Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

Binafsi nilijua kadiri umri unavyosonga ndivyo busara inakua kubwa, Lakini kwa huyu Dokta Mihogo hakika anazidi kuwa hayawani.!

This is too bad.
Wewe na busara zako ndo zimekufundisha kumuita mtu fisadi Zaid ya miaka8 na Kisha kuja kumnadi kwenye kampeni kama mgombea wako!!
 
Njaa mbaya sana, mzee anafukuzia kauteuzi laki anakosea step, kuegemea Sukumagang kunamkosesha teuzi
We unafikiri KWA heshima ya Dr.slaa enzi na enzi angeamua kuuza utu wake KWA pesa angekua wapi?Mmezoea wanasiasa malaya malaya ndo Tatzo,leo mnamuita Fisadi kesho ndo apeperushe bendera ya chama
 
Tunakushukuru sana Mungu kwa kutuondolea huyu Mamluki Chadema
Shame on you,Unaijua Chadema na kutukana humu KWA sababu take yeye kukuhubiria na kujenga imani ya hicho chama mpaka Sasa unalipwa kushinda humu kuandika habari za porojo porojo,Slaa anapeperusha bendera ya chama 1995 we ulikua wapi!!
 
We unafikiri KWA heshima ya Dr.slaa enzi na enzi angeamua kuuza utu wake KWA pesa angekua wapi?Mmezoea wanasiasa malaya malaya ndo Tatzo,leo mnamuita Fisadi kesho ndo apeperushe bendera ya chama

..umesahau majina ambayo Ccm walikuwa wanamuita Dr.Slaa, halafu leo ndio wanamkumbatia?

..Na Lowassa alivyokuwa akitukanwa alipohamia Cdm, halafu aliporudi Ccm waliokuwa wakimtukana walisemaje?
 
Heko mzee Slaa,siku zote simamia ukweli daima na ndo legacy itayoeza ishi daima,Hawa CDM na wenzao Kijani ni watu walokosa morality ya kukemea ufisadi.

Nchi hii kuna wapuuzi wanajidai wafia chama,siku zote ni bendera fata upepo na ndo wamejaa humu kutusi na kubwabwaja KWA kuangalia upepo wa mabwana zao
 
..Dr.Slaa ameulizwa mara nyingi suala la Tundu Lissu.

..lakini mpaka sasa hivi bado anatoa majibu yasiyoendana na Dr.Slaa wa kabla hajahama Chadema.

..angekuwa amekosea mara ya kwanza tungeweza kusema ni bahati mbaya, but over and over anatoa majibu ya ajabu-ajabu.

cc MTAZAMO
Kuna siku alijibu na kicheko cha kejeli kuwa “cha ajabu Lissu kupigwa risasi ni kipi? Marekani watu wanapigwa risasi kila siku na maisha yanaendelea”! Nilishangaa sana; nikajua huyu mzee keshapinda kweli kweli.

Anyway, Dr. Slaa’s moment of fame ended at Serena Hotel in 2015. Wanaompa nafasi ya mahojiano siku hizi wajue pale hakuna thamani tena: no value for money. He’s already gone overboard.
 
..umesahau majina ambayo Ccm walikuwa wanamuita Dr.Slaa, halafu leo ndio wanamkumbatia?

..Na Lowassa alivyokuwa akitukanwa alipohamia Cdm, halafu aliporudi Ccm waliokuwa wakimtukana walisemaje?
Hakuna ccm fisadi anayeweza mkumbatia Dr.slaa,ila wale smart na wasio wafia vyama ndo wanaelewa Dr.Slaa siku zote anasimamia misimamo.CHADEMA HAWATOKUJA KUJISAFISHA KWA KUPOKEA MAFISADI.
Hilo linatosha kabisa Bila kuanza kuingia ndani,Drama zao na CCM sisi tunaona waigizaji tu na ndugu zao kina mzito kabwe
 
1. Sikubaliani naye kuhusu mtazamo wake kuhusu ripoti ya CAG kwamba isiwe public discussion. Mimi nadhani hoja za CAG zijibiwe na hao walioandikwa "vibaya." Hoja hizo zijibiwe kwa wananchi na zijibiwe mbele ya kamati ya bunge.

2. Sikubaliani na mtizamo wake kuhusu wabunge 19 ambao Chadema iliwakana. Ningemuelewa kama angeshauri mamlaka za uchunguzi zifuatilie kujua kilichotokea. Kama Chadema wanakana kuwa hawakuwapitisha wanachama wao kwenda bungeni, je nani aliwawezesha? Hilo ni suala la POLISI / TAKUKURU kuchunguza.

3. Kuhusu suala la Tundu Lissu, hivi Dr.Slaa anashindwa hata kutoa pole? Dr.Slaa anashindwa kushauri iundwe Tume ya Uchunguzi ili tujue nani alitaka kumuua mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni? Dr.Slaa anashindwa kumtaka Spika / Bunge lieleze Kamati ya Adadi Rajabu ilitoa ripoti gani ilipotakiwa na Spika Ndugai kuchunguza suala hilo?

4. Sikubaliani na kauli zake kuhusu Katiba Mpya. Kauli kwamba Katiba sio muarubaini wa matatizo ya Watanzania ni kauli zinazolenga kufifisha juhudi na harakati za kudai Katiba mpya. Hakuna aliyedai kwamba Katiba mpya ni muarubaini wa matatizo ya nchi yetu. Katiba sio muarubaini, sasa kwanini tuliandika katiba ya 1962, 1965, na 1977? Na kwanini tusiandike mpya sasa hivi kama tunaamini ya 1977 haitufai?
1. Mtu anayeamini katika transparency atasemaje kuwa ripoti ya CAG iwe siri na wananchi wapewe taarifa tuu itakayopitishwa na Bunge la Ndugai na Tulia?
2.Chadema watamshtaki nani wakati wao hawana ushahidi wowote wa kabrasha zilizotumiwa na Ndugai kufikia uamuzi wake. Wao wanasema hawakuandika barua yoyote kwa taasisi yeyote kuwapendekeza wakina Halima. Onus ilikuwa kwa Spika/ Mahere kutoa uthibitisho kuwa Chadema waliandika barua hiyo. Hapo ndipo Chadema wangeweza kwenda Mahakamani kushtaki kuwa sahihi zao zimekuwa forged.
3. Hilo la Lissu halistahili jibu. Lakini si ajabu. Kama mtu anasema kuwa alinyamaza pale jaribio la kumuua Joseph asingeweza kusema kitu kwenye tukio la Lissu halafu a jeopardise ugali wake. He is a coward.
4. Huyu alisema Human Rights sio kipaumbele cha watanzania. Ata support vipi Katiba.
Ametoa mfano wa Marekani na jaribio la Trump kubatilisha matokeo ya uchaguzi mkuu. Asichosema ni kuwa waliomzuia kufanya hivyo ni viongozi waliokataa kukiuka Katiba. Secretary of State wa Georgia alimkatalia ingawa nae ni Republican. Pence pia alimkatalia. Hapa kwetu wakina Mahere na maDED wanakiuka Katiba with abandon kwa sababu wanajua hamna consequences kwa kufanya hivyo. Pence alijua angemkubalia Trump angeishia lupango. Katiba bora ni muhimu. Na Katiba ni kitu hai ambacho kinaboreshwa kila inapobidi.

Amandla...
 
Kuna siku alijibu na kicheko cha kejeli kuwa “cha ajabu Lissu kupigwa risasi ni kipi? Marekani watu wanapigwa risasi kila siku na maisha yanaendelea”! Nilishangaa sana; nikajua huyu mzee keshapinda kweli kweli.

Anyway, Dr. Slaa’s moment of fame ended at Serena Hotel in 2015. Wanaompa nafasi ya mahojiano siku hizi wajue pale hakuna thamani tena: no value for money. He’s already gone overboard.
Ila wewe wenye thamani kwako ni Wale wanakwambia zungusha mikono ndo mabadiliko!!Nyi jamaa akili kisoda sana
 
Hakuna ccm fisadi anayeweza mkumbatia Dr.slaa,ila wale smart na wasio wafia vyama ndo wanaelewa Dr.Slaa siku zote anasimamia misimamo.CHADEMA HAWATOKUJA KUJISAFISHA KWA KUPOKEA MAFISADI.
Hilo linatosha kabisa Bila kuanza kuingia ndani,Drama zao na CCM sisi tunaona waigizaji tu na ndugu zao kina mzito kabwe

..tatizo ni Dr.Slaa kuikumbatia Ccm baada ya kuondoka Cdm.

..ni afadhali angetafuta chama kingine cha upinzani halafu akaendeleza harakati zake.

..huwezi kushambulia Ccm ya mafisadi, halafu ukakumbatia Ccm ya watekaji na wauwaji, halafu ukatarajia watu wakuheshimu.

cc MTAZAMO, Nguruvi3
 
CDM mnatokwa povu humu mpaka Basi mtafikiri Dr.slaa kawasingizia,nyinyi ni CCM-B kwa matendo na hata kauli zenu,Nyinyi ni waroho wa madaraka,wachumia tumbo,bendera fata upepo tu
 

Mwanasiasa Willbrod Peter Slaa amefanya mahojiano na kuzungumza mambo mengi kuhusu siasa, mahojiano haya ni mwendelezo ya interview aliyofanya wiki iliyopita.

TAARIFA YA CAG INAPOTOSHWA
“Kuna upotoshwaji kwenye taarifa ya CAG, nadhani Zito Kabwe angelisaidia sana taifa hili kama angekuwa mkweli, mimi na Zitto tulishiriki kutengeneza sheria ya ukaguzi wa fedha 2009, hata maneno yaliyopo kwenye sheria hiyo yametoka kwetu.

“Moja ya maelezo ya ile sheria inasema baada ya CAG kukabidhi ripoti yake kwa Rais kisha kuifikisha Bungeni siku saba baadaye, ripoti hiyo haitakiwi kuwa public discussion, kwa kuwa ni kama mhtasari tu wa ripoti.

“Inatakiwa Kamati ya Bunge ndiyo iifanyie kazi, mfano kuna sehemu unaweza kukuta risiti haikuonekana wakati wa ukaguzi lakini hiyo ikapitishwa na kuonekana ni wizi, tumepotosha maana ya ile taarifa ya CAG.

CAG AMESABABISHA TAHARUKI KWA RIPOTI YAKE
“Kwanza hata CAG mwenyewe amechangia kuleta hii taaruki kwa kuwa huwa ni ya awali tu na analijua hilo, inatakiwa irudi kwa akaunti ofisa wa Serikali ijadiliwe, pia CAG wakati anatoa taarifa zake hadharani hatakiwi kuingia ndani kutoa ufafanuzi zaidi kama anavyofanya.

“Unaweza kukuta ripoti hiyo ikifika kwenye Kamati ya Bunge vitu vingi vikawekwa sawa, mfano labda kulikuwa na upotevu fulani wa mambo madogomadogo ambayo kwa nje yanaonekana kama ni wizi lakini details zikiwekwa sawa kunakuwa hakuna tatizo.

UBUNGE WA KINA MDEE SPIKA HANA KOSA, NITAZUNGUMZA CHADEMA WAKISHAKAA KIKAO
“Nimeona kwenye vyombo vya habari kuwa watajadiliwa na chama chao katika rufaa yao, naona lawama zimepelekwa kwa mtu ambaye hausiki (Spika).

“Chama kilitakiwa kufungua kesi Mahakamani kuhoji Tume ya Uchaguzi kwa kupitisha majina hayo lakini sijaona kesi. Mimi nitazungumza baada ya rufaa yao kupitiwa na CHADEMA, nimesikia wanakaribia kuwajadili kwenye kikao chao.

HOJA YA KATIBA SIYO MAHITAJI MUHIMU YA WANANCHI
“Mabosi wa vyama vya siasa ni wananchi, wanatakiwa kujiuliza wanayoyafanya yanawagusa vipi wananchi, kwa sasa kuna mambo mengi ya muhimu lakini hivyo vyama vimekuwa bize kuzungumza habari za ajenda ya Katiba.

“Hawana ajenda ambazo mwananchi anaweza kujiuliza kama inaweza kuweka chakula mezani, hakuna katiba ambayo inaweza kuzungumzia kila kitu.

“Katiba yetu ina vipengele vingi vya muhimu lakini havitekelezwi, japo sijasema kuwa katiba siyo muhimu.

“Mimi ni kati ya watu waliozunguka Tanzania kukusanya maoni lakini tusipotoshe kuwa katiba ndiyo jibu la kila kitu, siyo kweli.

“Leo hii Marekani ina katiba tunayoisifu lakini Donald Trump si alishutumiwa anataka kufanya mageuzi.

KATIBA PENDEKEZWA NI MBOVU KULIKO KATIBA YA SASA
Sisi tuna maoni ya Jaji Warioba, licha ya kuwa kulikuwa kuna mambo yamekosekana lakini yapo mazuri ambayo tunaweza kuyatumia.

“Baada ya maoni hayo kupelekwa Bungeni ikachujwa ikatoka inayoitwa Katiba Pendekezwa, ni mbovu kuliko hata katiba tuliyonayo sasa hivi.

SIZUNGUMZII SUALA LA LISSU KUPIGWA RISASI SABABU UTEKAJI ULIKUWEPOA CHADEMA
“Kuna watu wananiuliza kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi, kuwa sipendi kulizungumzia hilo kwa kuwa sita taarifa zake za uhakika.

“Nitoe mfano iliwahi kutokea huko nyuma nikiwa Katibu Mkuu CHADEMA, nililetewa taarifa za mtu wangu anaitwa Joseph, huyu alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, alitekwa saa sita usiku. Kesho yake saa sita mchana nikahitisha mkutano na waandishi wa habari nikaisema sana Serikali na Usalama wa Taifa.

“Saa nane mchana siku hiyohiyo Joseph akapatikana, alikutwa ametupwa maeneo ya Ununio ameumia sana usoni.

“Mwezi mmoja baadaye kijana wangu wa Red Brigade anakuja kwangu kuniambia yeye ndiye aliongoza kukosi cha kwenda kumteka nyara huyo mwenyekiti huyo.

“Nikauliza kwa nini hakuja kwangu akasema ‘wapo viongozi wanaojua’, nikaamua kunyamaza, ndiyo maana ninapoulizwa suala la Lissu ninasema hapana, CHADEMA kwanza wajiangalie wao ndani.

“Huyo kijana (Joseph) walivyomtupa ufukweni walijua amekufa, kumbe alikuwa hajafa labda upepo ulimpiga akaamka. Miaka kadhaa baadaye tukaanza kusikia watu wanaokotwa wamekufa ufukweni, unadhani inatoa pcha gani!

“Ukiwa kiongozi lazima uwe kunasema ukweli hata kama unaona watu wako wanakosea.

SINA TATIZO LA LOWASSA
“Mimi na Lowassa tulipishana kwenye principal siyo maisha, mimi niliwahi kufanya fund rising na Jakaya Kikwete siku moja baada ya kupanda jukwaani na kumsema tena kwa mambo mazito.

“Nimeishi Ulaya, nimeona mambo ya kwenye mabunge, kuna muda inafika hatua wabunge wanapigana ngumi lakini wakitoka wanaenda kunywa bia. Unatakiwa kutofautisha maisha binafsi na siasa. Hivyo sikuwa na tatizo binafsi na Lowassa.

AWAMU YA TANO HAIKUFELI DIPLOMASIA YA KIMATAIFA
“Watanzania tuwe wakweli, tumefeli wapi, mimi nimekutana na wafanyabiashara wengi, wapo walioniambia wamchoshwa na Tanzania yenye ufisadi.

“Wapo walioamua kuondoa biashara zao huko nyuma lakini katika awamu ya tano waliamua kurejesha biashara hapa nchini, kwa nini? Ni kwa sababu kulikuwa kuna mambo mengi yanaenda vizuri, nazungumza kwa kuwa najua zaidi kilichokuwa kinaendelea.”



Chanzo: Dar24
Kwamba Lisu alitekwa na CHADEMA tumuogope Mungu maana kulikuwa na haja gani tena Mbowe kuhangaika kumpeleka Nairobi si angemwacha afe ili litimie walilopanga kama Chama.
 
..tatizo ni Dr.Slaa kuikumbatia Ccm baada ya kuondoka Cdm.

..ni afadhali angetafuta chama kingine cha upinzani halafu akaendeleza harakati zake.

..huwezi kushambulia Ccm ya mafisadi, halafu ukakumbatia Ccm ya watekaji na wauwaji, halafu ukatarajia watu wakuheshimu.

cc MTAZAMO, Nguruvi3
Slaa always Yuko free na wala haikumbatii hao mafisadi wenzenu wa fisiemu,Nyinyi ndo mnalazimisha kuwa hivyo na hata yeye kawa muwazi tu na kusema ufisadi umeanza kurudi,KAZI kwenu wafia vyama mlonyang'anywa fikra huru KWA mgongo wa vyama
 
Mdini sana huyu Mzee.
Kila akitokea Kiongozi Muislam Dr. Slaa anapanua mdomo Kama Chai Jaba.

Hivi haoni kuwa uhuru wa kisiasa ndio unampa fursa ya kuzungumza na kutetea Chama chake Cha UP.!!
Hatapata wanachama ndio atajua kuwa yeye SI chochote si lolote ndani ya CCM Wala Chadema.

Hawezi kupata wanachama hata laki Moja.
Kama anabisha 2025 achukue fomu agombee aone kuwa Watanzania sio wajinga.

Yani mpumbavu sana huyu Slaha mihogo ,amesahau watu walivyopoteza maisha Kwa maandamano aliyokua anayaratibu akiwa Katibu mkuu wa Chadema.? Amesahau kuwa Kuna watu walikua wanafungwa Kwa sababu ya kutaka haki hasa wakati wa uchaguzi ?

Hivi huyo Slaa haoni kuwa Afrika hakuna mtu anayetegemea serikali kula? Hata kabla ya hizi takataka za kikoloni zinazoitwa serikali na maendeleo kuja Afrika waafrika walikua wanatafuta chakula Chao wenyewe. Sasa kusema kuwa Katiba haimpi mtu chakula mezani ni kuwadharau watanzania. Yeye ndiye anayepewa chakula mezani lakini wanyonge wanajitafutia wenyewe hawahitaji serikali iwape chakula. Hata somalia pasipo na serikali watu wanaishi. Watu wanataka haki tuu. Watu wanataka wapate haki sawa mbele ya vyombo vya dola lakini haki ya kupanda na kufikia ndoto zao za kisiasa bila kuzuia na Dola Kwa sababu ya kulinda CCM pekee. Watu wanataka CCM iwekwe madarakani kihalali na waonyesha hayo waliyofanya sio Kwa kubebwa na Polisi na Tume.

Kama Dr. Slaa hajui ugumu wa kuendesha shughuli za kisiasa chini ya Katiba iliyopo basi Hana tofauti na mtoto wa kishetani anayemtoa baba yake kafara ili apate Mali.
Afrika Ina laana mbaya sana kuwa na wanasiasa wanafiki wanaojali matumbo yao.

Waafrika wanapigania mtu badala ya falsafa.
Kwa nchi yetu na Katiba iliyopo ni Bora TU Dr. Slaa akae kimya ale alichopewa na serikali ya CCM mana kama ana ndoto za Urais basi anajidanganya. Haiwezekani hii nchi akabidhiwe padri muasi. Mtu aliyemuasi Mungu hawezi kuwa mwaminifu Kwa wanadamu ndio maana hazungumzii haki. Kazi ya serikali ni kutenda haki.
Maendeleo ni Kodi za Wananchi wenyewe sio hisani. Haki ndiyo itakayowafanya Watanzania wapate mrejesho wa Kodi yao.

Leo Slaa amesahau kuwa wabunge na kamati zao wamekua wakihongwa ili watetee wezi ? Amesahau Sakata la Jairo. Leo anamfunga mdomo Zito wakati Kuna utata. Alikufa ni Magufuli Sasa Kuna dhambi Gani kuwajibishwa wasaidizi wake walioiba wakati wapo.? Hofu yao Nini kama sio kweli wezi wapo. ?
Magufuli alikua ni Rais lakini alikua na wasaidizi ambao ndio walioipaka matope serikali yake , wawajibishwe wao sio hayati. Aliwaamini wakamwangusha na kumpa ripoti za uongo.

Tunajua Slaa ni lile kundi lisilomkubali Mama Samia ndio maana anazunguka zunguka TU na vijembe vyake akidhani kuwa mama naye anaipenda hii katiba mbovu. Mama ni Mpenda haki na Demokrasia. Hakuna mpenda haki anayeamini katika katiba inayowafanya watawala kuwa miungu. Rais anakua na mamlaka makubwa kuliko Mungu kwenye nchi iliyoumbwa na Mungu . Haya maisha ni ya kupita TU hakuna haja ya kujisahau kama hao wazee wanavyojisahau wakidhani wataishi milele.
 
Slaa always Yuko free na wala haikumbatii hao mafisadi wenzenu wa fisiemu,Nyinyi ndo mnalazimisha kuwa hivyo na hata yeye kawa muwazi tu na kusema ufisadi umeanza kurudi,KAZI kwenu wafia vyama mlonyang'anywa fikra huru KWA mgongo wa vyama

..Dr.Slaa amesema nini kuhusu ubaguzi, utesaji, utekaji, na mauaji, ktk awamu ya 5 ?

..Umesahau kwamba Dr.Slaa aliwahi kusema kuwa akipata madaraka atamfunga Dr.John Magufuli?

..Dr alitakiwa kuanzisha chama au kujiunga na chama kingine cha upinzani lakini sio kujiegemeza Ccm.
 
Kweli kwenye siasa hamna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu🤗
 
Back
Top Bottom