Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

Nakukumbusha tu maana umesahau hata juzi juzi tu mwangosi ulikuaje?Dr ulimboka unajua nani alimng'oa kucha?Abson kibanda?Mwakyembe?wafanya biashara wa madini?Mashekhe wa uamsho?,bomu la mkutano wa CDM Arusha?Unajua Ulemavu wa mkono wa Dr.Slaa ameupata wap?Na wengine wengi?Walikua wamejificha?

WaTZ wepesi kusahau sanaaa,Juzi mwezi wa12 tu hapa vijana wa4 hawajaonekana Hadi leo,na wengine wanazidi kupotea lakini Mnaleta hoja nyepesi tu.Nyinyi mmeimbishwa hoja na mafisadi na mmeipokea na kucheza Ngoma msiyo ijua,na Sasa mnaona aibu

..Dr hazungumzii tena kuhusu mke wake kujeruhiwa na polisi, ameungana na Ccm waliotuma Polisi kumshambulia.

..lakini kuna tofauti kati ya awamu ya 4 na ya 5 ktk mambo haya ya ukatili. Hoja yangu ni kwamba awamu ya 5 walikuwa wanafanya waziwazi na ndio maana nasema walivuka mpaka ukiwalinganisha na wenzao huko nyuma.

..kuhusu Mwakyembe kwanini hakufuatilia suala lake la kuwekewa sumu? Mwakyembe si alikuwa waziri wa sheria nini kilimzuia?

..Magufuli naye anadai alilishwa sumu kwanini hakuwakamata wahusika alipokuwa Raisi? Hivi inawezekana Magufuli awashughulikie wapinzani na kuwaacha waliomlisha sumu?

..Ni kweli awamu ya 4 walifanya ukatili, lakini wao walikuwa tofauti na awamu ya 5 kwasababu walifanya kwa kificho. Awamu ya 5 walifanya waziwazi na walihalalisha ukatili wakidai wanashughulikia wasaliti.
 
Wewe ndo mdini na si Dr.slaa
Ukiweka akili sawa na kuondoa mind set ya dini utamuelewa vizuri tu.
Nitarudi badae baada ya kula daku
Ni Mdini Mimi sio mwanasiasa. Na hua najua kabisa hata maofisini Kuna watu ni wadini. Hata akiingia mtu amevaa kanzu anamchukia bila sababu. Ni aina ya Slaa. Kuna wakati watu walikua wanachukiwa TU Kwa kufuga ndevu. Lakini tunamshukuru Mungu Sasa kufuga ndevu imekua fashion Kwa watu wote Duniani isipokua tu Wachima mana wengi hata ndevu hawana.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Slaa kamwe hawezi kumsifia Kiongozi asiye wa dini yake.ndiyo hulka aliyo nayo. Ni watu wanaoamini kuwa uongozi unatokana dini yake bila kujua kuwa uongozi ni kipaji.
Hivi unaamini kabisa kuwa Zito anakosea kuchambua ripoti ya CAG.?

Hivi huoni kuwa Kuna rushwa kubwa sana inatolewa na wale waliokuwa kwenye serikali ya awamu ya 5 ili wasije wakachunguzwa ?
Wanamtumia Marehemu Rais aliyepita kama chambo Cha kutafuta huruma.

Serikali ya Awamu ya Tano ilikua na watendaji ambao mpaka Sasa wapo Sasa Kwa Nini wasichunguzwe kama walioiba au hawakuiba. Magufuli hakuwa anatoa VISA , Magufuli hakuwa anafanya kazi BENKI KUU, MAGUFULI HAKUWA ANAJEMGA BARANARA. Magufu hakuwa anafanya kazi bandarini. Sasa Kwa Nini wanapoteza mada Kwa kusema kuwa hatukubali Magufuli achafuliwe. Waliomchafua ni wale aliowaamini na kiwapa nafasi wakafanya ufisadi. Hawa wajiandae TU kuwajibika sio kujifanya wanalinda legacy ya MAGUFULI huku wakiwa wamefuja Mali za umma.
 
HOJA UPINGWA KWA HOJA SIO MATUSI WALA KEJELI.
Nani alimteka na kumtesa Joseph?
Hilo lisipite hivi hivi
 
Utekaji,mauaji,utesaji ulikuepo Tangu nchi hii inapata uhuru na hata Sasa.Labda wewe muhamiaji tu ndo unaona mpya.

Nakukumbusha tu,Dr Slaa anasimamia msimamo uleule.Hakuna kumung'unya maneno mbele ya fisadi na Sasa kasema wazi umerudi na CDM pia hupokea mafisadi.Mbona Yuko wazi sanaaa,Tatzo nchi hii mnaona KILA mtu ni mfia vyama
Hivi wakoloni wangemteka Nyerere alipojaribu TU kuleta siasa akiwa Mwalimu tungewasifia ?

Sasa kumbe baada ya uhuru ndipo yalipoibuka makundi ya kihuni yanayolinda maslahi yao Kwa mgongo wa Dola.
Na Mungu alivyo Kwa Sasa hii Katiba iliyopo itamfyeka mtu yeyote bila kujali Chama. Hata waliopo wakitoka madarakani watasema .
 
Udini kusema ufisadi umerudi au?We ni mgeni nchii hii kushangaa Dr.Slaa kuongelea ufisadi?Wewe ndo mdini ulokosa hoja,unafikiri KWA kutumia mgongo wa dini
Slaa alikua wapi wakati Lisu anazungumzia ufisadi wa Serikali ya Mkapa na wizi wa madini na mauaji wa wazawa kwenye ardhi za madini?

Mbona haoni hasara serikali inayopata mpaka Leo kwa kuuza nyumba za serikali Kwa Bei isiyolingana na Bei ya kiwanja kwenye maeneo hayo au Kwa sababu ziliuzwa na Mkapa. Angeuza Kikwete au Mwinyi angepanua mdomo Kama chura aliyebanwa na mlango.

Slaa ni Mdini sana , narudia Tena ni Mdini Mdini Mdini Mdini hatari sana .Hafai kabisa kuachwa achafue nchi yetu.
Huo ufisadi uliorudi ni upi? Kwa Nini asisubiri ripoti ya CAG Kwa Mwaka wa fedha?

Yani anakuja na speculations zake ndio anaona ni sawa.Atupe data za ufisadi ndio Tumwamini
 
Pale Malaika anapoamua kugeuka Shetani, basi hata Mashetani hugeuka wanafunzi wa kujifunza Ushetani kwake..!
 
Kimsingi Dr Slaa alipaswa aripoti polisi, naamini kama jalada lilifunguliwa angesaidia uchunguzi. Kusema ukweli nje ya muda au sehemu ya kusawazisha mambo aikubaliki! Tukio la Lissu ni tofauti na linaacha alama nyingi ambazo azijashughukiwa, kama kuondolewa CCTV camera, kufuatwa mara kwa mara na aina fulani ya gari, kauli za viongozi kabla na baada ya tukio, kukataza maombi, kuto gharamia matibabu, nk.
 
Kwa Nini Tundu alipigwa risasi nakosa jibu kabisa , alikua na kosa Gani la kustahi ? Ni unyama wa Hali ya juu.
Dr. Slaa kumbe ni kati ya watu katili sana sana Duniani . Nimemchukia sana !
Hakuna aliyejua hili ! maandishi na matamshi yake yanaondoa shaka kuhusu uadilifu wake
Kufurahia na kushabikia BINADAM Mwenzake kupigwa risasi na Majambazi. Hata kama alipigwa na Wenzake wa Chadema hakustahili kupigwa.
D Slaa bado anashaka kama kweli TL alipigwa risasi! Slaa kapatwa na nini?

Mwangosi (pumzika kwa amani) alipigwa risasi mbele ya Dr Slaa na Polisi.
Hadi leo haki haijatendeka kwa aliyefanya unyama ule
Mkewe Dr Slaa alipigwa na Polisi na kuvuja damu.

Leo Padre Slaa ana shaka kama kweli TL alipigwa risasi na kama alipigwa pengine ni chama chake.

Bila haya hata kidogo anadiriki kutoka mfano wa kipuuzi!! mfano wa kitoto na kijinga sana alioutengeneza ili kuhalalisha mauaji au maumivu anayopitia TL.

Slaa hana chembe ya Utu anatafuta mkate kwa kushabikia uvujaji damu, ana push agenda kwamba TL hakushambuliwa na 'wasiojulikana''. Huyu aliyelalamika kuwekewa vinasa sauti Dodoma leo haamini mwenzake anayetembea kwa kuchechemea kwamba kadhulumiwa!

Dr Slaa kapoteza utu, ubinadamu , integrity and credibility yake, anaonekana msema hovyo

Acha kushabikia mauaji , kusukuma agenda uteuliwa katika bodi! Teuzi na vyeo ni mapito tu.

Wewe na mwendazake nani wa kumsaidia mwenzake?

 
..Dr hazungumzii tena kuhusu mke wake kujeruhiwa na polisi, ameungana na Ccm waliotuma Polisi kumshambulia.
Hajali damu ya mkewe ilivyovuja ndiyo maana haoni huruma kwa TL kuchechemea
Haamini kama kweli TL alipigwa risasi! Hiki ni kiwango cha chini kabisa cha maadili ya mwanadamu

Anaamini kabisa kwamba ni Chadema waliofanya hivyo, anakumbatia uongo akijua ni uongo lakini kwa kufikiria kipande cha mkate anajitoa ufahamu.

Dr Slaa atafutiwe washauri wa kumsaidia sidhani kama hii moral decay ni ya kawaida!

Kila siku akitoa kauli ni kujichafua sasa hachafuki tena maana hana pa kuchafuka
 
Hajali damu ya mkewe ilivyovuja ndiyo maana haoni huruma kwa TL kuchechemea
Haamini kama kweli TL alipigwa risasi! Hiki ni kiwango cha chini kabisa cha maadili ya mwanadamu

Anaamini kabisa kwamba ni Chadema waliofanya hivyo, anakumbatia uongo akijua ni uongo lakini kwa kufikiria kipande cha mkate anajitoa ufahamu.

Dr Slaa atafutiwe washauri wa kumsaidia sidhani kama hii moral decay ni ya kawaida!

Kila siku akitoa kauli ni kujichafua sasa hachafuki tena maana hana pa kuchafuka
Mke wake kapewa teuzi,so lazima ajikombe kombe kwa samia
 
Mimi ndio maana nina sympathy kidogo na wakina Halima. Wale toka wamefukuzwa kwenye chama sijawasikia wakitoa maneno ya shombo dhidi ya Chadema na/au viongozi wake. Tofauti kabisa na huyu jamaa.

Amandla...
 
Slaa alisema Wana mpango wa kufungua kampuni kubwa Sana na mshumbushi sijui imefikia wapi
 
Back
Top Bottom