Dkt. Slaa akamatwa na watu waliojitambulisha kama Polisi

Dkt. Slaa akamatwa na watu waliojitambulisha kama Polisi

Atakamatwa na atatupwa ndani na kazi zitaendelea,usilete mikwala yako ya mbuzi hapa .hakuna anayeogopwa wala anayeweza kushindana na serikali yetu hapa nchini. Sisi ndio wenye nchi na ndio tunasema kuwa kamata tupa ndani huko maana watanzania hatutaki mtu anayechochea machafuko na vurugu nchini
Umesahau kuweka namba yako
 
Huu ni zaidi ya ujinga unaofanywa na awamu hii ya sita

Jibuni hoja mmeshindwa mmeamua kutosha watu

Nchi ya hovyo hii😏
 
Malipo ya kupigania haki za watu weusi ni kifo.

Hutaungwa mkono, uta achwa peke yako ufe.

Waafrika na watanzania sio watu wa kuwapigania ni kuwaacha na shida zao.

Ukikuta mtu mweusi na nyoka wanapigwa muokoe nyoka.
Mbona Nyerere,Nkrumah n.k waliweza kutupigania,na wakafanikiwa,ambapo sasa mnawarudisha wakoloni kwa kasi sana?
 
Wakoloni walileta shanga na suti na kanzu kwa machifu nao wakafungua njia kwa mwarabu akamate wanyamwezi apeleke utumwani. Nilikuwa nawakumbusha historia Tu.
 
Muda mchache uliopita kavamiwa nyumbani kwake, polisi hawajasema wametoka kituo gani na haijajulikana anapelekwa wapi.

---
Kupitia mtandao wa X, Martin Maranja anahabarisha kuwa Dkt. Slaa amekamatwa...

Nimepata taarifa muda huu kwamba Dr. Wilbroad Peter Slaa amekamatwa na watu waliojitambulisha ni jeshi la Polisi muda huu akiwa nyumbani kwake Mbweni, Kawe, Dar es Salaam. Dr. Peter Slaa ni mmoja kati ya wakosoaji wa mkataba wa uuzwaji bandari kwa waarabu wa Dubai, DP WORLD.

View attachment 2716202


Pia Askofu Mwamakula amethibitisha taarifa hivyo kupitia mtandao wa X

BALOZI DKT. SLAA AKAMATWA NA POLISI!

Ndugu Watanzania!
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa Balozi Dkt. Willibrod Slaa amekamtwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwake muda huu.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula


View attachment 2716213
 
Back
Top Bottom