Kiby
JF-Expert Member
- Nov 16, 2009
- 6,921
- 4,683
Tutahudhuria maana kwa hakika hatuna urithi mwingine Mungu aliotupa zaid ya hivi tulivyo navyo ikiwepo bandari.WITO WA KUHUDHURIA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA: BANDARI ZETU! URITHI WETU!
Kwa viongozi wa dini zote na Madhehebu yote nchini Tanzania!
Sisi Watanzania tulioko ndani na nje tumeamua kulinda rasilimali za nchi tulizopewa na Mungu sisi na vizazi vyetu kama ilivyoanishwa kwenye Ibara ya 27 (1) na (2) ya Katiba yetu. Tunaomba waumini wote wafike kwa wingi na kuwaalika wengine kufika Mkutano Mkubwa wa Hadhara kupata elimu kuhusu Mkataba wa Bandari wa DP World siku ya Jumamosi 22 Julai 2023.
Viongozi wa dini, wanasiasa, mawakili, vyama vya kiraia na wanaharakati mbalimbali nchini watashiriki kwenye mkutano huo.
Taarifa itatolewa kuhusu mahali lakini muda ni kuanzia Saa 4 asubuhi mpaka saa 12 Jioni.
Imetolewa na
Dr. Wilbroad Peter Slaa, kwa niaba ya Sauti ya Watanzania (SYW).
Dar es Salaam, 14 Julai 2023
Mdhamini wetu mkoloni alitushikilia huu urithi hadi alipoona kuwa tumepevuka kiakili akaturudishia japo alitamani aendelee kuwa navyo.
Sasa tunatambua kuwa mdhamini hana nguvu tena mwana wa urithi anapo- mature unless otherwise mwana awe zezeta.