Hutakiwa kuwa mfuasi wa mtu bali mfuasi wa hoja za mtu.
Nijuavyo Dr. Slaa hajawahi kueleza popote kama aliwahi kurudi CCM na kuchukua kadi ya CCM. Alivyotoka CHADEMA alisema kuwa yeye anaachana na siasa za vyama, atabakia kuwa mwanasiasa huru.
Na hivi karibuni aliulizwa kama atarudi CHADEMA, alikataa na kusisitiza kuwa aliishasema kuwa ameachana na siasa za vyama. Sasa, labda useme wewe, ni lini alichukua tena kadi ya CCM? Hata hizi hoja zake za msingi kuhusu uhuni uliofanywa kwenye bandari, serikali yenye mashaka ya uhalali, bunge batili, ni masuala ya uzalendo, hayaangukii kwenye siasa za vyama.
Mpaka hapo, naamini kuwa wale wanaolitazama taifa kwanza, siyo vyama vya siasa kwanza, kwa vyovyote vile wataungana na Dr. Slaa katika hoja zake za kizalendo kuliko ujinga mwingine wowote.