KWELI Dkt. Slaa alitoa kauli ya kuipindua Serikali wakati wa mahojiano

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Salaam

Ndugu zangu, katik pitapita zangu mitandaoni hasahasa kwenye mjadala unaomuhusu Dkt Slaa nimekuwa nikikutana na clip fupi ya Sekunde zipatazo 15 ikimuonesha anatamka kuhusu kupindua Serikali. Kwa namna Clip hiyo ilivyokatwa nashindwa kuelewa muktadha wa kauli hiyo.

Naombeni mtusaidie kutafuta ukweli wa tukio hilo au Interview hiyo kwa kirefu zaidi.

Clip niliyokutana nayo na inayosambaa ni hii hapa chini:

1692205023774.png

Picha: Dkt Slaa

Video 1: Kipande (clip) inachosambaa kwenye mitandao ya kijamii

Video 2: Sehemu ya kipande cha Dkt. Slaa kwa urefu zaidi
Chanzo: Star TV
 
Tunachokijua
Tangu kukamatwa kwa Dkt. Slaa mnamo Agosti 13, 2023 kumeibuka mijadala mbalimbali kumhusu. Wakili wake Adv. Dickson Matata katika ukurasa wake wa X (zamani Twitter) alitoa taarifa zinazodai kuwa Dkt. Slaa amehojiwa kuhusu kosa la uchochezi kinyume na Sheria na baada ya muda tuhuma zikabadilika na kuwa uhaini.

Tangu kutolewa taarifa hiyo ya Wakili mijadala imeibuka katika mitando mbalimbali ya kijamii kuhoji sababu ya Dkt. Slaa kuhusishwa na kosa la uhaini. Baadhi ya watu katika mitandao wamekuwa wakisambaza video yenye Sekunde 15 ikimuonesha Dkt. Slaa akitamka kuhusu kupindua Serikali.

Je, ni kweli Dkt. Slaa alitoa kauli ya kuipindua Serikali?
JamiiForums imefanya uchunguzi na kubaini kuwa kauli hiyo ya Dkt. Slaa aliitamka katika mahojiano yake aliyofanyiwa kwenye kipindi cha Medani za Siasa kinaendeshwa na Star TV. Mahojiano hayo yaliwekwa katika ukurasa wa YouTube wa Star TV Habari mnamo Julai 1, 2023 yakiwa na urefu wa 01:30:53 (Saa moja dakika thelathini na sekunde hamsini na tatu).

JamiiForums baada ya kutazama mahojiano yote ambayo kwa kiasi kikubwa Dkt. Slaa aliongelea Mkataba wa Bandari na harakati zake za kisiasa. Imebaini kuwa kauli ya kuhusu kuipindua Serikali aliitoa kuanzia 1:06: 40. Sehemu ya mahojiano hayo Dkt. Slaa anasema:
Tunaishinikiza Serikali mpaka iondoke kwa sababu Serikali ibara ya nane ya katiba inasemaje?
Ni Serikali ya ajabu ambayo imeingia kwenye mkataba bila kushirikisha watu wake, tatizo lipo kwenye katiba yetu na ndiyo maana tunataka katiba mpya sasa, sio jana Wala si kesho Ili upuuzi usitokee tena.
Upuuzi imetokea, tazama Marekani Rais anapelekwa mahakamani. Donald Trump sasa hivi yupo mahakamani kwa kesi ya ngapi? Juzi amepelekwa na kushitakiwa kwa makosa 37 kwenye kesi Moja.
Sisi tumekinga Marais wa kwetu hii ni nchi ya aina gani? Tunaishi Dunia ipi? Afadhali Dunia ya kina Mangungo waliodanganywa kwa kupewa shanga na kioo Cha kujitazamia Hadi inauzwa ni kwa sababu ameletewa kitu Cha kujitazama, ndiyo kitu muhimu sana kwake.
Hatuko huko tena, tutapiga kelele, tutaishinikiza Serikali na Matokeo yake kama hawataona leo wataona karibuni sana.
Mwandishi: Hoja ya msingi hapa kwa sababu mmeshafikia kwenye hii hatua, Watanzania hawana Cha kufanya.
Dkt. Slaa: Sio hawana Cha kufanya Serikali inaweza, kwani Serikali zinapopinduliwaga sasa kwanini zinapinduliwa? Huwezi kuniambia hamna Cha kufanya.
Mwandishi: Tufanye nini sasa hapo?
Dkt. Slaa: The extreme ni kuipindia Serikali. Serikali ibara ya nane inasema mamlaka yake yote yanatoka kwa Wananchi, Serikali inayofanya vitu bila kujali mamlaka ya Wananchi na inafanya vitu kwa kejeli inatuona Sisi watoto wadogo.
Inasema kwamba itarekebisha wakati tunajua hakuna njia. Jana nilimsikiliza Shivji. Shivji katika nchi hii ni kama Dictionary ya Sheria. Amesema njia pekee ni Bunge likae chini na wajitambue kwamba walikosea, wajishushe, wabatilishe kwasababu ndiyo njia pekee iliyobaki kufuta huo mkataba mbaya na huyo ndiyo Mwalimu ambaye Dunia inamtambua kama mtaalaum wa sheria. Halafu Serikali inakuja inapiga piga machenga.

Hivyo, kutokana na chanzo hiki kilichopitiwa na JamiiForums, hoja inayodai kuwa Dkt. Slaa alitamka kuhusu kuipindua Serikali ni ya kweli.
Dkt. Slaa: The extreme ni kuipindia Serikali. Serikali ibara ya nane inasema mamlaka yake yote yanatoka kwa Wananchi, Serikali inayofanya vitu bila kujali mamlaka ya Wananchi na inafanya vitu kwa kejeli inatuona Sisi watoto wadogo.

Nilivyomuelewa Dkt Slaa hapa ni kuwa wananchi wana options tofauti hili na the "extreme" ni kuipindua serikali. Na kitu "extreme" hakipendezi na ni option ya mwisho ya wananchi pale wanapoona kuwa mamlaka yao hayathaminiwi.

Amandla...
Ni sahihi, ila changamoto tuliyonayo kama Taifa ni kukosa Wananchi Makini inapotokea mambo yahusuyo mustakabali wa maisha yao.

Kuna watu nimehuzunika kuwasikia wanabeza eti hata bandari ikiuzwa wao haiwahusu.

Unagundua Nyerere alipata shida sana kuwaongoza watu wenye mentality ya namna hii
 
Salaam

Ndugu zangu, katik pitapita zangu mitandaoni hasahasa kwenye mjadala unaomuhusu Dkt Slaa nimekuwa nikikutana na clip fupi ya Sekunde zipatazo 15 ikimuonesha anatamka kuhusu kupindua Serikali. Kwa namna Clip hiyo ilivyokatwa nashindwa kuelewa muktadha wa kauli hiyo.

Naombeni mtusaidie kutafuta ukweli wa tukio hilo au Interview hiyo kwa kirefu zaidi.

Clip niliyokutana nayo na inayosambaa ni hii hapa chini:

View attachment 2718624
Video 1: Kipande (clip) inachosambaa kwenye mitandao ya kijamii

View attachment 2718676
Video 2: Sehemu ya kipande cha Dkt. Slaa kwa urefu zaidi
Chanzo: Star TV
Sawa ngoja tuone zama mpya hii
 
Wahenga walisema, uwongo hutumia lifti kumfikia mlengwo na ukweli hutumia ngazi. Hii ina maana kuwa, uwongo hufika haraka sana kwa walengwa na ukweli huchelewa lakini hufika kwa walengwa.

Kuna kipande cha audio kinatembea kwenye mitandao ambacho kimehaririwa ikisikika sauti ya Dkt. Slaa na pia sauti za watu wengine “wakipanga kinachoitwa uhaini”.

Ukikichunguza kipande hicho cha audio utagundua kuwa kimetengenezwa kwa nia ya kupotosha kwa sababu sauti za watu mbalimbali zimewekwa pamoja ili kutengeneza ujumbe wa kupotosha jamii.

Sauti inayosikika ya Dkt. Slaa imetolewa kwenye mahojiano ambayo alifanya na mtangazaji StarTV anayeitwa Odemba katika kipindi kinachoitwa Medani za Kisiasa zaidi ya mwezi mmoja uliopita na kurushwa hewani.

Fikiria mahojiano yenye maneno ya “uhaini” yafanyike zaidi ya mwezi mmoja uliopita halafu yarushwe hewani nchini zaidi ya mwezi mmoja uliopita, eti ndio akamatwe juzi! Kwa nini chombo cha habari kilichorusha haya mahojiano hakijachukuliwa hatua kama kweli kuna maneno ya “uhaini” katika mahojiano?

Kama ukitaka kuona na kusikia mahojiano yote vizuri alichokisema Dkt. Slaa au kipande cha maneno yaliyowekwa kwenye audio inayozunguka kiko katika muda wa saa 1:01 ya maongezi katika video.

Video ya mahojiano hii hapa;

View: https://www.youtube.com/live/wKbNi6Rr66o?feature=share

Nilileta thread hapa ambayo nilisema kwa sasa utawala wa Rais Samia umekosa uungwaji mkono kwa wananchi wengi nchini hasa wa kipato cha chini na umeamua kwa sasa kutumia “kete” ya udini katika kusaka waungaji mkono katika misingi ya imani ya kidini.

Nilisema sakata la DP World limekuwa ni msumari wa mwisho katika kukataliwa na jamii ya watanzania wengi baada ya tozo mbalimbali ukiachilia baadhi ya wale wanavaa nguo za rangi ya bendera ya CCM!

Thread yangu hii hapa;
Kwa Rais huyu, CCM wana hali mbaya sana!

Rais anachofanya kwa sasa ni kuanza kutumia nguvu za dola kuwanyamazisha wale wanauchambua na kuuhoji utawala wake hasa mkataba wa DP World huku wakiwaelimisha wananchi kuhusu madhara ya mkataba huo.

Nilisema, Ilinichukua miezi mitano kufahamu kuwa Rais Samia hana maisha marefu ya kisiasa kwa sababu hana karama, kipaji na ujuzi wa uongozi.
 
Fikiria mahojiano yenye maneno ya “uhaini” yafanyike zaidi ya mwezi mmoja uliopita halafu yarushwe hewani nchini zaidi ya mwezi mmoja uliopita, eti ndio akamatwe juzi!
Ndio maana ya upelelezi
 
Wahenga walisema, uwongo hutumia lifti kumfikia mlengwo na ukweli hutumia ngazi. Hii ina maana kuwa, uwongo hufika haraka sana kwa walengwa na ukweli huchelewa lakini hufika kwa walengwa.

Kuna kipande cha audio kinatembea kwenye mitandao ambacho kimehaririwa ikisikika sauti ya Dkt. Slaa na pia sauti za watu wengine “wakipanga kinachoitwa uhaini”.

Ukikichunguza kipande hicho cha audio utagundua kuwa kimetengenezwa kwa nia ya kupotosha kwa sababu sauti za watu mbalimbali zimewekwa pamoja ili kutengeneza ujumbe wa kupotosha jamii.

Sauti inayosikika ya Dkt. Slaa imetolewa kwenye mahojiano ambayo alifanya na mtangazaji StarTV anayeitwa Odemba katika kipindi kinachoitwa Medani za Kisiasa zaidi ya mwezi mmoja uliopita na kurushwa hewani.

Kama ukitaka kuona na kusikia mahojiano yote vizuri alichokisema Dkt. Slaa au kipande cha maneno yaliyowekwa kwenye audio inayozunguka kiko katika muda wa saa 1:01 ya maongezi katika video.

Video ya mahojiano hii hapa;

View: https://www.youtube.com/live/wKbNi6Rr66o?feature=share

Nilileta thread hapa ambayo nilisema kwa sasa utawala wa Rais Samia umekosa uungwaji mkono kwa wananchi wengi nchini hasa wa kipato cha chini na umeamua kwa sasa kutumia “kete” ya udini katika kusaka waungaji mkono katika misingi ya imani ya kidini.

Nilisema sakata la DP World limekuwa ni msumari wa mwisho katika kukataliwa na jamii ya watanzania wengi baada ya tozo mbalimbali ukiachilia baadhi ya wale wanavaa nguo za rangi ya bendera ya CCM!

Thread yangu hii hapa;
Kwa Rais huyu, CCM wana hali mbaya sana!

Rais anachofanya kwa sasa ni kuanza kutumia nguvu za dola kuwanyamazisha wale wanauchambua na kuuhoji utawala wake hasa mkataba wa DP World huku wakiwaelimisha wananchi kuhusu madhara ya mkataba huo.

Nilisema, Ilinichukua miezi mitano kufahamu kuwa Rais Samia hana maisha marefu ya kisiasa kwa sababu hana karama, kipaji na ujuzi wa uongozi.
 
JF tayari imeshaverifie officially ni Dr Slaa aliongea hayo Maneno.

Kwahiyo ondoa hii takataka yako haina mashiko.
 
Wahenga walisema, uwongo hutumia lifti kumfikia mlengwo na ukweli hutumia ngazi. Hii ina maana kuwa, uwongo hufika haraka sana kwa walengwa na ukweli huchelewa lakini hufika kwa walengwa.

Kuna kipande cha audio kinatembea kwenye mitandao ambacho kimehaririwa ikisikika sauti ya Dkt. Slaa na pia sauti za watu wengine “wakipanga kinachoitwa uhaini”.

Ukikichunguza kipande hicho cha audio utagundua kuwa kimetengenezwa kwa nia ya kupotosha kwa sababu sauti za watu mbalimbali zimewekwa pamoja ili kutengeneza ujumbe wa kupotosha jamii.

Sauti inayosikika ya Dkt. Slaa imetolewa kwenye mahojiano ambayo alifanya na mtangazaji StarTV anayeitwa Odemba katika kipindi kinachoitwa Medani za Kisiasa zaidi ya mwezi mmoja uliopita na kurushwa hewani.

Fikiria mahojiano yenye maneno ya “uhaini” yafanyike zaidi ya mwezi mmoja uliopita halafu yarushwe hewani nchini zaidi ya mwezi mmoja uliopita, eti ndio akamatwe juzi! Kwa nini chombo cha habari kilichorusha haya mahojiano hakijachukuliwa hatua kama kweli kuna maneno ya “uhaini” katika mahojiano?

Kama ukitaka kuona na kusikia mahojiano yote vizuri alichokisema Dkt. Slaa au kipande cha maneno yaliyowekwa kwenye audio inayozunguka kiko katika muda wa saa 1:01 ya maongezi katika video.

Video ya mahojiano hii hapa;

View: https://www.youtube.com/live/wKbNi6Rr66o?feature=share

Nilileta thread hapa ambayo nilisema kwa sasa utawala wa Rais Samia umekosa uungwaji mkono kwa wananchi wengi nchini hasa wa kipato cha chini na umeamua kwa sasa kutumia “kete” ya udini katika kusaka waungaji mkono katika misingi ya imani ya kidini.

Nilisema sakata la DP World limekuwa ni msumari wa mwisho katika kukataliwa na jamii ya watanzania wengi baada ya tozo mbalimbali ukiachilia baadhi ya wale wanavaa nguo za rangi ya bendera ya CCM!

Thread yangu hii hapa;
Kwa Rais huyu, CCM wana hali mbaya sana!

Rais anachofanya kwa sasa ni kuanza kutumia nguvu za dola kuwanyamazisha wale wanauchambua na kuuhoji utawala wake hasa mkataba wa DP World huku wakiwaelimisha wananchi kuhusu madhara ya mkataba huo.

Nilisema, Ilinichukua miezi mitano kufahamu kuwa Rais Samia hana maisha marefu ya kisiasa kwa sababu hana karama, kipaji na ujuzi wa uongozi.

Kimbilia mahakamani na huu "utetezi" wako.🤣
 
Ni sahihi, ila changamoto tuliyonayo kama Taifa ni kukosa Wananchi Makini inapotokea mambo yahusuyo mustakabali wa maisha yao.

Kuna watu nimehuzunika kuwasikia wanabeza eti hata bandari ikiuzwa wao haiwahusu.

Unagundua Nyerere alipata shida sana kuwaongoza watu wenye mentality ya namna hii
Hayo ya kukuhusu au kutokuhusu mbona ni cha mtoto kubwa na UJINGA NI KUSEMA AU KUDHANI BANDARI INAWEZA KUUZWA
 
Salaam

Ndugu zangu, katik pitapita zangu mitandaoni hasahasa kwenye mjadala unaomuhusu Dkt Slaa nimekuwa nikikutana na clip fupi ya Sekunde zipatazo 15 ikimuonesha anatamka kuhusu kupindua Serikali. Kwa namna Clip hiyo ilivyokatwa nashindwa kuelewa muktadha wa kauli hiyo.

Naombeni mtusaidie kutafuta ukweli wa tukio hilo au Interview hiyo kwa kirefu zaidi.

Clip niliyokutana nayo na inayosambaa ni hii hapa chini:

View attachment 2718624
Video 1: Kipande (clip) inachosambaa kwenye mitandao ya kijamii

View attachment 2718676
Video 2: Sehemu ya kipande cha Dkt. Slaa kwa urefu zaidi
Chanzo: Star TV
Mahojiano yalifanyika tarehe,, mwezi na mwaka gani?

Wakati anahojiwa suala la bandari na DPW lilikuwa tayari linazingumzwa kwa uwazi na wananchi?

Mjadala ulikuwa unahusu nini na mwandishi huyu anayejiita chief 'O' was StarTv?

Clip nzima kuanza mwanzo hadi mwisho dakika 45 iko wapi ili kujua 'full contents' ya 'interview' husika?
 
Ccm wao ni kuuza rasilimali tu kwa matumbo yao
fuatilieni TBC mpate habari za uhakika wacheni kuokotaokota porojo za watu wanajifungia kwenye kachumba na kijirekodi wakijiropokea tuh kama kavimbiwa mbaazi.ccm inachapa kazi kwa mchakamchaka wa hali yajuu ndio mana wanachi wanawapuza sana chadema kwani wakitizama wanayoongea na uhalisia haviendani hata robo
 
Yaani mpaka tuzione tbc ya ccm? Kwani hatuna macho?
 
hii ndio shida mliyo nayo mkielezwa wagumu kuelewa..kwa maelezo yako huna haja ya kitizama habari kwani unamini utazishuhudia njiani

hovyo kabisa
 
Aisee !!!

Hivi unajua naweza kuleta clip ya Samia anayosema hata upinzani wakipiga kura vipi ni CCM ndio wataunda Serikali !!!

Kwa maneno hayo naweza kutafsiri maneno hayo ni kusema kwamba wataiba Kura...

Tuachane na kushikana na kutumia semantics tujenge nchi; tumetoka kwenye mjadala wa uzuri au ubaya wa Mkataba tumeingia kwenye uchochezi na Ugaidi (all at Taxpayers money expense)
 
Back
Top Bottom