Dkt. Slaa kuongoza kongamano kujadili falsafa ya Hayati Magufuli

Nashauri Tundu Lissu ashiriki hata kama ni virtually. Hii itasaidia kuweka sawa mzania wa falsafa hiyo ya JPM
Hahaha kwani Lissu si unamsikia kila siku huko space?

Lissu hana mawaazo chanya hata siku moja, yye ni negative tu. Hivyo kuwa followers wake ni kujipa mzigo akilini.

Heko Balozi Dk. Slaa.
 
Alisema tuseme mbowe ni gaidi.

I hate Wilbrod Slaa
Hata ukimchukia humpunguzii wala kumuongezea kitu.
Dr Slaa atabaki kuwa mwanasisa mkweli na asiyeyumba wala kuyumbishwa kwa anachosimamia.
 
Balozi Dk Wilbroad Slaa anatarajiwa kuongoza kongamano la tafakuri tunduizi ya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha hayati John Pombe Magufuli.

Kongamano hilo litakalofanyika Ijumaa Machi 25, mwaka huu katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Mwanza pia linalenga kufanya tafakuri ya miaka sita ya utekelezaji wa falsafa aliyoitumia hayati Magufuli wakati akiomba ridhaa ya kuiongoza nchi 2015.

Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake, Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Mwanza, Profesa Costa Mahalu ametaja wazungumzaji wengine katika kongamano hilo kuwa ni Mbunge Mstaafu wa Bariadi Mashariki, John Shibuda na Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Profesa Costa Mahalu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Mwanza.

Wengine ni wahadhiri na watafiti wabobezi wa Historia na Uchumi katika chuo hicho, Profesa Mihanjo Eginald na Dk Anne Gongwe.

"Wakati wa uchaguzi mwaka 2015, tulisikia CCM ikitumia slogani ya Magufuli for Change huku Chadema ikitumia- Movement for Change, kongamano hili litaenda kutafakari utekelezaji kwa vitendo vya slogan hizo," amesema Profesa Mahalu

Profesa Mahalu amewaomba wasomi, wanataaluma na watanzania kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo ili kutoa mchango wao wakati huu ambao nchi inafanya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha Hayati John Magufuli na mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ni uongo, nchi au serikali haina jambo hilo, waseme wao kama wao (Saut) wameamua kufanya hivyo. Wazee wa legacy mtapata tabu sana
 
Hahaha kwani Lissu si unamsikia kila siku huko space?

Lissu hana mawaazo chanya hata siku moja, yye ni negative tu. Hivyo kuwa followers wake ni kujipa mzigo akilini.

Heko Balozi Dk. Slaa.
Upo sahihi kabisa, lakini kupitia kwake tunaweza kupata kujua watanzania wengine wanaizungumziaje falsa ya hayati JPM. Dk Slaa Na wenzake tunajua watasifu tu mwanzo mwisho.
 
Pamoja na mazuri yote aliyoyafanyika chini ya utawala wake pia mjadili na wote waliopotea ama kuumizwa wakati wa utawala wake.
 
Magufuli hakuwa na falsafa yoyote, alikuwa ni mtu wa kukurupuka, hakuna mwanafalsafa mkurupukaji wale anaeunda "kikosi kazi" cha mauaji.

Huyo Slaa ubalozi aliohongwa asitake kulisha watu matango pori.
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Huyu Costa Mahalu, hivi ndiyo yule aliyewahi kuwa Balozi wetu nchini Italy kwenye awamu ya 3, na akaja kushtakiwa na awamu ya 4 kwamba alitumia pesa vibaya? Kabla ya kutetewa na BWM kortini?

Ndiye huyu?
Ndio yeye haswaa. Lakini hakuwa na kosa na aliachiliwa na mahakama lakini pia JPM alimrudishia hadhi ya ubalozi wake. Hakuwa na kosa, yeye alitekeleza maagizo ya rais Mkapa katika ununuzi wa Jengo la ubalozi wa Tanzania Rome kwa namna BM kama mkuu wa nchi aliona ina maslahi kwa Taifa na ndio maana alimtetea. Kushtakiwa kwake ilikuwa ni aina ya kulipiziwa kisasi na JK kwa kumkatalia kutumia kinyume na sheria Diplomatic pouch wakati JK anausaka Urais. Ni aina ya ushamba, ambao viongozi hawatakiwi kuuendekeza. Vijimambo vya JK. Yote sasa ni historia.
 
Balozi Dk Wilbroad Slaa anatarajiwa kuongoza kongamano la tafakuri tunduizi ya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha hayati John Pombe Magufuli.

Kongamano hilo litakalofanyika Ijumaa Machi 25, mwaka huu katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Mwanza pia linalenga kufanya tafakuri ya miaka sita ya utekelezaji wa falsafa aliyoitumia hayati Magufuli wakati akiomba ridhaa ya kuiongoza nchi 2015.

Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake, Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Mwanza, Profesa Costa Mahalu ametaja wazungumzaji wengine katika kongamano hilo kuwa ni Mbunge Mstaafu wa Bariadi Mashariki, John Shibuda na Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Profesa Costa Mahalu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Mwanza.

Wengine ni wahadhiri na watafiti wabobezi wa Historia na Uchumi katika chuo hicho, Profesa Mihanjo Eginald na Dk Anne Gongwe.

"Wakati wa uchaguzi mwaka 2015, tulisikia CCM ikitumia slogani ya Magufuli for Change huku Chadema ikitumia- Movement for Change, kongamano hili litaenda kutafakari utekelezaji kwa vitendo vya slogan hizo," amesema Profesa Mahalu

Profesa Mahalu amewaomba wasomi, wanataaluma na watanzania kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo ili kutoa mchango wao wakati huu ambao nchi inafanya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha Hayati John Magufuli na mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Hao wasemaji wakuu, ukiachilia mbali Professor Costa Mahalu, hawana credibility ya kuwa wasemaji katika jambo serious. Hawana moral authority. Comedian Msukuma kwenda kuongea Chuo kikuu? A very big joke found in Tanzania only! Anatakiwa kuishia kwenye makongamano ya chama cha mpapinduzi na primary schools. Si vinginevyo. Tuweni serious.
 
Magufuli hakuwa na falsafa yoyote, alikuwa ni mtu wa kukurupuka, hakuna mwanafalsafa mkurupukaji wale anaeunda "kikosi kazi" cha mauaji.

Huyo Slaa ubalozi aliohongwa asitake kulisha watu matango pori.
Falsafa ya kutokuvaa barakoa naamini uliitumia na unaitumia
 
Zama za Dr. Slaa zilishakwisha kitambo sana. Hajui anasimamia nini kwa sasa, yaani ni kama popo.

Sio mtu sahihi kuwa katika hilo kongamano kama mzungumzaji. Kifupi anatafuta political attention ili aweze kurejea kwenye siasa za Tz.

Note
Ni dhambi kwa mwanaCCM kwa sasa kuzungumzia falsafa za Mafuguli mbele ya utawala wa Samia, na ilikuwa hivyo hivyo pia wakati wa Utawala wa Magufuli kuzungumzia falsafa ya uongozi wa Kikwete.
CCM Walimuingiza cha kikeni, wakamwambia yeye ni mkubwa kuliko CDM, sasa wamemtumia kama muwa, mzee anabaki amepanic
 
Msukuma mboma hawamuiti Dr. Msukuma?

Wanamshusha hadhi yake.[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hakutafuta shahada ili abadili jina lake.
Mali alizonazo zinatosha kumtangaza kuanzia Angani hadi Ardhini
 
Mnajadili falsafa za Magufuli fo change VS Movement for change huku mmejaza mashabiki wa upande mmoja?
Wamewaalika watu wote tena wa kila nyanja.
Kama unaweza karibu tupambane kwa hoja.
 
Huyu mzee mwisho wake hautakuwa mzuri, sasa amekuwa wakala wa kazi ndogo ndogo za CCM.
 
Ndio yeye haswaa. Lakini hakuwa na kosa na aliachiliwa na mahakama lakini pia JPM alimrudishia hadhi ya ubalozi wake. Hakuwa na kosa, yeye alitekeleza maagizo ya rais Mkapa katika ununuzi wa Jengo la ubalozi wa Tanzania Rome kwa namna BM kama mkuu wa nchi aliona ina maslahi kwa Taifa na ndio maana alimtetea. Kushtakiwa kwake ilikuwa ni aina ya kulipiziwa kisasi na JK kwa kumkatalia kutumia kinyume na sheria Diplomatic pouch wakati JK anausaka Urais. Ni aina ya ushamba, ambao viongozi hawatakiwi kuuendekeza. Vijimambo vya JK. Yote sasa ni historia.
Hakika mkuu! Umenena vyema.. BM alinifurahisha sana kwenda kortini kumtetea huyu Prof.
 
Balozi Dk Wilbroad Slaa anatarajiwa kuongoza kongamano la tafakuri tunduizi ya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha hayati John Pombe Magufuli.

Kongamano hilo litakalofanyika Ijumaa Machi 25, mwaka huu katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Mwanza pia linalenga kufanya tafakuri ya miaka sita ya utekelezaji wa falsafa aliyoitumia hayati Magufuli wakati akiomba ridhaa ya kuiongoza nchi 2015.

Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake, Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Mwanza, Profesa Costa Mahalu ametaja wazungumzaji wengine katika kongamano hilo kuwa ni Mbunge Mstaafu wa Bariadi Mashariki, John Shibuda na Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Profesa Costa Mahalu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Mwanza.

Wengine ni wahadhiri na watafiti wabobezi wa Historia na Uchumi katika chuo hicho, Profesa Mihanjo Eginald na Dk Anne Gongwe.

"Wakati wa uchaguzi mwaka 2015, tulisikia CCM ikitumia slogani ya Magufuli for Change huku Chadema ikitumia- Movement for Change, kongamano hili litaenda kutafakari utekelezaji kwa vitendo vya slogan hizo," amesema Profesa Mahalu

Profesa Mahalu amewaomba wasomi, wanataaluma na watanzania kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo ili kutoa mchango wao wakati huu ambao nchi inafanya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha Hayati John Magufuli na mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Ni bora watu kama Tundu Lissu, Vicky Kamata, Zitto Kabwe na Anthony Diallo wakahusishwa na mjadala huu kama kweli tunataka kutenda haki.

Kukusanya akina Dr Slaaa, Costa Mahalu na Musukuma ambao ni wanufaika wa moja kwa moja wa Magufuli kwenda kumsifia ni sawa na kuipaka MARASHI MAITI.

Hivyo Hilo kongamano haliwezi kuwasaidia Watanzania
 
Back
Top Bottom