Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

Huu ni uthibitisho mwingine wa namna Chadema walivyokwepa risasi kwa kumtosa na kwenda na Lowassa. Huyu angeunga mkono juhudi katikati ya kampeni.

Amandla...
 
Siku hizi humu baada ya uzi ni matusi tu. Kwani mnaomtukana huyu mzee mnakosoa hoja ipi? Zamani watu wali quote sentensi na kupangua hoja! Mbona mambo mengi kaongea kwa ushahidi mzuri tu? Au mnataka kusikia yanayowasha masikio yenu tu!
 
Siku hizi humu baada ya uzi ni matusi tu. Kwani mnaomtukana huyu mzee mnakosoa hoja ipi? Zamani watu wali quote sentensi na kupangua hoja! Mbona mambo mengi kaongea kwa ushahidi mzuri tu? Au mnataka kusikia yanayowasha masikio yenu tu!

..Dr.Slaa anasema hataki kuzungumzia suala la Lissu.

..halafu baada ya hapo anazungumzia suala la Chadema kumteka na kumuumiza mwanachama wake.

..ukisoma between the lines, ni kwamba Dr.Slaa anadai kuwa inawezekana Chadema ndio waliojaribu kumuua Tundu Lissu.

..sasa kama ameamua kusema hivyo basi walau angetoa na mfano wa kijana wa Chadema aliyetekwa na serikali, Ccm, au chombo kingine.

..binafsi nadhani Dr.Slaa kila anapojaribu kuzungumzia suala la Lissu basi anaishia " kuteleza. "
 
Huyo Joseph alikuwa Chadema na inaelekea alikuwa ni mtu wa karibu wake. Waliomteka na kutaka kumuua walikuwa Chadema. Mmoja wa waliomteka akaja akakiri kwake kuhusu kuhusika kwake katika jaribio la kutaka kumuua Joseph, mtu wake wa karibu. Alipoambiwa kuwa lilikuwa ni agizo la viongozi wenzake akanyamaza. Huyu Padri alishindwa kuwakabili viongozi wenzake ili kuhakikisha vitendo hivyo visiendelee! Au hata kutaka tu haki itendeke tu kwa mtu aliye karibu nae na kuhakikisha kuwa hao Red Brigade hawarudi kumalizia walicho kusudia kufanya!

Kama anachosema ni kweli, anajua wangapi wameumizwa ambao angeongea wasingeumizwa? Hata Lissu asingepigwa risasi, Mbowe asingekanyagwa, Ben Saanane asingepotea maana uovu wote huu ulifanywa na Red Brigade.

Watu wa karibu nae wamwambie aache tu kuongea maana anazidi kujiharibia. Mimi nilimfuta pale aliposema kuwa human rights sio kipaumbele cha watanzania. Padri anasema hivyo kweli? Ni beyond redemption.

Amandla...
 
Kwamba chadema ndio waliotoa CCTV camera kwenye eneo la tukio pamoja na kuwafukuza polisi wa doria wanaolinda eneo hilo ili kupisha shambulizi?
Hizi ndio hoja za kumuuliza atoe maoni. Walau wewe umeibuka na hoja ya msingi. Dr Slaa kwa principles zake za kusimamia ukweli, hili la Lissu hajalisemea kwa viwango tunavyotegemea kwa levels zake.
 
I agree with you! Majibu yake kuhusu hili yanaleta tafsiri nyingi. Vipi kuhusu hoja zingine?
 
Naona mnamchambua yeye! Angekuwa kilema ndicho mngechambua. Jadilini hoja zake! Otherwise tumejaa unafiki tu! Hapa wote CCM na Chadema mtaungana sababu vyama vyenu ni sehemu ya tatizo nchi hii.

..sidhani kama huyu bwana anaishi kwa principles.

..angekuwa anaishi kwa principles asingewezana na ukandamizaji uliokuwa ukifanywa na serikali ya Magufuli.

..kwa upande wangu nadhani Dr.Slaa huwa ngangari na loyal kwa taasisi inayompatia mlo wake.

..wakati Chadema wakimpatia mlo alikuwa ngangari kuitetea. Magufuli alipokuwa akimpatia mlo alimtetea kwa nguvu zote.

..sasa hivi Dr yupoyupo akisoma upepo utaelekea wapi, lakini hawezi tena kufikia viwango alivyofikia akiwa Chadema.
 
Huyu jamaa kama manara

Muda wote anaiwaza chadema
 
Hizi ndio hoja za kumuuliza atoe maoni. Walau wewe umeibuka na hoja ya msingi. Dr Slaa kwa principles zake za kusimamia ukweli, hili la Lissu hajalisemea kwa viwango tunavyotegemea kwa levels zake.
Huyo dingi kama ameyasema hayo katika utimamu wake bila msukumo wa kitu kingine kichwani mwake basi hata watoto wake wakae naye kwa tahadhari sana
 
As usual toka amerudi na kuwa jobless ameona ili kuwa relevant aongelee mambo ya CHADEMA tu, kwani hana mambo ya kujadili especially mustakabali wa siasa zake maana huyu CCM hawamtaki na upinzani labda aanzishe au ajiunge na hicho chama kinachoendeleza siasa za Magufuli labda atapewa cheo apate chakula.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…