Pre GE2025 Dkt. Slaa: CHADEMA imeshindwa Kuwashawishi Watanzania Wakiamini

Pre GE2025 Dkt. Slaa: CHADEMA imeshindwa Kuwashawishi Watanzania Wakiamini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
My Take
1.Utaamini chama ambacho kwanachaguana Kwa rushwa?

2.Utaamini chama ambacho kina viongozi wanaonunulika kama nyanya?

3.Utaamini chama ambacho hakina Sera?

4.Utaamini chama ambacho kinatumia vurugu kulazimisha mambo Yao?

5.Utaamini chama ambacho kinatukana Watanzania?

6.Utaamini chama ambacho ni wakala na kibaraka wa Mabeberu?

7.Utaamini chama ambacho Viongozi wake wanafamilia Nje ya Nchi,wakikiwasha wanakimbia huko.

8.Utaamini chama ambacho kinategemea ushawishi wa mtu mmja mmja badala ya taasisi?

9.Utaamini chama ambacho kinahubiri Demokrasia huku wao Wakiwa hawana Demokrasia?

10.Utaamini chama Cha msimu wa uchaguzi?

11.Utaamini chama ambacho hakina itikadi kinaenda kama genge la wahuni au Mali ya mtu binafsi?

Mengine ongezeni wenyewe 😁😁😁😁👇👇

Dkt. Slaa apewe Ulinzi Kwa kusema ukweli huu maana Hawa Jamaa Huwa hawapendi kuambiwa ukweli.

Na ieleweke vyema kwamba Watanzania wamekubali sera na utekelezaji wa ilani ya CCM ndio maana wamewapuuza Wapinzani uchwara 👇👇

---
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Peter Slaa, amekosoa vikali viongozi wa sasa wa chama hicho kwa kushindwa kuwaongoza wananchi ipasavyo na kutokujenga uelewa wa kutosha juu ya wajibu wao wa kisiasa.

Akizungumza kupitia mtandao wa Clubhouse hivi karibuni, Dkt. Slaa alieleza kuwa CHADEMA imeshindwa kuwapatia wananchi ujasiri na uwezo wa kuleta mabadiliko makubwa nchini, hali iliyosababisha wananchi kubaki katika hali ya kutojiamini na kutegemea zaidi uongozi wa chama kuliko kuwa na nguvu zao wenyewe.

Katika mazungumzo yake, Dkt. Slaa alitilia mkazo umuhimu wa chama kuwa na mikakati ya kuwajengea uwezo wananchi, akieleza kuwa kwa muda mrefu wananchi wa Tanzania hawajawahi kupewa mwongozo madhubuti wa kujitegemea katika harakati za kisiasa.

"Usitegemee wananchi wawe mstari wa mbele, wanahitaji kuongozwa... CHADEMA mliwajengea uwezo? Upi? Kama mliwajengea uwezo wamefika wakashindwa kutekeleza, wananchi wajibu wao nini?" alihoji Dkt. Slaa, akisisitiza kuwa ni jukumu la viongozi wa kisiasa kuwaongoza wananchi na kuwapa moyo wa kusimama kidete kwa ajili ya haki zao.

Dkt. Slaa alitoa mfano wa matukio mbalimbali ya siku za karibuni likiwamo tukio la Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) kuchoma vitenge vilivyokuwa vimetolewa kama zawadi na Rais Samia Suluhu Hassan. Tukio kama hilo ni ishara ya namna chama kimeshindwa kuleta ushawishi wa kutosha kwa wananchi.

“Kwenye suala hili kwa mfano la kuchoma kanga na vitenge, wananchi hawakumualika Rais Samia, nyinyi ndiyo viongozi mliomualika, mlikwenda kama chama kwenda kumbana Samia kwamba ulitupa zawadi, sasa leo tunataka kuchoma hizi zawadi na mkachoma mbele yake? Wananchi mtawaingiza kwenye matatizo tu bila sababu”, amesema Dkt. Slaa na kuongeza,

“Wananchi wana jukumu lao, wananchi mliwaomba kwenye maandamano wametokea. Wananchi wanahitaji kupewa ujasiri, na kauli za vyama vya upinzani juu ya maandamano zilitokaje?"

Aidha Dkt. Slaa amezungumzia suala la maridhiano akilitaja kuwa halikuwa shirikishi kwani CHADEMA walikaa kwenye meza moja na serikali katika mchakato wa maridhiano bila kuwa wazi kwa wananchi. Alidai kuwa kitendo cha viongozi wa chama kukaa na serikali kimya kimya kiliwafanya wananchi kuendelea kukosa ujasiri wa kushiriki kikamilifu katika harakati za kisiasa.

"Leo unategemeaje wananchi walipuke wakati nyinyi wenyewe mlikuwa mnakaa meza moja na serikali mkinywa juisi... Vitendo vile vilifanya wananchi waendelee kulala," alisema Dkt. Slaa, akiongeza kuwa chama kilipaswa kuwa na mikakati ya wazi na madhubuti ya kushirikiana na wananchi ili kuongeza hamasa katika kudai haki.

Pia, Dkt. Slaa alieleza kuwa chama kinachotaka kushinda na kuongoza lazima kiwe na mbinu nyingi na za kisasa za kufanikisha malengo yake. Alihoji kama CHADEMA imewahi kuwa na mbinu zaidi ya elfu moja kama ambavyo chama tawala, CCM, hujigamba kuwa nacho.

"CCM wana mbinu elfu moja, nyinyi CHADEMA mna ngapi? Mliwahi kutoka hadharani kutuambia?" alihoji Dkt. Slaa,

Kwa upande mwingine, Dkt. Slaa alitoa changamoto kwa viongozi wa sasa wa CHADEMA kuwa wazi na kutoa taarifa zaidi kwa umma juu ya mbinu na mikakati yao ili kuwaongezea wananchi imani na ujasiri katika harakati za kisiasa. Alisema kuwa kama viongozi wa CHADEMA walitoka salama kwenye kesi ya ugaidi, basi walipaswa kutumia fursa hiyo kuonyesha wananchi jinsi walivyopambana na changamoto kubwa na kuwahamasisha kuendelea na mapambano ya kisiasa kwa ushirikiano wa karibu.
 
My Take
Utaamini chama ambacho kinagombea rushwa?

Utaamini chama ambacho kina watu wanaonunulika?

Utaamini chama ambacho hakina Sera?

Utaamini chama ambacho kinatumia vurugu kulazimisha mambo Yao?

Utaamini chama ambacho kinatukana Watanzania?

Utaamini chama ambacho ni wakala na kibaraka wa Mabeberu?

Utaamini chama ambacho Viongozi wake wanafamilia Nje ya Nchi,wakikiwasha wanakimbia huko.

Utaamini chama ambacho kinategemea ushawishi wa mtu mmja mmja badala ya taasisi?

Utaamini chama ambacho kinahubiri Demokrasia huku wao Wakiwa hawana Demokrasia?

Utaamini chama Cha msimu wa uchaguzi?

Mengine ongezeni wenyewe 😁😁😁😁👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DBaya1fC1lM/?igsh=aHBxemJ0Z3RrMWtu

Mda ukfka tutaongeza kngne saif tupo bze kusuka mfumo wa gadiola na zidane
 
HILI NALO MKALITAZAME.

Nawaagiza akina Kasimu na Kamanda Muliro mwende mkalitazame kwa makini ili tujue TUNAKWENDA VIPI.

Tumeanza kusikia vijikelele kelele kutoka kwa Kakaangu MBOWE kuwa CHADEMA imedorora, sasa nawaagiza mwende mkalitazame hili swala kwa makini kisha mnirudishie ripoti yenye HADIDU REJEA.

Kamanda Muliro nina imani na uzoefu wako wa kucheza JUDO hivyo nakutuma uende ukaiokoe CHADEMA ili tuweze kusonga mbele kama taifa.

Wewe ni KAMANDA, na mimi ni MAMA. UKINIKUNA NITAKUKUNA.

Cc: Mbaga Jr Lucas Mwashambwa Poor Brain Nyani Ngabu chiembe FaizaFoxy
 
Dr Slaa ni mkubwa kuliko Vyama Vyote vya Siasa

Dr Slaa ndiye alipewa Jukumu la kuratibu ziara ya baba Mtakatifu wa Dunia nzima Papa Yohane Paul I I na Rais Mwinyi

Kanisa Moja Takatifu la Mitume 🌹
Upinde 🚮🚮
 
Baada ya kujaribu kutumia mtutu wa bunduki kubackfire Jiwe akaamua Kutumia Rupia kununua wanachadema kimbelembele. Baada ya wananchi kuona kuwa hawa jamaa wananulika kirahisi wakaanza kuipuuza Chadema.

Lakini kingine kilichowakatisha watu tamaa ni kuona CHADEMA inaflipflop kwenye misimamo ya msingi. Kumleta Lowasa ambaye hakuwa anaamini hata kwenye misingi ya CHADEMA kuliwapa CHADEMA temporary gain lakini longterm damage, maana ilibidi CHADEMA wajifanye hamnazo ili kumnadi wakati walimuita fisadi kwa miaka mingi sana. Wananchi wanaziona hizi flipflops
 
Baada ya kujaribu kutumia mtutu wa bunduki kubackfire Jiwe akaamua Kutumia Rupia kununua wanachadema kimbelembele. Baada ya wananchi kuona kuwa hawa jamaa wananulika kirahisi wakaanza kuipuuza Chadema.

Lakini kingine kilichowakatisha watu tamaa ni kuona CHADEMA inaflipflop kwenye misimamo ya msingi. Kumleta Lowasa ambaye hakuwa anaamini hata kwenye misingi ya CHADEMA kuliwapa CHADEMA temporary gain lakini longterm damage, maana ilibidi CHADEMA wajifanye hamnazo ili kumnadi wakati walimuita fisadi kwa miaka mingi sana. Wananchi wanaziona hizi flipflops
Unaweza kiamini chama ambacho kinawafundisha watu kutengeneza value ya kununuliwa?

Wanaofika bei watakuja kupiga bei Nchi.
 
Back
Top Bottom