Dkt. Slaa Afuatiliwa na watu wasiojulikana kutoka Iringa hadi Dar Es Salaam

Dkt. Slaa Afuatiliwa na watu wasiojulikana kutoka Iringa hadi Dar Es Salaam

Baba MwanaASha hana habari na vitu visivyo na maslahi kwake,yeye kazi kubwa aliyonayo siku hizi ni kukaba 10% za mikataba ya gesi na ndio maana kila safari za nje hamuachi maziri wa nishati na madini!!
Hizo 10% nadhani zimeshamvimbisha tumbo ,kalewa mpaka kajisahau watu kama akina mulungo nao wanajiita maraisi....
janga la taifa ....
 
WANABODI,

Usalama wa viongozi wa chama kikuu cha upinzani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) upo hatarini.Akiwa njia ni kutokea Iringa, Dr. Slaa amefuatiliwa na Gari aina ya Landcruiser yenye vioo vya giza (Tinted) lenye namba za usajili T963 ABN. Awali waliokua ndani ya gari la Dr. Slaa hawakushtuka sana japo waliona kuna mchezo wa gari hilo kuwapita kwa kasi na kisha kupunguza mwendo ghafla na kisha gari la Dr. Slaa kuwapita tena.Walichukulia kama vile ni mchezo wa kawaida hadi walipofika Morogoro na kushtuka zaidi na kuanza kuchukua tahadhari kwa kunakili namba ya gari hilo


Walipofika kibaha ilibidi watoe taarifa kwa askari wa usalama barabarani.

Dr. Slaa na maofisa wa chama akiwemo afisa habari walishtuka zaidi walipofika njia panda ya Tamko-Bunju ambayo mara nyingi hutumika kunapokua na foleni kubwa ya maghari(Traffic Jam) na kulikuta gari hilo likiwasubiri

Baada ya kufuata barabara kuingia jijini Dar Es Salaam gari hiyo ghafla ikaingia nyuma ya gari aliyokua akitumia Dr. Slaa aina ya Landcruiser yenye namba za usajili namba T834 BJG. Ndipo afisa wake aliyekua ndani ya gari akapanda juu (Roof Top) na kufanikiwa kulipiga picha gari hilo.

Kuona hilo likifanyika gari hilo likapaki pembeni na ghafla likaondoka na kupotea hadi muda huu walipoingia Ubungo.

Sasa katika mazingira haya taifa linaelekea wapi? Kama watu wanafuatiliwa na kufanyiwa vituko mchana kweupe usalama wa Watanzania na hasa wanaharakati na viongozi wa upinzani Tanzania uko wapi? Mambo haya ni bora yafahamike mapema na watanzania wayajue. Hili ni tukio lisilo la kawaida kipindi hiki ambacho umma umekosa imani (loose confidence) na vyombo vya dola vinavyotumika kwa matakwa ya kisiasa.

Kuna matukio kadhaa yametokea miaka na miezi michache iliyopita yanayotoa taswira mbaya juu ya usalama wa raia na baadhi ya viongozi wanaokosoa utawala. Siku za karibuni Viongozi wa CHADEMA wamekua wakiwindwa sana na tayari chama hiki kikuu cha upinzani kilishatoa tuhuma kwa Usalama wa Taifa na baadhi ya viongozi wa juu serikali kuhusika katika mipango haramu ya kukihujumu chama hicho na hata kufikia hatua ya kuwabambikia kesi viongozi wake.

appreciation kamanda. tuko nyuma yako daima.
 
hivi ni mimi pekeyangu ninayehisi kuwa tangu Video ya Lwakatare itolewe, CHADEMA wamekuwa wakihangaika namna ya kuifunika na kuonesha kuwa mbaya ni serikali na vyombo vyake vya dola?? mana tangu kutoka kwa video ile, tuhuma dhidi ya serikali na vyombo vyake vimezidi maradufu, haya, lilipokuja bunge ndo kabisa, wakaweka tuhuma zao hadi kwenye hotuba ambazo zilistahili kulenga kuikosoa serikali katika kushindwa ama kuchelewa kuleta maendeleo ya nchi..badala yake zikaongelea tuhuma dhidi ya usalama, na kupigwa ama kutishiwa kuuwa kwa viongozi wa CDM?? hivi ni mimi pekee ninayeona kuwa hadi leo CDM imeshindwa kutoa neno ama skendo inayoweza fumba macho na ufahamu wa vijana wachache wa kitanzania ambao bado tuna uwezo wa kufikiri na kuamua tofauti na wale vijana waliokuwa brainwashed na kuamini kila neno linalotoka midomoni mwa viongozi wa CDM na kuwa tayari kutetea maneno hayo hata kwa uhai wao bila ya kufahamu ukweli wake??
Dr. W slaa, najua juzi tu CDM imetangaza kuwa wewe ndiye mgombea wa Urais 2015, hivi ukishinda, utahudhuria sherehe yoyote ya kitaifa?? hivi utafuta vyombo vyote vya ulinzi na usalama na kuweka watu wako?? hivi utafanya kazi na nani ambaye bado hujamtukana?? au hao vijana wako wanaovaa makoti makubwa meusi na miwani meusi ndiyo watakuwa wanausalama wako?? kwa akili yako, do u think its that simple?? au nawewe umekuwa brainwashed na wazungu??
Tatizo ni TISS mnapojiingiza kwenye siasa za vyama.Fanyeni kazi kwa uadilifu na hamtapa wasiwasi kama ccm ikiondolewa madarakani.
 
Possibly wewe ni miongoni mwa vijana msiojitambua mlio ajiriwa pale Lumumba kwa ajili ya kupost pumba hapa jamvini; Wewe unacho kiangalia ni content au ni spealing ? Check kwanza details zako, ndo twende sawa;
Join Date : 17th April 2013
Posts : 53
Rep Power : 312
Likes Received3
Likes Given2

hawa jamaa nizaidi ya wafu ni wapuuzi kupindukia...alafu huwa wanatoka familia maskini sana...watoo wa vigogo wa ccm wanafanya kaz BOT na kwingineko...wao wanapewa kazi za kishezi then wanashangilia...yani hawa jamaa ni wapumbav# sijawai ona...
 
maisha wanayo ishi watanzania....ndio kitu pekee kinacho ipeleka serekali ya ccm kaburini...nawashauri ccm wajaribu kupunduza ukali wa maisha wa raia....sio wana tafuta njia mbaya kuwaujumu viongozi wa upinzani...TISS hasa kitengo cha kudl na siasa fanyeni kazi yenu kwa manuufaa ya umma, sio mnafanya kazi kwa maslai ya ccm
 
Taifa hili liwe makini sana.
Kama walishindwa kuidhibiti CHADEMA kabla ya 2005 basi watulie. Sasa hivi CHADEMA hakishikiki ni chama pendwa na viongozi wake wanapendwa sana na watanzania. Siyo siri. Kiongozi kama Dr Slaa hawezi kuwasingizia. Naomba ndugu zangu watanzania, muelewe kwamba kumdhuru Dr Slaa au kiongozi yeyote yule wa kitaifa kutoka CHADEMA ,kwa vyovyote vile utakuwa ni msiba mkubwa na mwanzo wa machafuko makubwa sana. CCM wajue na ninaamini wanalijua hilo. Kuanzia hapo ni lazima vyombo vya dola vitagawanyika, taifa litapasuka kabisa. CCM wasijidanganye huo mpango una hatari kubwa sana. Mungu aepushie mbali.

well said....
 
Anachofanya sasa hivi Dr Slaa na wenzake pamoja na Bavicha ni kutafuta huruma kutoka kwa wananchi kusingizia mambo kuwa wanawindwa na Usalama wa Taifa wauawe.

Madai ya Dr Slaa kuwa walikuwa wanafuatiliwa na gari ambayo wameipiga picha si wawake hiyo picha basi kuliko kuja na porojo.

Madai ya aina hii mbali ya kuwa madai ya uongo, pia yanaonyesha upeo mdogo wa viongozi wa Chadema.

nani asie juwa TISS wanafanya kazi za Nape?..
 
Ni wapi Dr Slaa ametaja neno Usalama wa taifa? Alichosema ni kwamba alikuwa akifuatiliwa. Sasa wewe umekurupuka mithili ya mtu aliyefumaniwa na mke wa mtu! Au wewe ndiye co-ordinator wa tukio hilo nini!!

walio ajiriwa lumumba huwa awafaniwi husahili.....wote ni waganga njaa na wemetoka familia maskini sana
 
CHADEMA mmezidi sasa hadi inatia kinyaa! Mnashindwa hata kutunga uongo ukafanana japo kidogo na ukweli?

Njoo na ID yako verified halafu uone kama wiki ijayo hukupelekwa mahakamani kwa kumchafua anayetumia hilo gari ulilotaja namba zake (Kama sio feki).
Taratibu.....umesema wiki ijayo atapelekwa mahakamani?!

You wish.....ukimaliza, just serukamba yoirself and enjoy your evening.
 
kaka bongo systm ime corrupt kitambo
Quote niliyoijibu ni hiyo hapo chini...
hivi ukishinda, utahudhuria sherehe yoyote ya kitaifa?? hivi utafuta vyombo vyote vya ulinzi na usalama na kuweka watu wako?? hivi utafanya kazi na nani ambaye bado hujamtukana?? au hao vijana wako wanaovaa makoti makubwa meusi na miwani meusi ndiyo watakuwa wanausalama wako?? kwa akili yako, do u think its that simple?? au nawewe umekuwa brainwashed na wazungu??
 
Msikubali kulaghaiwa na Dr. Slaa.

Note kuwa hajataja namba ya gari. Hii ni kujaribu kujiweka mbali na responsibility za huu uzushi.

Hii simulizi ni sawa Dar Express lifike Arusha halafu waseme Scandnavia lilikuwa linatufuata!

Weka picha ya gari hapa tulione.

T963 ABN kama hujaiona.
 
Back
Top Bottom