Maundumula
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 7,553
- 3,081
Dr Slaa amekuwa mtu wa wasiwasi muda wote sijui kwa nini hivi unagetemea barabara zetu zilivyokuwa na msongamano wa magari si unaweza kusema foleni yote inanifuatilia mimi.
Mkuu hawa jamaa wanatafuta attention kwa gharama zote sasa,
Usishangae kesho ukisikia mbunge wa chadema anatoa show ya bolingo kariakoo ili aandikwe magazetini.
Haya mambo ya magari kukufuata au kuongozana nayo katika safari ni jambo la kawaida , wakati mwingine hutokea tu kwani wengine wakiwa kwenye safari ndefu hupenda kuongozana na magari mengine ili wasichoke na pia kuwa na back up kama wakipatwa na lolote barabarani, mimi pia huwa napenda kufuata gari ambalo naliona linaenda safari ndefu kama yangu kama kampani.
Na pia ni kawaida kwa binadamu kuhisi anafuatwa hasa pale anapokuwa mtu maarufu kama Dr.
Mbona mimi nilipotoka kwa Dr kuna magari mawili yalinifuata sana mpaka nikaamua kusimama na kuwapiga mkwara wakasepa? Dr si ana walinzi? kwa nini mlinzi asifyatue moja ya juu ili jamaa wasepe? Unajuje kama hao sio vibaka waliokuwa wanataka kuwapora hela walizochangisha kwenye mikutano?
Mzee anaweweseka kutafta huruma ya watanzania
hivi ni mimi pekeyangu ninayehisi kuwa tangu Video ya Lwakatare itolewe, CHADEMA wamekuwa wakihangaika namna ya kuifunika na kuonesha kuwa mbaya ni serikali na vyombo vyake vya dola?? mana tangu kutoka kwa video ile, tuhuma dhidi ya serikali na vyombo vyake vimezidi maradufu, haya, lilipokuja bunge ndo kabisa, wakaweka tuhuma zao hadi kwenye hotuba ambazo zilistahili kulenga kuikosoa serikali katika kushindwa ama kuchelewa kuleta maendeleo ya nchi..badala yake zikaongelea tuhuma dhidi ya usalama, na kupigwa ama kutishiwa kuuwa kwa viongozi wa CDM?? hivi ni mimi pekee ninayeona kuwa hadi leo CDM imeshindwa kutoa neno ama skendo inayoweza fumba macho na ufahamu wa vijana wachache wa kitanzania ambao bado tuna uwezo wa kufikiri na kuamua tofauti na wale vijana waliokuwa brainwashed na kuamini kila neno linalotoka midomoni mwa viongozi wa CDM na kuwa tayari kutetea maneno hayo hata kwa uhai wao bila ya kufahamu ukweli wake??
Dr. W slaa, najua juzi tu CDM imetangaza kuwa wewe ndiye mgombea wa Urais 2015, hivi ukishinda, utahudhuria sherehe yoyote ya kitaifa?? hivi utafuta vyombo vyote vya ulinzi na usalama na kuweka watu wako?? hivi utafanya kazi na nani ambaye bado hujamtukana?? au hao vijana wako wanaovaa makoti makubwa meusi na miwani meusi ndiyo watakuwa wanausalama wako?? kwa akili yako, do u think its that simple?? au nawewe umekuwa brainwashed na wazungu??
Kumbe Dr Slaa yupo paranoid namna hii?
Mbona mambo ya kawaida hayo barabarani?
Juzi juzi nilikuwa naenda Shinyanga nikaongozana na gari ipo nyuma yangu toka Dodoma hadi Shinyanga tumeachana wao wanaelekea Mwanza na tulikuwa tunapitana pitana.
Mkuu si unajua usiposikika ndio unakuwa umekwisha kisiasa ?
Inabidi ufanye lolote lakini sio kama anavyofanya lema ili uonekane upo, hiyo ndio siasa ya chadema
WANABODI,
Usalama wa viongozi wa chama kikuu cha upinzani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) upo hatarini.Akiwa njia ni kutokea Iringa, Dr. Slaa amefuatiliwa na Gari aina ya Landcruiser yenye vioo vya giza (Tinted) lenye namba za usajili T963 ABN. Awali waliokua ndani ya gari la Dr. Slaa hawakushtuka sana japo waliona kuna mchezo wa gari hilo kuwapita kwa kasi na kisha kupunguza mwendo ghafla na kisha gari la Dr. Slaa kuwapita tena.Walichukulia kama vile ni mchezo wa kawaida hadi walipofika Morogoro na kushtuka zaidi na kuanza kuchukua tahadhari kwa kunakili namba ya gari hilo
Walipofika kibaha ilibidi watoe taarifa kwa askari wa usalama barabarani.
Dr. Slaa na maofisa wa chama akiwemo afisa habari walishtuka zaidi walipofika njia panda ya Tamko-Bunju ambayo mara nyingi hutumika kunapokua na foleni kubwa ya maghari(Traffic Jam) na kulikuta gari hilo likiwasubiri
Baada ya kufuata barabara kuingia jijini Dar Es Salaam gari hiyo ghafla ikaingia nyuma ya gari aliyokua akitumia Dr. Slaa aina ya Landcruiser yenye namba za usajili namba T834 BJG. Ndipo afisa wake aliyekua ndani ya gari akapanda juu (Roof Top) na kufanikiwa kulipiga picha gari hilo.
Kuona hilo likifanyika gari hilo likapaki pembeni na ghafla likaondoka na kupotea hadi muda huu walipoingia Ubungo.
Sasa katika mazingira haya taifa linaelekea wapi? Kama watu wanafuatiliwa na kufanyiwa vituko mchana kweupe usalama wa Watanzania na hasa wanaharakati na viongozi wa upinzani Tanzania uko wapi? Mambo haya ni bora yafahamike mapema na watanzania wayajue. Hili ni tukio lisilo la kawaida kipindi hiki ambacho umma umekosa imani (loose confidence) na vyombo vya dola vinavyotumika kwa matakwa ya kisiasa.
Kuna matukio kadhaa yametokea miaka na miezi michache iliyopita yanayotoa taswira mbaya juu ya usalama wa raia na baadhi ya viongozi wanaokosoa utawala. Siku za karibuni Viongozi wa CHADEMA wamekua wakiwindwa sana na tayari chama hiki kikuu cha upinzani kilishatoa tuhuma kwa Usalama wa Taifa na baadhi ya viongozi wa juu serikali kuhusika katika mipango haramu ya kukihujumu chama hicho na hata kufikia hatua ya kuwabambikia kesi viongozi wake.
Na wakiweka watu aina ya zemarcopolo, chillisosi, chilli, lukosi na wa aina yao tutawakosa hivyo tutashindwa kupata mitazamo na viwango vya ufahamu wa masalia wa ccm. Hivyo hivyo tu twendeni. Kuna siku wataelewa, watakumbuka na kubadilika.PENDEKEZO: MODS, wekeni mtihani/ test ya kujiunga jf, otherwise tutaendelea kupokea pumba kama hizi za kina lukosi. Hawana hoja za msingi zaidi ya ushabiki.
Hivi ni kweli CCM inaiogopa chadema namna hii?
tunaomba muweke picha ya gari hapa maana ndio ushahidi na hili gari litafahamika nani miliki harisi wa hii gari sio muda mrefu
Rais to be labda jamaa wameanza kukulinda mapema kabla hujaingia ikulu?WANABODI,
Usalama wa viongozi wa chama kikuu cha upinzani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) upo hatarini.Akiwa njia ni kutokea Iringa, Dr. Slaa amefuatiliwa na Gari aina ya Landcruiser yenye vioo vya giza (Tinted) lenye namba za usajili T963 ABN. Awali waliokua ndani ya gari la Dr. Slaa hawakushtuka sana japo waliona kuna mchezo wa gari hilo kuwapita kwa kasi na kisha kupunguza mwendo ghafla na kisha gari la Dr. Slaa kuwapita tena.Walichukulia kama vile ni mchezo wa kawaida hadi walipofika Morogoro na kushtuka zaidi na kuanza kuchukua tahadhari kwa kunakili namba ya gari hilo
Walipofika kibaha ilibidi watoe taarifa kwa askari wa usalama barabarani.
Dr. Slaa na maofisa wa chama akiwemo afisa habari walishtuka zaidi walipofika njia panda ya Tamko-Bunju ambayo mara nyingi hutumika kunapokua na foleni kubwa ya maghari(Traffic Jam) na kulikuta gari hilo likiwasubiri
Baada ya kufuata barabara kuingia jijini Dar Es Salaam gari hiyo ghafla ikaingia nyuma ya gari aliyokua akitumia Dr. Slaa aina ya Landcruiser yenye namba za usajili namba T834 BJG. Ndipo afisa wake aliyekua ndani ya gari akapanda juu (Roof Top) na kufanikiwa kulipiga picha gari hilo.
Kuona hilo likifanyika gari hilo likapaki pembeni na ghafla likaondoka na kupotea hadi muda huu walipoingia Ubungo.
Sasa katika mazingira haya taifa linaelekea wapi? Kama watu wanafuatiliwa na kufanyiwa vituko mchana kweupe usalama wa Watanzania na hasa wanaharakati na viongozi wa upinzani Tanzania uko wapi? Mambo haya ni bora yafahamike mapema na watanzania wayajue. Hili ni tukio lisilo la kawaida kipindi hiki ambacho umma umekosa imani (loose confidence) na vyombo vya dola vinavyotumika kwa matakwa ya kisiasa.
Kuna matukio kadhaa yametokea miaka na miezi michache iliyopita yanayotoa taswira mbaya juu ya usalama wa raia na baadhi ya viongozi wanaokosoa utawala. Siku za karibuni Viongozi wa CHADEMA wamekua wakiwindwa sana na tayari chama hiki kikuu cha upinzani kilishatoa tuhuma kwa Usalama wa Taifa na baadhi ya viongozi wa juu serikali kuhusika katika mipango haramu ya kukihujumu chama hicho na hata kufikia hatua ya kuwabambikia kesi viongozi wake.
Na wakiweka watu aina ya zemarcopolo, chillisosi, chilli, lukosi na wa aina yao tutawakosa hivyo tutashindwa kupata mitazamo na viwango vya ufahamu wa masalia wa ccm. Hivyo hivyo tu twendeni. Kuna siku wataelewa, watakumbuka na kubadilika.