Dkt. Slaa Afuatiliwa na watu wasiojulikana kutoka Iringa hadi Dar Es Salaam

Dkt. Slaa Afuatiliwa na watu wasiojulikana kutoka Iringa hadi Dar Es Salaam

Kumbe Dr Slaa yupo paranoid namna hii?

Mbona mambo ya kawaida hayo barabarani?

Juzi juzi nilikuwa naenda Shinyanga nikaongozana na gari ipo nyuma yangu toka Dodoma hadi Shinyanga tumeachana wao wanaelekea Mwanza na tulikuwa tunapitana pitana.
 
Dr Slaa amekuwa mtu wa wasiwasi muda wote sijui kwa nini hivi unagetemea barabara zetu zilivyokuwa na msongamano wa magari si unaweza kusema foleni yote inanifuatilia mimi.

Mkuu Ritz; argument zako hazina tofauti na za muishiwa dhaifu anaye amini foleni za magari jijini Dar es Salaam is an indicator of economic growth; Foleni kutoka Iringa hadi Dar es Salaam ? Like father, like son.
 
Mkuu hawa jamaa wanatafuta attention kwa gharama zote sasa,
Usishangae kesho ukisikia mbunge wa chadema anatoa show ya bolingo kariakoo ili aandikwe magazetini.
Haya mambo ya magari kukufuata au kuongozana nayo katika safari ni jambo la kawaida , wakati mwingine hutokea tu kwani wengine wakiwa kwenye safari ndefu hupenda kuongozana na magari mengine ili wasichoke na pia kuwa na back up kama wakipatwa na lolote barabarani, mimi pia huwa napenda kufuata gari ambalo naliona linaenda safari ndefu kama yangu kama kampani.
Na pia ni kawaida kwa binadamu kuhisi anafuatwa hasa pale anapokuwa mtu maarufu kama Dr.
Mbona mimi nilipotoka kwa Dr kuna magari mawili yalinifuata sana mpaka nikaamua kusimama na kuwapiga mkwara wakasepa? Dr si ana walinzi? kwa nini mlinzi asifyatue moja ya juu ili jamaa wasepe? Unajuje kama hao sio vibaka waliokuwa wanataka kuwapora hela walizochangisha kwenye mikutano?

PENDEKEZO: MODS, wekeni mtihani/ test ya kujiunga jf, otherwise tutaendelea kupokea pumba kama hizi za kina lukosi. Hawana hoja za msingi zaidi ya ushabiki.
 
Mzee anaweweseka kutafta huruma ya watanzania

mimi napata shida na mzee slaa hapa tanzania barabara ipi utapita bila kukutana na magari basi itabid atumie ndege yao au apite njia za mkato.
 
hivi ni mimi pekeyangu ninayehisi kuwa tangu Video ya Lwakatare itolewe, CHADEMA wamekuwa wakihangaika namna ya kuifunika na kuonesha kuwa mbaya ni serikali na vyombo vyake vya dola?? mana tangu kutoka kwa video ile, tuhuma dhidi ya serikali na vyombo vyake vimezidi maradufu, haya, lilipokuja bunge ndo kabisa, wakaweka tuhuma zao hadi kwenye hotuba ambazo zilistahili kulenga kuikosoa serikali katika kushindwa ama kuchelewa kuleta maendeleo ya nchi..badala yake zikaongelea tuhuma dhidi ya usalama, na kupigwa ama kutishiwa kuuwa kwa viongozi wa CDM?? hivi ni mimi pekee ninayeona kuwa hadi leo CDM imeshindwa kutoa neno ama skendo inayoweza fumba macho na ufahamu wa vijana wachache wa kitanzania ambao bado tuna uwezo wa kufikiri na kuamua tofauti na wale vijana waliokuwa brainwashed na kuamini kila neno linalotoka midomoni mwa viongozi wa CDM na kuwa tayari kutetea maneno hayo hata kwa uhai wao bila ya kufahamu ukweli wake??
Dr. W slaa, najua juzi tu CDM imetangaza kuwa wewe ndiye mgombea wa Urais 2015, hivi ukishinda, utahudhuria sherehe yoyote ya kitaifa?? hivi utafuta vyombo vyote vya ulinzi na usalama na kuweka watu wako?? hivi utafanya kazi na nani ambaye bado hujamtukana?? au hao vijana wako wanaovaa makoti makubwa meusi na miwani meusi ndiyo watakuwa wanausalama wako?? kwa akili yako, do u think its that simple?? au nawewe umekuwa brainwashed na wazungu??

Well said mazee,

Naona huu mchezo wao umeosoma vizuri.

Wameona juzi kuna shutuma za mama Zitto wamerudi na hii kutupoteza malengo.
 
Kumbe Dr Slaa yupo paranoid namna hii?

Mbona mambo ya kawaida hayo barabarani?

Juzi juzi nilikuwa naenda Shinyanga nikaongozana na gari ipo nyuma yangu toka Dodoma hadi Shinyanga tumeachana wao wanaelekea Mwanza na tulikuwa tunapitana pitana.

Kumbuka yeye ni kiongozi wa juu wa chama kikuu cha upinzani ambcaho kimekijeruhi chama tawala kuliko wakati mwingine wowote huku usalama wa taifa ukihaha usiku na mchana kushirikiana na chama tawala na serikali (kama ilivyonukuliwa na Steven Wassira ambaye ni waziri ndani ya serikali) kukiangamiza pamaoja na viongozi wake

Dr.Slaa ni mgombea urais mwaka 2010 na ni mwanasiasa tishio kwa chama tawala na viongozi wake (kama ilivyonukuliwa na Samweli Sitta waziri mwandamizi katika serikali hii) katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015
 
Kama walikua wanania mbaya si wagewafanyizia kuliko kuwafata nyuma kama wanasindikiza harusi. Hizi ni siasa za kutafuta huruma.
 
Mkuu si unajua usiposikika ndio unakuwa umekwisha kisiasa ?
Inabidi ufanye lolote lakini sio kama anavyofanya lema ili uonekane upo, hiyo ndio siasa ya chadema

kwa hiyo kwa kulijua hilo, ili usikike ndo huwa unamwaga pumba zako hapa jamvin?? Umekuwa mtu mzima wewe, badilika.
 
WANABODI,

Usalama wa viongozi wa chama kikuu cha upinzani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) upo hatarini.Akiwa njia ni kutokea Iringa, Dr. Slaa amefuatiliwa na Gari aina ya Landcruiser yenye vioo vya giza (Tinted) lenye namba za usajili T963 ABN. Awali waliokua ndani ya gari la Dr. Slaa hawakushtuka sana japo waliona kuna mchezo wa gari hilo kuwapita kwa kasi na kisha kupunguza mwendo ghafla na kisha gari la Dr. Slaa kuwapita tena.Walichukulia kama vile ni mchezo wa kawaida hadi walipofika Morogoro na kushtuka zaidi na kuanza kuchukua tahadhari kwa kunakili namba ya gari hilo

Walipofika kibaha ilibidi watoe taarifa kwa askari wa usalama barabarani.

Dr. Slaa na maofisa wa chama akiwemo afisa habari walishtuka zaidi walipofika njia panda ya Tamko-Bunju ambayo mara nyingi hutumika kunapokua na foleni kubwa ya maghari(Traffic Jam) na kulikuta gari hilo likiwasubiri

Baada ya kufuata barabara kuingia jijini Dar Es Salaam gari hiyo ghafla ikaingia nyuma ya gari aliyokua akitumia Dr. Slaa aina ya Landcruiser yenye namba za usajili namba T834 BJG. Ndipo afisa wake aliyekua ndani ya gari akapanda juu (Roof Top) na kufanikiwa kulipiga picha gari hilo.

Kuona hilo likifanyika gari hilo likapaki pembeni na ghafla likaondoka na kupotea hadi muda huu walipoingia Ubungo.

Sasa katika mazingira haya taifa linaelekea wapi? Kama watu wanafuatiliwa na kufanyiwa vituko mchana kweupe usalama wa Watanzania na hasa wanaharakati na viongozi wa upinzani Tanzania uko wapi? Mambo haya ni bora yafahamike mapema na watanzania wayajue. Hili ni tukio lisilo la kawaida kipindi hiki ambacho umma umekosa imani (loose confidence) na vyombo vya dola vinavyotumika kwa matakwa ya kisiasa.

Kuna matukio kadhaa yametokea miaka na miezi michache iliyopita yanayotoa taswira mbaya juu ya usalama wa raia na baadhi ya viongozi wanaokosoa utawala. Siku za karibuni Viongozi wa CHADEMA wamekua wakiwindwa sana na tayari chama hiki kikuu cha upinzani kilishatoa tuhuma kwa Usalama wa Taifa na baadhi ya viongozi wa juu serikali kuhusika katika mipango haramu ya kukihujumu chama hicho na hata kufikia hatua ya kuwabambikia kesi viongozi wake.

tunashukuru katibu wetu mungu yuko nasi daima
 
tunaomba muweke picha ya gari hapa maana ndio ushahidi na hili gari litafahamika nani miliki harisi wa hii gari sio muda mrefu
 
Labda hao jamaa walikua wanalinda michango yao ya m4c ifike makao makuu, si unajua tena bongo, mambo ya kupaki gari porini na kugawana mshiko.
 
Hawa watu watatu na ID kibao humu wanakera sana. Mods kama kuna uwezekano tafuteni njia ya kukomesha huu mtindo wa ID ishirini kwa mtu mmoja. Hii si afya kwa jf.
 
PENDEKEZO: MODS, wekeni mtihani/ test ya kujiunga jf, otherwise tutaendelea kupokea pumba kama hizi za kina lukosi. Hawana hoja za msingi zaidi ya ushabiki.
Na wakiweka watu aina ya zemarcopolo, chillisosi, chilli, lukosi na wa aina yao tutawakosa hivyo tutashindwa kupata mitazamo na viwango vya ufahamu wa masalia wa ccm. Hivyo hivyo tu twendeni. Kuna siku wataelewa, watakumbuka na kubadilika.
 
WANABODI,

Usalama wa viongozi wa chama kikuu cha upinzani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) upo hatarini.Akiwa njia ni kutokea Iringa, Dr. Slaa amefuatiliwa na Gari aina ya Landcruiser yenye vioo vya giza (Tinted) lenye namba za usajili T963 ABN. Awali waliokua ndani ya gari la Dr. Slaa hawakushtuka sana japo waliona kuna mchezo wa gari hilo kuwapita kwa kasi na kisha kupunguza mwendo ghafla na kisha gari la Dr. Slaa kuwapita tena.Walichukulia kama vile ni mchezo wa kawaida hadi walipofika Morogoro na kushtuka zaidi na kuanza kuchukua tahadhari kwa kunakili namba ya gari hilo

Walipofika kibaha ilibidi watoe taarifa kwa askari wa usalama barabarani.

Dr. Slaa na maofisa wa chama akiwemo afisa habari walishtuka zaidi walipofika njia panda ya Tamko-Bunju ambayo mara nyingi hutumika kunapokua na foleni kubwa ya maghari(Traffic Jam) na kulikuta gari hilo likiwasubiri

Baada ya kufuata barabara kuingia jijini Dar Es Salaam gari hiyo ghafla ikaingia nyuma ya gari aliyokua akitumia Dr. Slaa aina ya Landcruiser yenye namba za usajili namba T834 BJG. Ndipo afisa wake aliyekua ndani ya gari akapanda juu (Roof Top) na kufanikiwa kulipiga picha gari hilo.

Kuona hilo likifanyika gari hilo likapaki pembeni na ghafla likaondoka na kupotea hadi muda huu walipoingia Ubungo.

Sasa katika mazingira haya taifa linaelekea wapi? Kama watu wanafuatiliwa na kufanyiwa vituko mchana kweupe usalama wa Watanzania na hasa wanaharakati na viongozi wa upinzani Tanzania uko wapi? Mambo haya ni bora yafahamike mapema na watanzania wayajue. Hili ni tukio lisilo la kawaida kipindi hiki ambacho umma umekosa imani (loose confidence) na vyombo vya dola vinavyotumika kwa matakwa ya kisiasa.

Kuna matukio kadhaa yametokea miaka na miezi michache iliyopita yanayotoa taswira mbaya juu ya usalama wa raia na baadhi ya viongozi wanaokosoa utawala. Siku za karibuni Viongozi wa CHADEMA wamekua wakiwindwa sana na tayari chama hiki kikuu cha upinzani kilishatoa tuhuma kwa Usalama wa Taifa na baadhi ya viongozi wa juu serikali kuhusika katika mipango haramu ya kukihujumu chama hicho na hata kufikia hatua ya kuwabambikia kesi viongozi wake.
Rais to be labda jamaa wameanza kukulinda mapema kabla hujaingia ikulu?
 
kazi zenu mlizo nazo zinatosha mkiongeza mnajiumiza wenyewe roho wa mungu awambia chadema.
 
daima machweo yanapo fika mambo mengi huibuka machweo ya mzee slaa yaja hivyo lazima ajitahid kujihami mapema.
 
Na wakiweka watu aina ya zemarcopolo, chillisosi, chilli, lukosi na wa aina yao tutawakosa hivyo tutashindwa kupata mitazamo na viwango vya ufahamu wa masalia wa ccm. Hivyo hivyo tu twendeni. Kuna siku wataelewa, watakumbuka na kubadilika.

Inataka moyo sana kukaa na hawa watu jukwaa moja. Uwezo wao ni megabyte but wenyewe wanalazimisha kujifanya wa gigabytes. Anyway, acha tuwabebe hivohivo mkuu.

Na umewapatia kweli kuwataja.

Umemsahau M23 hapo, full pumba. Huwa nawafananisha na ma-MC.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom