Dkt. Slaa: Bunge la bajeti ni takwa la kikatiba haliwezi kuahirishwa, Chadema wanatafuta huruma ya kisiasa lakini wamechelewa

Dkt. Slaa: Bunge la bajeti ni takwa la kikatiba haliwezi kuahirishwa, Chadema wanatafuta huruma ya kisiasa lakini wamechelewa

Balozi wetu huko Sweden amesema bunge la bajeti ni takwa la kikatiba hivyo haliwezi kuahirishwa kwa sababu zozote.
Katiba inatamka wazi kuwa bunge la kbajeti litakaa kwa siku zisizozidi 45 ukiondoa week end na sikukuu hivyo hakuna namna unaweza kuahirisha na wabunge wanalijua hilo.

Pili Dr Slaa amesema haiwezekani kusimamisha miradi mikubwa kwa kisiñgizio cha Corona maana hata Sweden hawafanyi hivyo.

Balozi amewaponda wanaosema " maisha kwanza uchumi baadae " kwamba hawana hoja kwa madai uchumi ndio unabeba maisha.

Amewataka Chadema kutoitumia Corona kama sababu ya wao kushindwa kutimiza majukumu yao ya kikatiba.

Chanzo: Channel ten!
Ukishiba sana mpaka ukaanza kujamba Jamba hovyo hujijui kama unajivunjia heshima mpaka njaa itakapokukuta tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dr. Slaa Chadema hakuna pahali nimesikia wanasema bunge la budget lifutwe Kuna Tofauti kufuta na kusimamisha bunge.

Chadema wanataka wabunge wapimwa je wamepimwa? Chadema wanataka takwimu halisi wanaoambukizwa na kufa je zimetolewa?

Chadema nanataka wa nchi madactari wapewe vifaa je wamepewa?

Tumia muda wako kumshauri jiwa asiendelee kujificha chato.
Ina maana hata mtoa mada hujamuelewa? Nini maana ya kuahirishwa? Au ndio kupinga kupinga kupinga tu.
 
Mkuu Yohane Mbatizaji, kwanza asante kwa taarifa hii, ila Bunge hili sio Bunge la Katiba ni Bunge la Bajeti!.

Pili Dr. Slaa hayuko right, hii Corona ni janga kama janga lingine lolote, kisheria ni tukio linaloitwa force majeure, hivyo shughuli zozote zinaweza kusimama hadi mikataba kusitishwa, hali ikiwa mbaya sana hata Bunge linasimama!.

P
Heshima sana mkuu P.
Kwa stage ya corona tuliyonayo sasa, na hasa kwa shughuli za bunge na tahadhari zote zilizochukuliwa, ni sahihi kuita "janga" kubwa hivyo ku warrant kusimamisha bunge?

Na Kama bunge ni sahihi kusimamisha, then by the same token tusimamishe shughuli za polisi, jeshi, mahakama, usafiri wote, masoko, na wengine wanasema hata hospitali sababu wa kwenye fani hii wana haki ya kujikinga na ugonjwa wenyewe hauna tiba, labda wachache wao wawaelekeze wananchi namna ya kujihudumia huko majumbani.
 
Kwa hiyo hadi China iliyihairisha binge kwa sababu ya ugonjwa,kwao sio takwa la kikatiba??.
Huyo slaa anaweza akawa amezeeka na akili yake inashindwa kufanya kazi vizuri lakini wewe uliyechukua hii habari na kuiweka humu na ukaona unafaa kusomwa na wana JF ndio una matatizo zaidi.
Dah!

Unataka kusema China na Tanzania katiba zao zinafanana?
 
Back
Top Bottom