Salaam
Ndugu zangu, katik pitapita zangu mitandaoni hasahasa kwenye mjadala unaomuhusu Dkt Slaa nimekuwa nikikutana na clip fupi ya Sekunde zipatazo 15 ikimuonesha anatamka kuhusu kupindua Serikali. Kwa namna Clip hiyo ilivyokatwa nashindwa kuelewa muktadha wa kauli hiyo.
Naombeni mtusaidie kutafuta ukweli wa tukio hilo au Interview hiyo kwa kirefu zaidi.
Clip niliyokutana nayo na inayosambaa ni hii hapa chini:
Picha: Dkt Slaa
Video 1: Kipande (clip) inachosambaa kwenye mitandao ya kijamii
Video 2: Sehemu ya kipande cha Dkt. Slaa kwa urefu zaidi
Chanzo: Star TV
Ndugu zangu, katik pitapita zangu mitandaoni hasahasa kwenye mjadala unaomuhusu Dkt Slaa nimekuwa nikikutana na clip fupi ya Sekunde zipatazo 15 ikimuonesha anatamka kuhusu kupindua Serikali. Kwa namna Clip hiyo ilivyokatwa nashindwa kuelewa muktadha wa kauli hiyo.
Naombeni mtusaidie kutafuta ukweli wa tukio hilo au Interview hiyo kwa kirefu zaidi.
Clip niliyokutana nayo na inayosambaa ni hii hapa chini:
Picha: Dkt Slaa
Video 1: Kipande (clip) inachosambaa kwenye mitandao ya kijamii
Video 2: Sehemu ya kipande cha Dkt. Slaa kwa urefu zaidi
Chanzo: Star TV
- Tunachokijua
- Tangu kukamatwa kwa Dkt. Slaa mnamo Agosti 13, 2023 kumeibuka mijadala mbalimbali kumhusu. Wakili wake Adv. Dickson Matata katika ukurasa wake wa X (zamani Twitter) alitoa taarifa zinazodai kuwa Dkt. Slaa amehojiwa kuhusu kosa la uchochezi kinyume na Sheria na baada ya muda tuhuma zikabadilika na kuwa uhaini.
Tangu kutolewa taarifa hiyo ya Wakili mijadala imeibuka katika mitando mbalimbali ya kijamii kuhoji sababu ya Dkt. Slaa kuhusishwa na kosa la uhaini. Baadhi ya watu katika mitandao wamekuwa wakisambaza video yenye Sekunde 15 ikimuonesha Dkt. Slaa akitamka kuhusu kupindua Serikali.
Je, ni kweli Dkt. Slaa alitoa kauli ya kuipindua Serikali?
JamiiForums imefanya uchunguzi na kubaini kuwa kauli hiyo ya Dkt. Slaa aliitamka katika mahojiano yake aliyofanyiwa kwenye kipindi cha Medani za Siasa kinaendeshwa na Star TV. Mahojiano hayo yaliwekwa katika ukurasa wa YouTube wa Star TV Habari mnamo Julai 1, 2023 yakiwa na urefu wa 01:30:53 (Saa moja dakika thelathini na sekunde hamsini na tatu).
JamiiForums baada ya kutazama mahojiano yote ambayo kwa kiasi kikubwa Dkt. Slaa aliongelea Mkataba wa Bandari na harakati zake za kisiasa. Imebaini kuwa kauli ya kuhusu kuipindua Serikali aliitoa kuanzia 1:06: 40. Sehemu ya mahojiano hayo Dkt. Slaa anasema:
Tunaishinikiza Serikali mpaka iondoke kwa sababu Serikali ibara ya nane ya katiba inasemaje? Ni Serikali ya ajabu ambayo imeingia kwenye mkataba bila kushirikisha watu wake, tatizo lipo kwenye katiba yetu na ndiyo maana tunataka katiba mpya sasa, sio jana Wala si kesho Ili upuuzi usitokee tena. Upuuzi imetokea, tazama Marekani Rais anapelekwa mahakamani. Donald Trump sasa hivi yupo mahakamani kwa kesi ya ngapi? Juzi amepelekwa na kushitakiwa kwa makosa 37 kwenye kesi Moja. Sisi tumekinga Marais wa kwetu hii ni nchi ya aina gani? Tunaishi Dunia ipi? Afadhali Dunia ya kina Mangungo waliodanganywa kwa kupewa shanga na kioo Cha kujitazamia Hadi inauzwa ni kwa sababu ameletewa kitu Cha kujitazama, ndiyo kitu muhimu sana kwake.Hatuko huko tena, tutapiga kelele, tutaishinikiza Serikali na Matokeo yake kama hawataona leo wataona karibuni sana. Mwandishi: Hoja ya msingi hapa kwa sababu mmeshafikia kwenye hii hatua, Watanzania hawana Cha kufanya. Dkt. Slaa: Sio hawana Cha kufanya Serikali inaweza, kwani Serikali zinapopinduliwaga sasa kwanini zinapinduliwa? Huwezi kuniambia hamna Cha kufanya.Mwandishi: Tufanye nini sasa hapo? Dkt. Slaa: The extreme ni kuipindia Serikali. Serikali ibara ya nane inasema mamlaka yake yote yanatoka kwa Wananchi, Serikali inayofanya vitu bila kujali mamlaka ya Wananchi na inafanya vitu kwa kejeli inatuona Sisi watoto wadogo. Inasema kwamba itarekebisha wakati tunajua hakuna njia. Jana nilimsikiliza Shivji. Shivji katika nchi hii ni kama Dictionary ya Sheria. Amesema njia pekee ni Bunge likae chini na wajitambue kwamba walikosea, wajishushe, wabatilishe kwasababu ndiyo njia pekee iliyobaki kufuta huo mkataba mbaya na huyo ndiyo Mwalimu ambaye Dunia inamtambua kama mtaalaum wa sheria. Halafu Serikali inakuja inapiga piga machenga.
Hivyo, kutokana na chanzo hiki kilichopitiwa na JamiiForums, hoja inayodai kuwa Dkt. Slaa alitamka kuhusu kuipindua Serikali ni ya kweli.