Dkt. Slaa aachiwa kwa Dhamana kituo cha Polisi Oysterbay

Nilishaeleza tafsiri ya uhaini hivyo sina haja ya kuirudia kwenye mada japo nitaweka dondoo mojawapo inayohusiana na kosa/tuhuma ya uhaini.. Dondoo ni kwamba KOSA LA UHAINI HALINA dhaman...
"What A JOKE" !!!!!
 
Napendekeza Slaa arudishwe remanded.
Shame on you. Najua umeisema hiyo jokingly, lakini kwa uliyosema baada ya kukamatwa kwake, naweza kusema bila kupepesa macho kuwa hicho ndicho ulichomaanisha.
Ulishangilia kukamatwa kwake, sasa yako wapi? Utashangiliaje kukamatwa kwa mtu anayepigania maslahi ya taifa? Ingawa wewe na mimi ni kama watani wa jadi maana ligi yetu imeanzia mbali, lakini kwa hilo uliniudhi sana. Uwe unapima mambo ya kusema!
 
Acha kushangilia tu niliagiza hadi Konyagi mara tu niliposikia Slaa kanyakwa
 
Ila jamani Serikali isijiabishe tena kwa case za hivi. Haya mambo ya kuzimwa watu kutoa maoni yalitakiwa yasahaulike mazima. Wasiachiwe watu wasio na busara kufanya maamuzi ya hovyo hivi; mfano kuamua hawa tuwakamate na kuwapa case fulani. Unatoaje case ya uhaini kiholela hivi kweli?
 
Safari hii naona Kingai amestuka na kuona kesi hii haina maslahi kwa nchi.
 
Ni aibu isiyo kifani
1. Uhaini hauna dhaman, lakini Slaa amepata dhamana

2. Au yale mashtaka ya uchochezi ya mwanzo yaliyobadilishwa na kuwa uhaini, yamerudishwa?

3. Au wamemtoa kuwauwa nguvu wale waliotaka kwenda mahakamani kushinikiza akina Slaa waondolewe polisi na kupelekwa mahakamani?

AIBU TUPU KWA SERIKALI NA AINA HII YA KESI
 
IGP Wambura alitoa tamko lililoleta taharuki kubwa.

DPP anapaswa kuelewa hili
Sasa hivi kila upande inabidi ucheze karata zao vizuri maana watanzania waleo siyo wale wa enzi za zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama.
 
Sasa hivi kila upande inabidi ucheze karata zao vizuri maana watanzania waleo siyo wale wa enzi za zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama.
Ikulu ni mahali patakatifu
Ikulu siyo pango la wanyang'anyi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…