Dkt. Slaa adokeza kuwa amepata habari Deus Soka atauawa leo na kutupwa kwenye msitu

Dkt. Slaa adokeza kuwa amepata habari Deus Soka atauawa leo na kutupwa kwenye msitu

habari hiyo ni kwa mujibu wa Tweeter ukimnukuu Dr. Slaa

TAARIFA!! TAARIFA!! TAARIFA!!
Taarifa niliyoisikia toka kwa Dr. SLAA (amesema akiwa public) ni kwamba amepewa taarifa na watu wema kuwa AMRI imetolewa ya Ndg. SOKA kuuawa usiku wa leo (kabla ya saa 8) kwenye moja ya misitu nje kidogo ya DSM. Amesema, jopo la kutekeleza mkakati

View attachment 3075985

Pia soma:KWELI - Dkt. Slaa asema amepata taarifa kuwa Deusdadit Soka atauawa na kutupwa msituni
Hivi CCM unajisikiaje taarifa mbaya kama hizi katika utawala wa awamu yenu ya sita!?...
 
EEEeeeenHeeEeeeeh!
Kwani ilikulazimu kweli kuweka komenti kama hiyo?
Wewe unaichukulia kuwa kama ni mzaha, au siyo?

"Ampate au amfuatilie" wapi sasa? Yeye ni polisi? Hivi polisi wapo kwa kazi gani hasa, kuteka watu?
Kwa kuwa anatoa chronology ya events hadi za mbele
 
Same trend inajirudia. Maana ilikuwa hivi hivi watu wanatoweka so sijaona tofauti naona ni mwendo ule ule
Ya Magufuli alikuwa anateka mwenyewe na kikundi cha WASIOJULIKANA (Tundu Lissu, Ben Saanane). Ya sasa ni wananchi wenyewe wanatekana
 
Ya Magufuli alikuwa anateka mwenyewe na kikundi cha WASIOJULIKANA (Tundu Lissu, Ben Saanane). Ya sasa ni wananchi wenyewe wanatekana
Kweli nimeamini kila zama na watetezi wake.
Ingelikuwa ni wananchi wanatekana polisi wangeshalifanyia kazi wasingekuwa wanatoa majibu mepesi mepesi same kama kipindi cha magufuli.
Mbinu ni ile ile ni vile aliyepo unamkubali
 
Tukizoea uuaji hasa wa ndugu zetu damu itawalilia wauaji, taifa na vizazi. Hakika Damu na roho ni nzito. Nzito hasa. Wauaji msitekeleze hilo kwa huyo na wengine ili mjiokoe na kuokoa Taifa. Mungu hadhiakiwi.
 
Mama huku unakotupeleka sio kuzuri, kwani amewafanya nini huyo kijana hata watu hawamjui
 
Kweli nimeamini kila zama na watetezi wake.
Ingelikuwa ni wananchi wanatekana polisi wangeshalifanyia kazi wasingekuwa wanatoa majibu mepesi mepesi same kama kipindi cha magufuli.
Mbinu ni ile ile ni vile aliyepo unamkubali
Haya Polisi wakati wa Magufuli walisemaje kutekwa kwa MoDewji?

Au ulisikia uchunguzi gani baada ya Lissu kushambuliwa akitoka Bungeni kwenye nyumba za maafisa wa Serikali?
 
😭😭😭😭😭😭😭😭😭 my Country
 
Haya Polisi wakati wa Magufuli walisemaje kutekwa kwa MoDewji?

Au ulisikia uchunguzi gani baada ya Lissu kushambuliwa akitoka Bungeni kwenye nyumba za maafisa wa Serikali?
Hivi unasoma ninachokiandika?
Nmekwambia kinachofanyika sasa hivi ni kile kile kilichofanyika kipindi cha magufuli ndio maana polisi majibu yao hayaonyeshi kama wanachukua hatua zozote maana bila shaka wanajua kinachoendelea
 
Tofauti sana. Hivi wakati wa Mwendazake Mbowe angepata hata muda wa kupanda kwenye jukwaa na kuongea kuwa kuna watu wanatekwa?

Tatizo la kutekana, kuiba watoto, kuua albino, kuua vikongwe na tatizo lenu Watanzania wenyewe.
 
Hizo za mbele ni zipi tena. Kwamba mtekwa atauliwa? Wewe unaweza kujuwa kuwa hatauawa?
Ndiyo hapo sasa. Kama Dr Slaa anajuwa atauawa ina maana ana details zote. Azifikishe Polisi na atoe hizo locations au watu wanaompa taarifa
 
Ndiyo hapo sasa. Kama Dr Slaa anajuwa atauawa ina maana ana details zote. Azifikishe Polisi na atoe hizo locations au watu wanaompa taarifa
Uko sawa mkuu 'Stuxnet'. Lakini usisahau pia kwamba polisi hao hao huwa hawasubiri kuzuia maandamano, kwa mfano kwa sababu kama hizo hizo za Slaa. Tena usisahau kuwa huyo anaye semwa kuuwawa tayari katekwa, au hata hilo hulijui?
Siku hizi unanishangaza sana ninapo kusoma humu.
 
Back
Top Bottom