Pre GE2025 Dkt. Slaa: Minyukano ya kambi za uchaguzi wa Mwenyekiti (Mbowe & Lissu) CHADEMA, sababu ni Mbowe anataka kugombea Urais 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu Gagi,@gagnija,mypic ni kushindwa kuona mbali!,no election ni kitu kisichotekelezeka,utopia!,nguvu itakayotumika kuzuia uchaguzi,ingetumika kujipanga,Chadema ingetusua kwa ulaini kama kuokota dodo chini ya mwembe!。

Nilipokuwa kule,nikaiona fursa,nikaitangaza humu Inawezekana Wamarekani ni wajinga ajabu? Wamemchagua mwanaume na kumtosa Mwanamke. 2025 Watanzania tuchague mwanamke kuonesha tuna akili zaidi yao? kisha nikashauri Kilichotokea Uchaguzi wa Marekani, kinaweza kutokea Uchaguzi 2025?. Tuyatumie matokeo yao kama shamba darasa la 2025 au wao ni wao, na sisi ni sisii?

P
 
Mkuu p hakuna cha fulsa ,acha kutupanga hivi sheria za USA za uchaguzi na Tz mbona ni mbingu na ardhi, hadanganyiki mtu ,no reforms no election
 
Mungu mkubwa. Kama Mbowe angerejea kwenye nafasi yake ya Mwenyekiti wa CDM, kazi ya kwanza ilikua ni "KUMSHUGHULIKIA" TAL, na kwa bahati sote tulishuhudia katika majadiliano yake yote Sultan Mbowe alikuwa akiahidi kazi yake ya kwanza itakuwa ni "kushughulikia wavunja katiba" kwenye chama chake.

Sasa kwisha habari yake, ni kama AMEJIFUKUZISHA mwenyewe.
 
Bwana Paskali sisi sio watoto, upinzani unawezaje "kufanya vizuri" kwenye uchaguzi kupitia mifumo hii tuliyonayo ya CCM?
Uchaguzi mkuu ukifanyika katika mifumo hii hii tuliyonayo, matokeo yake yatakuwa ya HOVYO KABISA kuliko hata yale ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 2024.

Acha utoto.
 
We TAPELI upo?
 
Wakati Dodoma wanajipitisha kugombea urais na kumpa mzee Wasira umakamu mwenyekiti, walijua wameshamaliza kazi kwenye uchaguzi wa chadema, wakijua mtu wao atapita kwa kishindo.

Ilifanyika juhudi kubwa kwa upande wa Lissu kuzuia hujuma zozote ambazo zingefanywa kuvuruga uchaguzi. Ushindi wa Lissu uliwaacha na mshangao mkubwa hadi leo.
 
Kwa kweli ilikuwa ni pigo kubwa sana kwa CCM na magenge yake yote.
 
hisia tupu
 
Mleta mada Umeandika kirefu tuhuma bila chembe ya ushahidi hakikika hata mmoja

Umejaza umbeya wa uswahilini mwanzo hadi mwisho
Nimekuwekea mpaka video za wahusika wakisema maneno yao...

Lakini cha ajabu wewe huoni wala kusikia...!!
 
Mleta mada Umeandika kirefu tuhuma bila chembe ya ushahidi hakikika hata mmoja

Umejaza umbeya wa uswahilini mwanzo hadi mwisho
Nimekuwekea mpaka video za wahusika wakisema maneno yao...

Lakini cha ajabu wewe huoni wala kusikia...!!
 
Uko wapi ndugu RMC.....?

Una maoni yoyote au umelowa na umeamua kulamba vumbi moja kwa moja...?

Umeshajiunga na NO REFORMS, NO ELECTION; Tone Tone pamoja NA MIMI NIMO...?

Pole sana brother...
 
Uko wapi ndugu RMC.....?

Una maoni yoyote au umelowa na umeamua kulamba vumbi moja kwa moja...?

Umeshajiunga na NO REFORMS, NO ELECTION; Tone Tone pamoja NA MIMI NIMO...?

Pole sana brother...
Katika uchaguzi kuna kushinda na kushindwa.

Lissu amemshinda Mbowe kwa margin ndogo ta kura 31.

Mbowe bado atabaki kuwa kiongozi bora aliyeijenga CDM.

No reform no election siwezi kujiunga nayo na mwisho wa hiyo slogan ni October 2025. Uchaguzi utafanyika kama kawIaida. Hata wewe hapo hautatoka nje ya key board kwenda kuzuia uchaguzi.
 
Kazi yangu ni kukumbusha tu. Hivyo, nitakukumbusha wakati wake ukifika...

Nevertheless, nimependa hoja yako Moja. Kwamba, kwenye uchaguzi kuna kushindwa au kushinda no matter the margin difference ya kura. Ushindi ni ushindi tu, au siyo ndugu RMC...?

Kikubwa na muhimu ni wapiga kura, mshindi na mshindwa waridhike na mchakato mzima wa uchaguzi kuwa, huu kweli ulikuwa uchaguzi huru, wa wazi na wa haki. Bila shaka kwa hili, tunakubaliana wote. Na kwa hhakika uchaguzi wa CHADEMA wa 21. 01. 2025 ulibeba sifa hizi zote ndiyo maana hakuna malalamiko....

Tuje kwa hoja na dhana nzima ya movement ya NO REFORMS, NO ELECTION inayoongozwa na CHADEMA...

Wewe unaonaje chaguzi za nchi hii? Kwanini zisifanyike kama huu wa CHADEMA tunaousifia? Huoni kuwa chaguzi za Tanzania zinaweza tu kuwa HURU, za HAKI na za WAZI iwapo tutakuwa na sheria na utaratibu mzuri wa kuzisimamia? Au wewe unaona mambo ni mazuri tu na chaguzi zetu Tanzania hazina shida yoyote...?

Hapa ninachotaka ujue ni kuwa hakuna anayesema kuwa uchaguzi hautafanyika..

No Reforms, No Election haina maana ya "uchaguzi usifanyike..."

Maana yake ni kuwa, tufanye uchaguzi lakini baada ya reforms kadhaa muhimu za kisheria na kikatiba kufanyika ili kuruhusu chaguzi Huru, za Wazi na za Haki kufanyika hapa Tanzania...

Na sababu ya kila mtu kutaka mabadiliko haya ni ili wewe RMC kura yako iwe kwenye hesabu na ihesabiwe kwani as for now, viongozi tulionao wanaongoza serikali kuu na za huku chini hawakutokana si ridhaa ya wananchi, Bali wamepachikwa tu....

Hawatukuwachagua, wako pale kwa chaguzi ambazo ni rigged and manipulated. Hii maana yake kura yangu na ya kwako chini ya mfumo huu wa chaguzi hata ukienda kupiga kura kuchagua kiongozi umtakae, haina maana wala thamani yoyote. Hebu nijibu toka moyoni mwako, kwamba, hivi ndivyo unavyotaka iwe...?

Kwa hiyo kubwa kuliko yote tunataka ,fumo wa kutupatia viongozi wa serikali waliochaguliwa kwa kura za wananchi si kama ilivyo sasa...!

Wewe hutaki hayo? Wewe hupendi na hutaki uchaguzi HURU, wa HAKI, na ulio WAZI? Ina maana hupendi haki na badala yake unapenda dhuluma ndugu RMC..?

Kwa hiyo hakuna asemaye tusiwe na uchaguzi kabisa. Uchaguzi utafanyika lakini si lazima iwe Oktoba, 2025 iwapo reforms tunazotaka hazitakuwa zimefanyika...

Uchaguzi mkuu utafanyika tu hata kama ni mwakani 2026 au 2027 only after all necessary legal and constitutional reforms are made...

Do you now understand? Do you agree that, as it stands now, free, fair and transparent elections in our country are absolutely impossible?

If you agree, why then hesitate to support this very crucial movement of NO REFORMS, NO ELECTION by CHADEMA in order to put pressure on the rulers to accept changes..?

And remember, the changes/reforms we all demand are for the benefits of all us as a nation, our children and the entire coming generations...

HAKI HUINUA TAIFA..
 
Japo sikubaliani na wewe katika baadhi ya hoja ulizozieleza lakini nakiri kuwa umejitahidi kujenga hoja objectively.

Mimi huwa siku zote nachangia hoja objectively siyo subjectively.

Nimekuwa nikishiriki uchaguzi tangu mwaka 1985 na sijawahi kukosa kupiga kura na mwezi oktoba 2025 nitapiga kura.

Ninafahamu kuwa uchaguzi wa mwisho katika nchi hii ulifanyika mwaka 2015 japo haukukidhi viwango kwa asilimia 100 lakini walau matokeo ya kura kwa kiasi kikubwa yaliamua nani awe mbunge/ diwani japo kwa urais ilipangwa. Mwaka 2019, 2020, 2024 hakukuwa na uchaguzi bali maigizo na ilipangwa nani awe mbunge , diwani na kura za urais zilipangwa.

Ninahisi pia 2025 yatajirudia yaleyale. Kwa nini ninashiriki? Mungu anataka tutmize wajibu wetu ndipo tumuombe msaada. Najua kura yangu inaweza isiheshimiwe lakini nikimlilia Mungu akiamua anaweza kunisaidia kwa sababu nilitimiza wajibu wangu

No reform no election haiafanikiwa.
Katiba na sheria za kweli na za haki haziwezi kupatikana kwa aina hii ya watu waliopo. Watanganyika hawa ambao tangu asubuhi hadi usiku wanachajadili Simba na yanga, mapenzi na umbea ndio washinikize no reform no election? Rejea nchi kama Kenya, Benin na nchi zingine katiba zao zilipatilanaje Kenya kwa mfano kila mwanasiasa ana watu na anajua idadi yake ndio maana hata kukaa mezani kupanga inawezekana. Juzi hapa Ruto baada ya kuona amekosana na Gachagua aliyekuwa makamo wake na pia amekosana na Kenyatta, akajua fika kariba nusu ya kura alizopata hatazipata mwaka 2027 hivyo ameingia makubaliano na Raila ambaye ana kura milioni kadhaa za wajaluo. Hivyo wajaluo kama kabila la tatu kwa ukubwa na Wakalenjini kama kabila la kwanza wakijumlisha kura zao zitafikia nusu na wakiongezea na za wanasiasa wa makabila mengne ana uhakika wa ushindi. Japo mwaka 2027 bado haujafika lakini kwa hesabu za mezani Ruto au mtu yeyote mfuatiliaji anaweza kukwambia Ruto atapata kura ngapi. Basis ya hii yote ni kwa sababu Kenya wanasiasa wana watu nyuma yao.

Hapa Tanzania huwa nasema mwanasiasa pekee aliyekuwa na watu ni maalim Sefu na Nyerere basi. Kwa sasa si CCM wala upinzani hakuna mwanasiasa binafsi mwenye watu. Maalim Sefu kwa zanzibar alikuwa na watu karibia nusu ya pupalation na nusu ya wapiga kura ( laki mbili hivi) na alikuwa na uwezo wa kuwaingiza barabarani. Kama isingekuwa support ya Tanganyika CCM ya Unguna ingelazimika kukubaliana na matakwa ya wazanzibari na ndiyo sababu pekee inayofanya CCM UNGUJA iuhitaji muungano. Kama zanzibar ingekuwa,nchi huru siku nyingi wazanzibari wangekuwa na katiba mpya na sheria mpya na za haki za uchaguzi.

Wakati Mbowe alilpoitisha maandamano yaiyoshindwa, wakati wa uchaguzi wafuasi wa Lissu walimtukana kuwa watu hawajitokezi sababu wamemstukia ni pandikizi. Sasa tusubiri Lissu aitishe maandamano ya no reform no election tuone kama mtajitokeza hata wewe hautaingia barabarani.

CDM wanajidanganya kuwa watarally support ya vyama vingine. Kwanza nje ya CDM vyama vingine vyote vilivyo upinzani ni CCM B. ACT kwa mfano wao wanaendelea kuandaa wagombea huku wakiwahadaa kuwa wanapogania sheria za uchaguzi zibadilishwe. Oktoba watashiriki uchaguzi na watagawiwa baadhi ya viti vya ubunge na udiwani pamoja na vyama vingine ili kuleta taswira ya kuendelea kuhadaa dunia kuwa uchaguzi ulkuwa huru.

Katika. mazingira haya ya watu waliolala usingizi ni afadhali kushiriki uchaguzi kuliko kususia.

Hoja yenu ya no reform no election Ingeweza kufanikiwa kama mmgekuwa na watu. Viongozi wa CDM ghafla hawawajui watanganyika?

Kitakachotokea oktoba 2025 itakuwa ni aibu na failure kubwa kwa Lissu, CDM itakuwa haina ruzuku, itakuwa imethibitika haina watu, haitakuwa na mbunge wala diwani.

Oktoba 2925 sio mbali tusubiri tuone.

Nb, CCM wanajua fika wakiruhusu uchaguzi hata walau ule wa kiwango cha mwaka 2015 wataambulia kura zisizozidi asilimia 65 na hata chini ya hapo. Wanaweza kupoteza ubunge kwa hadi asilimia 45. Hivyo kutegemea itaruhusu shinikizo tena la kwenye social media ni kujidanganya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…