwa hawapo tayari kuharibu amani ya Taifa letu na hawapo tayari kutumika na wanasiasa na wanaharakati uchwara walioishiwa hoja na sera za kuwashawishi watanzania.
Watanzania wanasema ya kuwa watajitokeza kwa wingi kabisa kupiga kura uchaguzi ujao na wapo tayari kumpigia kura za ndio Mama yetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.